Visomo hivi si dalili njema sana

Visomo hivi si dalili njema sana

Ni jambo gumu kidogo kwa wale ambao si waamini. Visomo hivi vimezoeleka kuwa kwenye mambo ya binafsi zaidi. Hili la wiki hii ni kama linaelekea kuwa jambo la kitaifa.

Nimesikia majigambo mengi ya watawala, Nimemuona kwa macho yangu Ndugai akisema kwa midomo wake maneno haya CHEZA NA KITU KINGINE SIO NDUGAI. niliogopa sana.

Muda huu alfajiri kuna maombi yanafikia tamati pale kariakoo... Mchungaji kiongozi anataja damu iliyomwagika Tanzania.

Ishu ya kisomo hata kama imekuzwa sana lakini vema watawala wapate ujumbe wa kiroho wenye tafakuri kuu.

Kwamba wananchi wanaona hakuna kimbilio tena na hawana imani na serikali yao, sasa wanapeleka mashtaka yao kwenye NGUVU zisizojulikana. Hata kama visomo hivyo havitaleta madhara tarajiwa lakini ni ujumbe mbaya kwa serikali, kuna kaliba inahisi kuonewa na kunyanyaswa, kuna kaliba inaona wazi kabisa imetengwa na kufanywa yatima.

Energy ya hii kaliba isipuuzwe chondechonde! Tusiwafundishe watu kuacha misingi.

Viongozi na watawala tendeni kwa weledi, tendeni kwa hekima, tendeni kwa tafakuri na maono makuu.Angalieni malalamiko yasiwe mengi mno.

Tumshukuru Mungu wameamua kutumia silaha za maombi na visomo, waacheni msiwazuie. Hawana pengine pa kupumulia, hakuna mikutano ya kisiasa, hakuna kuandamana. Hivi vitu husaidia mno kupunguza nyongo iliyozidi.

Tendeni kwa weledi sana hakukuwa na haja ya kuzuia wachangia damu pale Temeke hospital.. Mambo mengine mbona ni ya kawaida mno?

Kuna ule wimbo wa Ney, ule wa wapo. Baada tu ya Mwakyembe kuruhusu upigwe, haraka sana ule wimbo ukawa sio habari tena!

Visomo hivi ni njia mpya ya kushtua ya kupeleka ujumbe mkubwa.

Visipuuzwe! Visomo vikishindikana hali inaweza kuwa tofauti LAKINI visomo vikijibu hata kama ni coicedence? Tutegemee nini kama taifa?
Mku hata Mzee wetu alifika mahali akapotoa na pale alipokosa marafiki kutokana na jeuri ya mdomo wake.
Ukishakosa marafiki usitegemee kuwa na mwisho mzuri kwani kila mmoja anaongea lake na hapo mabaya ndo mengi.
Uongozi una muda wake kwa hiyo mwisho mzuri ni ulimi wake
 
Hakuna dini hapo usanii Tz na inapangwa Sio eti kwamba Watz wamegusws. Wtz ni wasanii snaa. Wale wa kibiti Maombi gani yalitolewa. "usihukumu na hautahukumiwa@ sasa nani ana uhakika wa haya mambo. Mmekuuwa na majibu ya haraka sna. Kma mmepanga kabisa haya mambo. Ndo mnafanya watu wenye akili wafikirie mbali. Mbona hamkuwahi kusoma kwa wezi wa mali za Taifa kama ndo uzalendo. Usanii huu utawarudia. MUNGU HAJARIBIWI endeleeni tu kuligawa taifa.
Punguza jazba na kuhema kwa spidi, karibu kuelewa concern ya mtoa mada.

Hayajawahi kuzaliwa mapenzi ya kulazimisha. Kama yalitokea Kibiti na hakukuwa na maombi, hakuzuii watu kuomba leo. Kwani ikitokea (Mungu aepushie mbali) Tanga ikakumbwa na tetemeko, wananchi watalaumiwa kwa kulisbabisha? Nina mashaka kama utanielewa
 
Mkuu hua ninakupa respect sna ktk maneno yako na hua sewezi kupingana na wewe lakini najaribu pia kufikili kwa undani na kukumbuka ya nyuma kwa sisi wenyewe wananchi kwamba

1. Ktk nchi hii huko nyuma kidogo tu watu walipiga kelele sana juu ya uongozi wa juu na mambo yanavyokwenda

2. Hawakuishia hapo wakaenda mbele wakisema nchi hii inahitaji uongozi mkali na wenye uthubutu huku wakitoa maneno makali ya kukashifu waliokuwepo ktk kipindi hicho wakisema ni dhaifu na nchi inaibiwa sana kupita kiasi,na kuna watu waliomba kwa MUNGU vivyo hivyo wakisema nchi imekua inaibiwa,vijana wetu wanaangamia kwa madawa ya kulevya na mambo chungu mzima

3. Nina kumbumbuku pia watu wa vyama pinzani walisema maneno mazuri tu kama kuishauli serikali yetu na kupiga kelele sana,jambo ambalo mpaka leo tulipo kuna baadhi ya mambo wananchi tunaona uongozi wa juu ndio unaoshughulika nayo,kwa mfano issue ya madini lakini hapo hapo na wale wale wameanza tena kulaumu na kusema huyu ndugu anatupeleka pabaya kiasi kwamba sisi wananchi tunashindwa hata kujua tunapelekwa wapi na nani tumuamini.

