Vodacom Tanzania: Support thread (Maswali, malalamiko na Ushauri)

Promosheni ya vodacom gawio tangu ianze nimepokea 750 tu,sijajua wanatugawia kama zawadi au wanatuenjoy
 
Mi nataka waje tupeane mkataba rahisi wajenge mnara huku kwetu maana watumiaji ni wengi na minara iko miwili. Net haiko strong sana muda mwingine. Ila wako vzr kwenye speed ya 3G
 
Hivi hizi line za Wakala Mpesa Zanzibar kuzipata ni miongo mingapi? maana wanasema km unataka kukodi fremu.. bora usubir !?!
 
Kipindi hiki Tabata Aroma Dar Es Salaam mtandao wa vodacom kenge sana... sometimes unaambiwa no network kabisa....internet ni kenge kabisa... zamani hata mechi nilikuwa naweza kustream lakini zaizi ni balaa.. sijui ni kwani nini? ukitumia line ya halotel unapata internet vizuri tuu lakini hawa voda hamna kitu..
 
Vodacom ni waongo wa kutupwa. Au vijana wao ni wezi? Waliniandikia msg kwamba ndani ya siku 45 nitapata bonus ya sh.4,890. Juzi wameniwekea sh 250 tu kwenye MPesa. Ni wezi au waongo or both
 
Nliwahi kusema Adui Mkuu wa maendeleo ya digital hapa bongo ni TCRA. Makampuni ya Simu yanawaibia Raia fedha kila sekunde ila wao wamelifumbia macho swala hili. Ifike pahala sasa TCRA ifumuliwe yote na Kuundwa upya Pengine tutapata ahueni
 
Nimetumia voda tangu mwaka 2004, kasi ya internet naiona iko vizuri kinachonikwaza, unapotuma pesa makosa ni yenu ya kimtandao mnatuwajibisha wateja wenu pesa ikae masaa 72 , hii sio sawa tafuteni ufumbuzi wa hili jambo jamani.
 
Kumekuwa na malalamiko mengi mitandaoni kuwa Makampuni ya Mitandao ya simu hasa Tigo na Vodacom kuwa na tabia ya kutoa vifurushi vya data ambavo haviendani na jinsi wanavyokuwa wakionesha kwenye menu zao.

Kwa mfano unanunua kifurushi chenye 1024Mb lakini unatumia 700, bundle linaisha.

Sasa kwa kanda ya ziwa kuna bundle za vodacom ambazo ni maalumu kwa watu wa kanda ya ziwa kama Mwanza, Kagera na Musoma.
072cbe504c26c6ca5d6cc85408525b31.jpg


Ukiangalia kwenye menu kuna kifurushi number 3 ambacho mnunuzi anapewa Mb 150 na Fb bure. Mteja akimaliza kununua hiki kufurushi anapata tex inayomuambia kuwa amepata mb 70 tu na FB bure.
fd137aabcfb19527329f598b66ca843d.jpg


Huu ni Wizi kweupe kabisa. TCRA SHUGHULIKIA HAWA WATU
 
Tcra iko kwenye cyber crime tu. Wao wakishatoa leseni hawajali tena maana wanajua watapata kodi. Chukulia local channel,chukulia malalamiko ya makampuni hayo ya simu
 
Mimi juzi nimenunua bundle la 1024GB kwabahati mbaya umeme haukuwepo, simu iliisha chaji kukiwa na 900 MB, niliwasha simu dakika 10 kabla ya bundle kukata ili niupdate so ningekua na bundle ya 1924GB.

Dakika kumi nzima mtandao ulikua unasumbua lakini ilipoingia sms ya ndg mteja kifurushi chako..... Menu ikafunguka. Nilitamani kupasua simu
 
Back
Top Bottom