Visomo hivi si dalili njema sana

Visomo hivi si dalili njema sana

Na wasome tu vitawarudia hiyo ni dalili ya kutapatapa
Kama visomo vingekua vinafanya kazi Sefu angekua madarakani,hakuna serikali inayoanguka kwa visomo,haswa vikiwa vinasomwa na wasanii
 
Mleta mada,
Nilikuwa naheshimu michango yako humu JF. Japo mengine yalipingana na Imani yangu ya dini lakini nilivumilia na kuamini ya kwamba wewe ni mtu makini na Mwenye busara.
Sikujua kama wewe ni mpuuzi wa kiwango hiki. Nashukuru kwa kunijulisha hilo.
Mnasambaza chuki na sumu ya ukabila katika Taifa letu. Ila Mungu ni zaidi ya nyinyi na soon ukweli utakuwa upenuni.
Shame on you mchawi kiongozi wa JF.
 
Watanzania tunafanya mambo kwa ajiri ya wanasiasa na si kwa ajiri yetu sie,tumeweka matumaini kwa wanasiasa.
 
Tulipo fikia wenye akili wanajua tupo pabaya yaani kama ni shetani katuweka chumbani watu wameanza kutokuwa na imani ata na Mwenyezi Mungu na kutafuta nguvu za ziada za kimuungu ukiona hili ujue mioyo ya watu imejaaa maumivu kuna watu wamejisahau na kudhani wataishi milele wamepewa madaraka wakawasahau hata waliowashika mkono Mwenyezi Mungu tusaidie taifa letu lisiangamie
 
Ninakumbuka mwaka 2011 kama sijakosea nilisafiri na Egypt Air na transit yangu ilikuwa Cairo. Ilikuwa ni mwezi December kutokana na sababu mbili tatu nilikuwa a pale kwa siku mbili. Wananchi walinieleza walivyo choshwa na utawala wa upendeleo wa Hussain Mubaraka na walionyesha kukata tamaa ya maisha.

Ni miezi michache tu baadae niliona mabadiliko makubwa ya watu ambao hawakuogopa kifo.
 
Ni jambo gumu kidogo kwa wale ambao si waamini.... Visomo hivi vimezoeleka kuwa kwenye mambo ya binafsi zaidi... Hili la wiki hii ni kama linaelekea kuwa jambo la kitaifa
Nimesikia majigambo mengi ya watawala.... Nimemuona kwa macho yangu Ndugai akisema kwa midomo wake maneno haya.... CHEZA NA KITU KINGINE SIO NDUGAI. niliogopa sana
Muda huu alfajiri kuna maombi yanafikia tamati pale kariakoo... Mchungaji kiongozi anataja damu iliyomwagika Tanzania
Ishu ya kisomo hata kama imekuzwa sana lakini vema watawala wapate ujumbe wa kiroho wenye tafakuri kuu... Kwamba wananchi wanaona hakuna kimbilio tena na hawana imani na serikali yao, sasa wanapeleka mashtaka yao kwenye NGUVU zisizojulikana
Hata kama visomo hivyo havitaleta madhara tarajiwa lakini ni ujumbe mbaya kwa serikali, kuna kaliba inahisi kuonewa na kunyanyaswa, kuna kaliba inaona wazi kabisa imetengwa na kufanywa yatima.... Energy ya hii kaliba isipuuzwe chondechonde! Tusiwafundishe watu kuacha misingi
Viongozi na watawala tendeni kwa weledi, tendeni kwa hekima, tendeni kwa tafakuri na maono makuu... ANGALIENI MALALAMIKO YASIWE MENGI MNO....
Tumshukuru Mungu wameamua kutumia silaha za maombi na visomo, waacheni msiwazuie.. Hawana pengine pa kupumulia, hakuna mikutano ya kisiasa, hakuna kuandamana.... Hivi vitu husaidia mno kupunguza nyongo iliyozidi
Tendeni kwa weledi sana hakukuwa na haja ya kuzuia wachangia damu pale Temeke hospital.. Mambo mengine mbona ni ya kawaida mno?
Kuna ule wimbo wa Ney, ule wa WAPO... Baada tu ya Mwakyembe kuruhusu upigwe, haraka sana ule wimbo ukawa sio habari tena!
Visomo hivi ni njia mpya ya kushtua ya kupeleka ujumbe mkubwa...... Visipuuzwe! Visomo vikishindikana hali inaweza kuwa tofauti LAKINI visomo vikijibu hata kama ni coicedence? Tutegemee nini kama taifa?

