Hivi kwanini vipindi vya weather huko nje wanapenda kutumia warembo sana?pamoja kwa kwamba kwenye television warembo ni kawaida ila kwenye weather forecast wanaweka warembo zaidi?
Ok mkuu,hili swali huwa najiuliza sana sipati jibu
Babu yenu ngoja nijaribu.
Katika stesheni nyingi matangazo ya hali ya hewa huja mwishoni kabisa mwa taarifa ya habari. Wakati huu watazamaji wanakuwa wameshapata habari zote muhimu na kuna uwezekano mkubwa wa watazamaji wengi kutoangalia sehemu hii ya mwisho.
Wakati huo huo sehemu hii ndiyo ina matangazo ya kumalizia malizia. Wanasaikolojia wanaamini kuwa binadamu hukumbuka zaidi taswira anazoziona mwishoni mwishoni mwa tukio kwa hivyo matangazo haya ya mwisho wa taarifa ya habari (hasa nyakati za jioni ambayo ni prime time) huwa yanagombaniwa na ni ghali sana hivyo ni sehemu mojawapo nzuri ya vituo vingi kujipatia pesa ya kueleweka. Ndiyo maana hutafutwa kila njia ili kuwafanya watazamaji wabakie wakiangalia sehemu hii ya mwisho.
Njia mojawapo ni kuweka hawa watangazaji wa kike walimbwende sana sana, wenye bashasha na wanaojua kuvaa, kurembua, kutabasamu, kucheka vizuri; na kuchomekea viutani vya hapa na pale ili tu kumpumbaza mtazamaji abakie akiangalia. Wanaume wengi kuanzia miaka 18-60 watabakia ili kumwangalia mtangazaji anavyoonekana siku hiyo pamoja na mbwembwe zake; na wanawake 18-45 hivi watabakia kuangalia fasheni mpya ya nguo atakayokuwa amevaa siku hiyo, jinsi alivyosuka nywele zake, chain aliyovaa shingoni, lipstick na hata rangi za kucha na kope. Na makampuni mengi ya nguo hutumia nafasi hii kutoa nguo zao bure ili zivaliwe na watangazaji hawa kwa ajili ya kutambulisha fasheni zao mpya. Ukiangalia kwenye credits utaona "meteorologist fashion by Dudubaya Fashion Limited"
Chunguza vizuri utaona. Matangazo kibao...mtangazaji anajichekesha chekesha linachomekewa tangazo jingine halafu utasikia "when I come back, I will tell you about the weekly forecast" halafu mnapigwa matangazo mengine ya kufa mtu....Ukimwangalia kavaa kigauni cha kubana, kifuani cleavage safi, usoni ameiva yaani unaweza kujikuta mnara unasoma hata kama unaambiwa kesho kuna kimbunga na dhoruba kali


Ni marketing strategy....