Watoto ndo wanarudi likizo
Swalehe hapa karudi kawa wa 34 namwuliza imekuwaje umeporomoka toka namba moja ananambia
Baba kwani elfu moja na elfu kumi ipi kubwa nkamjibu elfu kumi
Akanambia Basi sawa mzee , Mimi ndo namba kubwa hapo kuliko wote

na kuliko pacha wake Micaela (yeye kawa wa tano )nmeshindwa kumjibu chochote maana Kuna homework alileta akakosa zote nlifanya nae kwenda shuleni wakamwambia wewe na baba yako wote wajinga

Nmewaacha na ugomvi hapa yeye na dada ake waamue nani ana namba kubwa
Wewe umekutana na kituko gani ?