4. Na la mwisho kabisa leo watu tunafanya kisomo na huko nyuma kisomo na maombi yalifanyika kuiombea nchi na uongozi,wenye kuomba mema juu ya uongozi walikuwepo,wenye kuomba mabaya juu ya uongozi walikuwepo pia,sasa hili nalo najikuta nachelea kusema kwamba MUNGU ni wa wote na hujibu kwa kadri ya watu watakavyo.yamkini kuna maombi yalienda mbele sana mpaka yakafika kwa MUNGU kama yale maombi ya kolnerio na sasa MUNGU ameshuka kujibu tulichoomba,leo tena tuombe MUNGU abadilishe uelekeo atatuelewa kweli?

Najaribu kujifikirisha kwa sauti mkuu AKSANTE
Nakubaliana nawe kabisa na tuliposema tunahitaji complete overhaul haikumaanisha kuwe na uonevu na mambo yote yanayotia madoa mekundu ya damu kanzu nyeupe
Kuna mambo machache yanayochafua mazuri mengi yanayofanywa na Bob, pamoja na kwamba hakuna mkamilifu lakini kuna vitu vya kawaida kabisa ambavyo mamlaka zinatetemeka mno vinapofanyika
 
Mkuu mshana jr, umenena vyema sana.

Hawa watawala wanajichanganya sana.

Kama ulivyotoa mfano juu ya Ngoma ya Ney ilipoachia baada ya muda ikapotea.

Kama wangekuwa na akili , wangeacha kutozuia watu kuchangia damu maana lingefanyika kwa muda mfupi na kusahaulika.

Lakini wakizuia ndio wanachochea chuki miongoni mwa jamii.

Serikali haina dini, lakini wananchi wake wana dini, inashangaza serikali ambayo haiamini juu ya Imani inakataza watu wenye Imani kufanya mambo ya Kiimani.

Wanahofia nini hasa!

Dalili ya mvua ni mawingu!!
Wallah akafa mgonjwa kwa kukosa damu ilhali kuna damu ilikataliwa kwa kuwa tu ni ya khaki....
 
Ndio maana ya imani haionekani wala haishikiki na ina nguvu ya kuangusha jabali.
Iman ya mashetan?Hahahaaaaaaaa chama cha albadir kweli mmeishiwa maarifa mmebaki kuamini uchawi na nguvu za giza
 
Ndio maana ya imani haionekani wala haishikiki na ina nguvu ya kuangusha jabali.
Iman ya mashetan?Hahahaaaaaaaa chama cha albadir kweli mmeishiwa maarifa mmebaki kuamini uchawi na nguvu za giza
 
Hakuna dini hapo usanii Tz na inapangwa Sio eti kwamba Watz wamegusws. Wtz ni wasanii snaa. Wale wa kibiti Maombi gani yalitolewa. "usihukumu na hautahukumiwa@ sasa nani ana uhakika wa haya mambo. Mmekuuwa na majibu ya haraka sna. Kma mmepanga kabisa haya mambo. Ndo mnafanya watu wenye akili wafikirie mbali. Mbona hamkuwahi kusoma kwa wezi wa mali za Taifa kama ndo uzalendo. Usanii huu utawarudia. MUNGU HAJARIBIWI endeleeni tu kuligawa taifa.
Vipi wale wanaojazana uwanja wa Taifa eti kuomba Amani uliwahi kuwakumbusha wawaombee wezi wa mali za Taifa? na je vipi na yule anayetaka kila siku watu wamuombee kwa nini asiseme waombewe wezi wa mali za Taifa?
 
Watu wanajisahau kwa kulewa madalaka pasipo kujua ni kido za watanzanua tena wa hali ya chini zinazo walipa wao na kuota mivitambi alafu wanashindwa kuwatumikia maboss wao ila wanamtumikia huyo mungu mtu wao. Yan mungu na ajidhihilishe juu yao kwa njia ya fundisho ili iwe funzo kwa wengne
 
Sahivi hata akifa mtu ni visomo vitasingiziwa. Mawaziri, viongozi, wabunge, matajiri n. k walikuwa wanakufa ila Ole atakaye kufa kuanzia leo atasingiziwa hadi akonde kaburini.
 
