Bavaria
JF-Expert Member
- Jun 14, 2011
- 53,092
- 53,568
hilo ndio agizo la kutenganisha data na vifurushi vya maongezi. mfano wake chukulia muda wa maongezi ni kuku na data ni chips halafu serikali ipige marufuku chips kuku, ili upate chips kuku inabidi ununue chips kivyake (data) na kuku kivyake (maongezi). ila kwa huruma zao wauza chips(mitandao) waamue ukinunua kuku wanakuekea na vibale kidogo vya chips (mb 8).
mi nataka tu nijue hekima ya TCRA walioitumia hadi kuamua wavitenganishe hivi vifurushi.
Hilo wazo lilitolewa na hiyohiyo mitandao ya simu. Dhumuni kubwa ni kumaxmize profit. Wauze chips tofauti na kuku.