Kwa lugha fupi halotel wana advantage sana ukilinganisha na kina voda, tigo n etc, ngoja nidadavue kidogo kuna njia kuu tatu za uunganishwaji ya hii minara ya simu mpaka kumfikia mtumiaji wa mwisho na simu, tablet au kifaa chochote, kuna copper cables, microwave, optic fiber kati ya hizi tatu njia yenye gharama nafuu kabisa ni microwave, na ya juu kabisa ikiwa ni optic fiber. Tukirudi kwa kampuni kama voda na tigo uunganishwaji wa mitandao yao kote nchini ni kwa njia ya microwave na optic fiber, optic fiber ikitumika kwenye masafa marefu kuunganisha hub mbali mbali, mfano dar-moro, moro-dom ila wakishafika iwe dom, moro na kwingineko microwave backhaul hutumika kwa hiyo katika mkoa mmoja wapo minara mingi kama sio yote itaendeleza muunganisho wa mtandao husika wirelessly, kwa hiyo minara ya voda ina majukumu mawili kutoa muunganisho kwa mteja (wirelessly) na kwa minara iliyo karibu yake hivo hivo (wirelessly) lakini hii ni tofauti kwa halotel minara yao yote imeunganishwa na Optic fiber kwa hyo kazi ya minara yao ikibaki kutoa muunganisho kwa wateja wa mwisho tu (wirelessly)[na ndio maana minara yao inaonekana midogo kwasababu kazi kubwa imebebwa na optic fiber] , kama inavyofahamika optic fiber ina advantage kubwa ukilinganisha na microwave kwanza ina kinga dhidi ya interference mbalimbali, kama hali ya hewa, electrical, mechanical(vibrations), Bandwidth kubwa, speed na nyingine kedekede kwa hiyo tutegemee huduma nzuri kutoka kwa hawa jamaa, kuna sehemu mvua ikinyesha tu simu hazitoki haya yote yatasahaulika.