Hufikia hatua hii ya kumuachia Mungu atende ni dalili za kuwa watanzania hawana imani tena
 
Mleta mada,
Nilikuwa naheshimu michango yako humu JF. Japo mengine yalipingana na Imani yangu ya dini lakini nilivumilia na kuamini ya kwamba wewe ni mtu makini na Mwenye busara.
Sikujua kama wewe ni mpuuzi wa kiwango hiki. Nashukuru kwa kunijulisha hilo.
Mnasambaza chuki na sumu ya ukabila katika Taifa letu. Ila Mungu ni zaidi ya nyinyi na soon ukweli utakuwa upenuni.
Shame on you mchawi kiongozi wa JF.
Asante kwa kutoa nyongo, siwezi kumridhisha kila mtu kwenye kila mada bali huangalia uhalisia na mtazamo wenye misingi ya kutoa taswira fulani
 
Hakuna dini hapo usanii Tz na inapangwa Sio eti kwamba Watz wamegusws. Wtz ni wasanii snaa. Wale wa kibiti Maombi gani yalitolewa. "usihukumu na hautahukumiwa@ sasa nani ana uhakika wa haya mambo. Mmekuuwa na majibu ya haraka sna. Kma mmepanga kabisa haya mambo. Ndo mnafanya watu wenye akili wafikirie mbali. Mbona hamkuwahi kusoma kwa wezi wa mali za Taifa kama ndo uzalendo. Usanii huu utawarudia. MUNGU HAJARIBIWI endeleeni tu kuligawa taifa.
Kwa hiyo mlimpiga risasi Lissu kwa sababu kule kibiti kuna watu wengine pia wanawapiga risasi RAIA wasio na hatia?
 
Asante kwa kutoa nyongo, siwezi kumridhisha kila mtu kwenye kila mada bali huangalia uhalisia na mtazamo wenye misingi ya kutoa taswira fulani
Hauna msingi wowote. Wewe ni mkabila na una chuki ambayo inakutafuna ndani kwa ndani. Nashangaa kwa mtu kama wewe kuandika upuuzi kama huu. Umetumwa na nani kutufarakanisha Watanzania!?
Unasikitisha sana kupita maelezo. Sina haja ya kufurahishwa na mtu kama wewe Mwenye mrengo wa chuki na sumu ya ukabila. Ninakemea huu upuuzi kwa nguvu zote na ushindwe pia Ulegee kama mlenda uliotiwa roico.
 
Hakuna kitu hapo bana, mm ni Muislam walichofanya kama kisomo wapo kinyume kabisa na uislam, kisomo cha al badr ni ushirikina tena mkubwa hizo ni mbwembwe tu!, yaani mishirikina inawatisha mishirikina wenzakeo ujinga mtupu bora wangesema wanaomba dua, Adui mwombee dua njema huenda atakua mtu mzuri mbeleni au ukishindwa hilo omba dua kisha pigana Vita kavu kavu hill ndo ninalofahamu ktk uislam hakuna msaada isipokua kwa Mungu tu badr si ktk dini yetu ya uislam waache kuisingizia dini yetu na kuichafua wapumbavu wakubwa.
Sasa kwanini serikali inazuwia?
 
Hauna msingi wowote. Wewe ni mkabila na una chuki ambayo inakutafuna ndani kwa ndani. Nashangaa kwa mtu kama wewe kuandika upuuzi kama huu. Umetumwa na nani kutufarakanisha Watanzania!?
Unasikitisha sana kupita maelezo. Sina haja ya kufurahishwa na mtu kama wewe Mwenye mrengo wa chuki na sumu ya ukabila. Ninakemea huu upuuzi kwa nguvu zote na ushindwe pia Ulegee kama mlenda uliotiwa roico.

Mshana Jr,Wapuuzi wengine ni wa ku ignore tu,wala hauna haja ya kuwajibu.Washakula buku saba za Lumumba.
 
Hakuna dini hapo usanii Tz na inapangwa Sio eti kwamba Watz wamegusws. Wtz ni wasanii snaa. Wale wa kibiti Maombi gani yalitolewa. "usihukumu na hautahukumiwa@ sasa nani ana uhakika wa haya mambo. Mmekuuwa na majibu ya haraka sna. Kma mmepanga kabisa haya mambo. Ndo mnafanya watu wenye akili wafikirie mbali. Mbona hamkuwahi kusoma kwa wezi wa mali za Taifa kama ndo uzalendo. Usanii huu utawarudia. MUNGU HAJARIBIWI endeleeni tu kuligawa taifa.
Nimekuelewa sana mkuu.
 
Back
Top Bottom