Vita kubwa ya maneno inayoendelea kati Lema Vs Zitto Kabwe

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Feb 7, 2022
2,308
5,460
Wanasiasa wawili maarufu, Godbless Lema ambaye aliwahi kuwa Mbunge wa Arusha Mjini kwa tiketi ya Chadema, na Zitto Kabwe, kiongozi wa ACT Wazalendo wameingia katika vita ya maneno.

Kupitia akaunti yake ya mtandao wa kijamii wa Twitter, Lema ameandika ujumbe ambao bila kumtaja mtu jina, unamuelezea kijana mmoja ambaye amefananisha na Mwenyekiti wa TLP, Augustino Mrema.

Lema ameandika: “Kuna Kijana mmoja ana-behave na anataka aonekane kama mpinzani wa kweli huku kimsingi yeye ni kama Mrema wa TLP lakini yeye akiwa mchangamfu zaidi.”

Muda mfupi baada ya kupost ujumbe huyo, Zitto Kabwe akaibuka na kuja kuujibu ujumbe huo chini yake, akiandika: “Kijana huyo ndiye aliyekutoa wewe kwa Mrema ukaingia ulipo sasa mwaka 2007. Kijana huyohuyo kwa kushiriakiana na wadau wakiwemo viongozi wako wa sasa ndiyo wataweka mazingira mazuri ya siasa. Endelea wailing sisi tunakuwekea mazingira mazuri ya kufanya siasa.”

Baada ya Zitto kujibu ujumbe huo, wachangiaji wengi wa mitandaoni wakaunganisha picha na kugundua kwamba kumbe aliyelengwa na Lema japokuwa hakuwa amemtaja jina, ni Zitto.

Zitto ni miongoni mwa viongozi wa upinzani ambao wapo katika kamati maalumu iliyoundwa na Rais Samia Suluhu Hassan ya kupitia hoja zilizojitokeza katika mkutano wa wadau wa siasa na vyama uliofanyika mwishoni mwa mwaka jana, mkutano ambao Chadema hawakushiriki.
 
Kwa mtazamo wangu Zito ni mwanasiasa na ndio maana alitoka ktk chama kilichomkuza na bado yupo hewan lkn Lema ni chawa wa mwanasiasa akitoka nje ya chama kilichomlea ataishia km Kafulia na wengineo ambao tumeshawasahau.


Na kuhusu unafki,uongo,umbea,majungu na mengineyo huo ndio msingi wa wanasiasa sidhan km kuna mwanasiasa asiyekuwa na sifa hizo
 
Naamini watu wengi hawamuelewi Zitto Kabwe ni mwanasiasa wa aina gani. Wengi sana hasa mashabiki wa wanasiasa wakiharakati kamwe kumuelewa Zitto Zuberi Kabwe Ruyagwa ni ngumu sana

Lema angekuwa Mwanasiasa wa kweli mfia demokrasia wa nchi yake asingekimbia vitisho hewa.

Lema si wakulinganishwa na Zitto hata kidogo.
 
Wanasiasa wanapiga Siasa hakuna Jipya....

Ifike wakati wananchi tujitahidi kutenda na kufanya mambo kwa manufaa yetu na kuwakumbusha wanasiasa nani kashika mpini; Blah, Blah, Blah zimekuwa nyingi sana hakuna value for our hard earned cash (kodi)

Siasa imegeuka kuwa mtaji / ajira na sehemu ya kujineemesha
 
Wanasiasa wa bongo Bado Wana utoto sana,kwanini hatijifunzi kutoka kwa kaka zetu Kenya,

Jana miaka mitano iliyopita Uhuru Kenyata alimpiga mabomu ya machozi Odinga na wafuasi wake,wakatukanana matusi kibao,leo Uhuru huyo huyo anampigia Kampeni Odinga awe Raisi ajaye baada yake,amemtosa makamu wake Ruto aliyemsaidia kuingia Madarakani,

Kalonzo musyoka alihapa hata kuja kumsaidia Odinga kwa mala ya tatu kuingia Ikulu,lakini jana amesema Odinga tosha!!

Tukomae jamani,siku Mbowe akiteuliwa kuwa waziri mkuu,na wafuasi wake wakapewa nafasi za wizara na ukuu wa mikoa,inabidi tuone ni kitu Cha kawaida.
 
Back
Top Bottom