Viva viettel (halotel)

Viva viettel (halotel)

kesho kutwa wanazindua officially halo tel. line yangu ya vodacom naitupia,kapuni
 
nipo kijijini natumia modem ya halotel iko faster balaa yaani naangalia movie online
 
Chief-Mkwawa hivi data roaming ikiwa checked ktk setting inasaidia nn.?!

roaming inasaidia kama mtandao wako wa simu haupo hilo eneo upate mtandao mwengine wa patner wao. mfano umetoka Tanzania umeenda Kenya na line ya Vodacom, kufika kenya hakuna network ya Voda line yako itaconect na mtandao wa Safaricom hio ndio roaming. ila sometime huwa wanakata hela nyingi ukifanya roaming kama hizo za nje ya nchi.
 
Last edited by a moderator:
Wameshapanga vifurushi vyao viko tofauti kidogo na mitandao mingine.
 
Nothing new

Sijashawishika bado. Vifurushi havitofautiani na walio tangulia
 
Nothing new

Sijashawishika bado. Vifurushi havitofautiani na walio tangulia

dah.., kwa vifurushi vile asee kweli bado wanasafari ndefu kuwashawishi watu waondoke voda, tigo na airtel
 
roaming inasaidia kama mtandao wako wa simu haupo hilo eneo upate mtandao mwengine wa patner wao. mfano umetoka Tanzania umeenda Kenya na line ya Vodacom, kufika kenya hakuna network ya Voda line yako itaconect na mtandao wa Safaricom hio ndio roaming. ila sometime huwa wanakata hela nyingi ukifanya roaming kama hizo za nje ya nchi.

Shukrani kwa ufafanuzi murua wa kuelimishana..
 
Kwa lugha fupi halotel wana advantage sana ukilinganisha na kina voda, tigo n etc, ngoja nidadavue kidogo kuna njia kuu tatu za uunganishwaji ya hii minara ya simu mpaka kumfikia mtumiaji wa mwisho na simu, tablet au kifaa chochote, kuna copper cables, microwave, optic fiber kati ya hizi tatu njia yenye gharama nafuu kabisa ni microwave, na ya juu kabisa ikiwa ni optic fiber. Tukirudi kwa kampuni kama voda na tigo uunganishwaji wa mitandao yao kote nchini ni kwa njia ya microwave na optic fiber, optic fiber ikitumika kwenye masafa marefu kuunganisha hub mbali mbali, mfano dar-moro, moro-dom ila wakishafika iwe dom, moro na kwingineko microwave backhaul hutumika kwa hiyo katika mkoa mmoja wapo minara mingi kama sio yote itaendeleza muunganisho wa mtandao husika wirelessly, kwa hiyo minara ya voda ina majukumu mawili kutoa muunganisho kwa mteja (wirelessly) na kwa minara iliyo karibu yake hivo hivo (wirelessly) lakini hii ni tofauti kwa halotel minara yao yote imeunganishwa na Optic fiber kwa hyo kazi ya minara yao ikibaki kutoa muunganisho kwa wateja wa mwisho tu (wirelessly)[na ndio maana minara yao inaonekana midogo kwasababu kazi kubwa imebebwa na optic fiber] , kama inavyofahamika optic fiber ina advantage kubwa ukilinganisha na microwave kwanza ina kinga dhidi ya interference mbalimbali, kama hali ya hewa, electrical, mechanical(vibrations), Bandwidth kubwa, speed na nyingine kedekede kwa hiyo tutegemee huduma nzuri kutoka kwa hawa jamaa, kuna sehemu mvua ikinyesha tu simu hazitoki haya yote yatasahaulika.

Usitukane mkunga na uzazi ungalipo!
 
airtel sitoki ila netwerk yao iko poa sana hawajanivuta kwa ghalama nafuu airtel tu
 
Unaweza kutuwekea hapa hivyo vifurushi vyao.

nimeviangalia havina tofauti yoyote na tigo
ndo vile vile tu zikitofautiana ni mb chache na
wameiga kale ka katabia ka tigo kusema
kifurushi ni unlimited kumbe wanamaanisha
unlimited speed. kwa faida ya wengine
internet siku
-sh 250 utapata mb 50
-sh 500 utapata mb 200
internet wiki
-sh 2000 utapata mb 400
-sh 3000 utapata mb 600
internet mwezi
-sh 2000 utapata mb100
-sh 5000 utapata 1gb
-sh 10,000 utapata 3gb
vifurushi hivyo hapo juu hawajasema kitu,
kuna vifurushi ambavyo wanaviita unlimited
-sh 1000 utapata mb800 kwa siku
-sh 5000 utapata gb 1 kwa siku
-sh 15,000 utapata gb 2 kwa mwezi
-sh 25,000 utapata gb 5
mpaka hapo juu tayari wameshafeli, mtandao
mpya ila vifurushi bora ya hao wa zamani.
vifurushi vya maongezi
hapa pia hamna jipya, labda hizo mb
kuongezeka toka mb1 hadi 3
1. vya siku
-sh 400 unapata dk 6 sms 50 na mb3
-sh 600 unapata dk 12 sms 500 na mb5
-sh 800 unapata dk19 sms 1000 na mb8
2. vya wiki
-sh 2000 unapata dk30 sms 300 na mb60
-sh 4000 unapata dk 100 sms 1000 na mb60
-sh 10000 unapata dk 200 sms 1000 na mb60
*aliepanga hivyo vifurushi pia hakutumia akili
hapa ukijiunga vifurushi viwili vya wiki vya
4000 kwa jumla ya 8000 unapata dk200 sms
2000 na mb120 ambazo ni nyingi kuliko
kifurushi cha 10,000 kwa wiki. hivyo kifurushi
cha 10,000 ni useless
3. vya mwezi
-sh 10,000 unapata dakika 160 sms 1500 na
mb80
-sh 15,000 unapata dakika 300 sms 2500 na
mb 300
-sh 20,000 unapata dakika 400 sms 3500 na
mb 300
-sh 30,000 unapata dakika 550 sms 5500 na
mb 500
-sh 50,000 unapata dakika 1000 sms 3000 na
gb 1
*hapa pia ukinunua vifurushi viwili vya 15,000
unapata dakika 600, sms 5000 na mb 600
ambavyo ni vingi kuliko kifurushi cha 30,000
hivyo inafanya hicho kifurushi kisiwe na
maana.
*hivyo hapo juu ni vifurushi vya mitandao yote
mi si mpiga simu sana hivyo siwezi coment.
nimependa tu hawa jamaa wamekuja
kutukumbusha basi letu jekundu liliopinduka
zamani
je unafkiri Halotel wameleta mabadiliko?
 
Shukrani kwa ufafanuzi mkuu, naona watu wa Internet tunazidi kuumizwa tu.

Hapo bado hawajanishawishi hata kidogo labda sijui kwenye speed.!
 
Back
Top Bottom