Hakuna dini hapo usanii Tz na inapangwa Sio eti kwamba Watz wamegusws. Wtz ni wasanii snaa. Wale wa kibiti Maombi gani yalitolewa. "usihukumu na hautahukumiwa@ sasa nani ana uhakika wa haya mambo. Mmekuuwa na majibu ya haraka sna. Kma mmepanga kabisa haya mambo. Ndo mnafanya watu wenye akili wafikirie mbali. Mbona hamkuwahi kusoma kwa wezi wa mali za Taifa kama ndo uzalendo. Usanii huu utawarudia. MUNGU HAJARIBIWI endeleeni tu kuligawa taifa.
Mmeanza kuogopa naona
 
Uongozi uliopo madarakani kwa sasa Tanzania katika mihimili hasa ya Serikali na Bunge ni wa hovyoo haujawahi kutokea Tanzania tangu ilipopata uhuru. Ni kioja sasa wananchi wanakimbilia kwenye albadili huku viongozi wa mihili hii wakijigamba "Sijaribiwi" na mwingine "chezea ndugai wewe!" . Huu ni ulofa wa uongozi uliopitiliza.
Mimi dua yangu Yohana mvinyo,DAB na Kazi....gai wafe kabla mwaka huu kwisha.
 
"....Hata kama visomo hivyo havitaleta madhara tarajiwa lakini ni ujumbe mbaya kwa serikali, kuna kaliba inahisi kuonewa na kunyanyaswa, kuna kaliba inaona wazi kabisa imetengwa na kufanywa yatima...." (Mshana Jr., 2017).

Umeandika vizuri sana Kiongozi
 
Mleta mada,
Nilikuwa naheshimu michango yako humu JF. Japo mengine yalipingana na Imani yangu ya dini lakini nilivumilia na kuamini ya kwamba wewe ni mtu makini na Mwenye busara.
Sikujua kama wewe ni mpuuzi wa kiwango hiki. Nashukuru kwa kunijulisha hilo.
Mnasambaza chuki na sumu ya ukabila katika Taifa letu. Ila Mungu ni zaidi ya nyinyi na soon ukweli utakuwa upenuni.
Shame on you mchawi kiongozi wa JF.
Umelewa ?
 
Hauna msingi wowote. Wewe ni mkabila na una chuki ambayo inakutafuna ndani kwa ndani. Nashangaa kwa mtu kama wewe kuandika upuuzi kama huu. Umetumwa na nani kutufarakanisha Watanzania!?
Unasikitisha sana kupita maelezo. Sina haja ya kufurahishwa na mtu kama wewe Mwenye mrengo wa chuki na sumu ya ukabila. Ninakemea huu upuuzi kwa nguvu zote na ushindwe pia Ulegee kama mlenda uliotiwa roico.
Jf kuna wagonjwa wa akili wengi hivi kumbe
 
Ni jambo gumu kidogo kwa wale ambao si waamini. Visomo hivi vimezoeleka kuwa kwenye mambo ya binafsi zaidi. Hili la wiki hii ni kama linaelekea kuwa jambo la kitaifa.

Nimesikia majigambo mengi ya watawala, Nimemuona kwa macho yangu Ndugai akisema kwa midomo wake maneno haya CHEZA NA KITU KINGINE SIO NDUGAI. niliogopa sana.

Muda huu alfajiri kuna maombi yanafikia tamati pale kariakoo... Mchungaji kiongozi anataja damu iliyomwagika Tanzania.

Ishu ya kisomo hata kama imekuzwa sana lakini vema watawala wapate ujumbe wa kiroho wenye tafakuri kuu.

Kwamba wananchi wanaona hakuna kimbilio tena na hawana imani na serikali yao, sasa wanapeleka mashtaka yao kwenye NGUVU zisizojulikana. Hata kama visomo hivyo havitaleta madhara tarajiwa lakini ni ujumbe mbaya kwa serikali, kuna kaliba inahisi kuonewa na kunyanyaswa, kuna kaliba inaona wazi kabisa imetengwa na kufanywa yatima.

Energy ya hii kaliba isipuuzwe chondechonde! Tusiwafundishe watu kuacha misingi.

Viongozi na watawala tendeni kwa weledi, tendeni kwa hekima, tendeni kwa tafakuri na maono makuu.Angalieni malalamiko yasiwe mengi mno.

Tumshukuru Mungu wameamua kutumia silaha za maombi na visomo, waacheni msiwazuie. Hawana pengine pa kupumulia, hakuna mikutano ya kisiasa, hakuna kuandamana. Hivi vitu husaidia mno kupunguza nyongo iliyozidi.

Tendeni kwa weledi sana hakukuwa na haja ya kuzuia wachangia damu pale Temeke hospital.. Mambo mengine mbona ni ya kawaida mno?

Kuna ule wimbo wa Ney, ule wa wapo. Baada tu ya Mwakyembe kuruhusu upigwe, haraka sana ule wimbo ukawa sio habari tena!

Visomo hivi ni njia mpya ya kushtua ya kupeleka ujumbe mkubwa.

Visipuuzwe! Visomo vikishindikana hali inaweza kuwa tofauti LAKINI visomo vikijibu hata kama ni coicedence? Tutegemee nini kama taifa?
Ubabe usio na tija..
 
Back
Top Bottom