Vituko mitandaoni. Tupia chako

Vituko mitandaoni. Tupia chako

πŸ˜œπŸ˜œπŸ˜œπŸ˜œπŸ˜œπŸ˜œπŸ˜œπŸ˜œπŸ˜…πŸ€£πŸ€£πŸ€£

1684440553483.jpg
 
JK ana wake wawili?

JK aliendaga kwa Dr. Sebi kabla Dr. Sebi hajauliwa. Ile tezi dume ilimtingisha kidogo. Huko nadhani alifundishwa siri za Alkaline diet na herbs zenye faida. Nasikia huwa anakunywa maji ya madafu peke yake...na mboga sana na mazoezi. Yuko vizuri kwa kweli!
Heloo.mkuu sorry naomba mdaada cm yangu nikifungua hasa picha hazionyeshi ila zamani nilikuwa nikifungua zinafunguka sijajua km.kuna mfumo mpya hapa jf au application gani nitumie niweze kuona picha cm yangu ni Samsung A 11
 
Heloo.mkuu sorry naomba mdaada cm yangu nikifungua hasa picha hazionyeshi ila zamani nilikuwa nikifungua zinafunguka sijajua km.kuna mfumo mpya hapa jf au application gani nitumie niweze kuona picha cm yangu ni Samsung A 11 mdaada please
Kuna hiyo shida kwa wote kwa baadhi ya picha kutoonekana! Ukijitaji kuona picha na hazifunguki tumia browser utaziona bila shida
 
Fuata maelekezo ya Melo hapa chini. Inavyoonekana ile app ya zamani wameamua kuitelekeza japo hawataki kusema. Ingependeza tu hata waiondoe huko Playstore maana kama wameitelekeza itakuwa rahisi sana kudukuliwa...

Shida ya hii app mpya haina mzuka sana kama hii ya zamani.
 
Babu yenu ngoja nijaribu.

Katika stesheni nyingi matangazo ya hali ya hewa huja mwishoni kabisa mwa taarifa ya habari. Wakati huu watazamaji wanakuwa wameshapata habari zote muhimu na kuna uwezekano mkubwa wa watazamaji wengi kutoangalia sehemu hii ya mwisho.

Wakati huo huo sehemu hii ndiyo ina matangazo ya kumalizia malizia. Wanasaikolojia wanaamini kuwa binadamu hukumbuka zaidi taswira anazoziona mwishoni mwishoni mwa tukio kwa hivyo matangazo haya ya mwisho wa taarifa ya habari (hasa nyakati za jioni ambayo ni prime time) huwa yanagombaniwa na ni ghali sana hivyo ni sehemu mojawapo nzuri ya vituo vingi kujipatia pesa ya kueleweka. Ndiyo maana hutafutwa kila njia ili kuwafanya watazamaji wabakie wakiangalia sehemu hii ya mwisho.

Njia mojawapo ni kuweka hawa watangazaji wa kike walimbwende sana sana, wenye bashasha na wanaojua kuvaa, kurembua, kutabasamu, kucheka vizuri; na kuchomekea viutani vya hapa na pale ili tu kumpumbaza mtazamaji abakie akiangalia. Wanaume wengi kuanzia miaka 18-60 watabakia ili kumwangalia mtangazaji anavyoonekana siku hiyo pamoja na mbwembwe zake; na wanawake 18-45 hivi watabakia kuangalia fasheni mpya ya nguo atakayokuwa amevaa siku hiyo, jinsi alivyosuka nywele zake, chain aliyovaa shingoni, lipstick na hata rangi za kucha na kope. Na makampuni mengi ya nguo hutumia nafasi hii kutoa nguo zao bure ili zivaliwe na watangazaji hawa kwa ajili ya kutambulisha fasheni zao mpya. Ukiangalia kwenye credits utaona "meteorologist fashion by Dudubaya Fashion Limited"

Chunguza vizuri utaona. Matangazo kibao...mtangazaji anajichekesha chekesha linachomekewa tangazo jingine halafu utasikia "when I come back, I will tell you about the weekly forecast" halafu mnapigwa matangazo mengine ya kufa mtu....Ukimwangalia kavaa kigauni cha kubana, kifuani cleavage safi, usoni ameiva yaani unaweza kujikuta mnara unasoma hata kama unaambiwa kesho kuna kimbunga na dhoruba kali

Ni marketing strategy....

View attachment 2625288
View attachment 2625291
View attachment 2625293
Mkuu!Mbona wa local channels hujaweka hapo!?
 
Back
Top Bottom