Visomo hivi si dalili njema sana

Visomo hivi si dalili njema sana

IMG-20170916-WA0085.jpg
 
Ni jambo gumu kidogo kwa wale ambao si waamini. Visomo hivi vimezoeleka kuwa kwenye mambo ya binafsi zaidi. Hili la wiki hii ni kama linaelekea kuwa jambo la kitaifa.

Nimesikia majigambo mengi ya watawala, Nimemuona kwa macho yangu Ndugai akisema kwa midomo wake maneno haya CHEZA NA KITU KINGINE SIO NDUGAI. niliogopa sana.

Muda huu alfajiri kuna maombi yanafikia tamati pale kariakoo... Mchungaji kiongozi anataja damu iliyomwagika Tanzania.

Ishu ya kisomo hata kama imekuzwa sana lakini vema watawala wapate ujumbe wa kiroho wenye tafakuri kuu.

Kwamba wananchi wanaona hakuna kimbilio tena na hawana imani na serikali yao, sasa wanapeleka mashtaka yao kwenye NGUVU zisizojulikana. Hata kama visomo hivyo havitaleta madhara tarajiwa lakini ni ujumbe mbaya kwa serikali, kuna kaliba inahisi kuonewa na kunyanyaswa, kuna kaliba inaona wazi kabisa imetengwa na kufanywa yatima.

Energy ya hii kaliba isipuuzwe chondechonde! Tusiwafundishe watu kuacha misingi.

Viongozi na watawala tendeni kwa weledi, tendeni kwa hekima, tendeni kwa tafakuri na maono makuu.Angalieni malalamiko yasiwe mengi mno.

Tumshukuru Mungu wameamua kutumia silaha za maombi na visomo, waacheni msiwazuie. Hawana pengine pa kupumulia, hakuna mikutano ya kisiasa, hakuna kuandamana. Hivi vitu husaidia mno kupunguza nyongo iliyozidi.

Tendeni kwa weledi sana hakukuwa na haja ya kuzuia wachangia damu pale Temeke hospital.. Mambo mengine mbona ni ya kawaida mno?

Kuna ule wimbo wa Ney, ule wa wapo. Baada tu ya Mwakyembe kuruhusu upigwe, haraka sana ule wimbo ukawa sio habari tena!

Visomo hivi ni njia mpya ya kushtua ya kupeleka ujumbe mkubwa.

Visipuuzwe! Visomo vikishindikana hali inaweza kuwa tofauti LAKINI visomo vikijibu hata kama ni coicedence? Tutegemee nini kama taifa?
Hakika umenena
 
Hakuna dini hapo usanii Tz na inapangwa Sio eti kwamba Watz wamegusws. Wtz ni wasanii snaa. Wale wa kibiti Maombi gani yalitolewa. "usihukumu na hautahukumiwa@ sasa nani ana uhakika wa haya mambo. Mmekuuwa na majibu ya haraka sna. Kma mmepanga kabisa haya mambo. Ndo mnafanya watu wenye akili wafikirie mbali. Mbona hamkuwahi kusoma kwa wezi wa mali za Taifa kama ndo uzalendo. Usanii huu utawarudia. MUNGU HAJARIBIWI endeleeni tu kuligawa taifa.
Suala la kibiti tulikatazwa tusiliongelee
 
Anaegawa taifa ni nani kama siyo rais wako na Bashite. Kwanini uue kwasababu ya kukosolewa au kuambiwa ukweli yaani kuwa rais ndio uue unavyotaka. Yaani ndio umpe bashite madaraka ya kufanya anavyotaka. Hivi wanawaza kuwa kesho nao hawatakuwa madarakani
 
Hivi na kuteketea kwa moto nyumba ya mbunge wa kigoma mjini muhshimia Zito zuber kabwe ndio muendelezo wa kutochezea NDINGAI?
 
b8837f4df954fdb5f42a331339f7551c.jpg
[emoji125] [emoji125] [emoji125] [emoji125] [emoji125] [emoji125] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23]
Mkuu Mshana Jr,imebidi nicheke japo si vyema. Hii picha imenikumbusha nilpokuwa mtoto mdogo . Unapokuwa unaendesha hicho kigurudumu,hata gari au chochote pembeni hukisikii. Mawazo yote yanakuwa kwenye hiyo driving stick na kigurudumu. Kama ni kwa mtu mzima anaendesha sipati picha,lazima iwe ni ukichaa fulani!
 
[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23]
 
Wewe na hao wasoma kisomo akili yenu sawa. Mbona hawakusoma kibiti au Idi Amini? Akili fupi! Wasome tu
Ni jambo gumu kidogo kwa wale ambao si waamini. Visomo hivi vimezoeleka kuwa kwenye mambo ya binafsi zaidi. Hili la wiki hii ni kama linaelekea kuwa jambo la kitaifa.

Nimesikia majigambo mengi ya watawala, Nimemuona kwa macho yangu Ndugai akisema kwa midomo wake maneno haya CHEZA NA KITU KINGINE SIO NDUGAI. niliogopa sana.

Muda huu alfajiri kuna maombi yanafikia tamati pale kariakoo... Mchungaji kiongozi anataja damu iliyomwagika Tanzania.

Ishu ya kisomo hata kama imekuzwa sana lakini vema watawala wapate ujumbe wa kiroho wenye tafakuri kuu.

Kwamba wananchi wanaona hakuna kimbilio tena na hawana imani na serikali yao, sasa wanapeleka mashtaka yao kwenye NGUVU zisizojulikana. Hata kama visomo hivyo havitaleta madhara tarajiwa lakini ni ujumbe mbaya kwa serikali, kuna kaliba inahisi kuonewa na kunyanyaswa, kuna kaliba inaona wazi kabisa imetengwa na kufanywa yatima.

Energy ya hii kaliba isipuuzwe chondechonde! Tusiwafundishe watu kuacha misingi.

Viongozi na watawala tendeni kwa weledi, tendeni kwa hekima, tendeni kwa tafakuri na maono makuu.Angalieni malalamiko yasiwe mengi mno.

Tumshukuru Mungu wameamua kutumia silaha za maombi na visomo, waacheni msiwazuie. Hawana pengine pa kupumulia, hakuna mikutano ya kisiasa, hakuna kuandamana. Hivi vitu husaidia mno kupunguza nyongo iliyozidi.

Tendeni kwa weledi sana hakukuwa na haja ya kuzuia wachangia damu pale Temeke hospital.. Mambo mengine mbona ni ya kawaida mno?

Kuna ule wimbo wa Ney, ule wa wapo. Baada tu ya Mwakyembe kuruhusu upigwe, haraka sana ule wimbo ukawa sio habari tena!

Visomo hivi ni njia mpya ya kushtua ya kupeleka ujumbe mkubwa.

Visipuuzwe! Visomo vikishindikana hali inaweza kuwa tofauti LAKINI visomo vikijibu hata kama ni coicedence? Tutegemee nini kama taifa?
Wewe
 
Back
Top Bottom