Hivi mnamuelewa Msemaji wa Serikali, Gerson Msigwa?

Hivi mnamuelewa Msemaji wa Serikali, Gerson Msigwa?

Endasak Masqaroda

JF-Expert Member
Joined
Jun 16, 2013
Posts
1,728
Reaction score
3,957
Habari wana jukwaa.

Moja kwa moja kwenye mada tajwa hapo juu.

Mimi binafsi bwana Endasak, sijawahi kumuelewa Msemaji wa Serikali ya Tanzania. Hivi karibuni ameonekana akizungumza kuwa wanachi waaamue wenyewe kuwasikiliza wanawahamasisha kufanya kazi wapate hela (Rais na viongozi wengine) au kuwasikiliza wanaoomba kuwachangia hata hicho kidogo wanachopata. Hii ni kauli ya kifala sana! Haifai kusemwa na mtu mwenye wadhifa wa msemaji wa Serikali. Au serikali ndio ilimtuma akaseme hivyo?

Wakati viongozi wakuu wa nchi wanahubiri utengamano wa kitaifa, maridhiano, na umoja nchini,yeye huwa anaongea vitu vinavyo wagawa Watanzania. Kuna wakati nawaza au mama alikosea kumteua huyu jamaa? Au ndio madaraka ya kulevya, ameshalewa madaraka sasa amekuwa roporopo anajiropokea tu kama yupo kwao Njombe kwenye kilabu ya pombe za kienyeji?

Kwa Kiswahili cha mtaani tunasema anampigisha shoti Rais wa nchi dhidi ya Wananchi wake. Yaani anamchonganisha tena na kizazi hiki cha Millenials na Gen Z ambao kimsingi wana ufahamu mkubwa na kumbukumbu nzuri sana kuliko kizazi chake kilichopita.

Nimpe taarifa tu bwana Msigwa kuwa Watanzania wa sasa sio wajinga kama anavyodhani. Kama anafikiria hivyo, kuna uwezekano mkubwa mjinga ni yeye lakini kwa bahati mbaya sana hatambui hilo. Lakini taarifa nyingine imfikie, hata CCM ilichangiwa na hao hao Watanzania. Lakini huko aliko, ajiulize hili swali na jibu akae nalo; KWANI YEYE NI MSEMAJI WA CHAMA CHA CCM? Ikikuuma katoe UFAFANUZI kama kawaida yako. Ukikausha baridi tu, lakini ujumbe umefika.

Mimi naamini Rais ana nia njema tu dhidi ya raia wake, lakini watu walio chini yake wa aina ya Msigwa ndio wanamuangausha vibaya mno. Huu sio wakati wa kuropoka ropoka hovyo kama umelewa ulanzi.

Adios!
 
IMG-20260724-WA0031.jpg
 
raisi hana njia njema na wasaidizi wake wanatekeleza matakwa yake

over
Unaona sasa, yale yale ya kuchonganisha rais na raia. Mwehu ndama umeshajionea kuwa rais hana nia njema na yeye Girishoni anatekeleza maagizo.
Kazi ipo.
 
Back
Top Bottom