Mkuu mbona hueleweki???...Umesoma vizuri huu uzi??? Rudia kusoma then toa maoni yako.....Hakuna dini hapo usanii Tz na inapangwa Sio eti kwamba Watz wamegusws. Wtz ni wasanii snaa. Wale wa kibiti Maombi gani yalitolewa. "usihukumu na hautahukumiwa@ sasa nani ana uhakika wa haya mambo. Mmekuuwa na majibu ya haraka sna. Kma mmepanga kabisa haya mambo. Ndo mnafanya watu wenye akili wafikirie mbali. Mbona hamkuwahi kusoma kwa wezi wa mali za Taifa kama ndo uzalendo. Usanii huu utawarudia. MUNGU HAJARIBIWI endeleeni tu kuligawa taifa.
Ni jambo gumu kidogo kwa wale ambao si waamini.... Visomo hivi vimezoeleka kuwa kwenye mambo ya binafsi zaidi... Hili la wiki hii ni kama linaelekea kuwa jambo la kitaifa
Nimesikia majigambo mengi ya watawala.... Nimemuona kwa macho yangu Ndugai akisema kwa midomo wake maneno haya.... CHEZA NA KITU KINGINE SIO NDUGAI. niliogopa sana
Muda huu alfajiri kuna maombi yanafikia tamati pale kariakoo... Mchungaji kiongozi anataja damu iliyomwagika Tanzania
Ishu ya kisomo hata kama imekuzwa sana lakini vema watawala wapate ujumbe wa kiroho wenye tafakuri kuu... Kwamba wananchi wanaona hakuna kimbilio tena na hawana imani na serikali yao, sasa wanapeleka mashtaka yao kwenye NGUVU zisizojulikana
Hata kama visomo hivyo havitaleta madhara tarajiwa lakini ni ujumbe mbaya kwa serikali, kuna kaliba inahisi kuonewa na kunyanyaswa, kuna kaliba inaona wazi kabisa imetengwa na kufanywa yatima.... Energy ya hii kaliba isipuuzwe chondechonde! Tusiwafundishe watu kuacha misingi
Viongozi na watawala tendeni kwa weledi, tendeni kwa hekima, tendeni kwa tafakuri na maono makuu... ANGALIENI MALALAMIKO YASIWE MENGI MNO....
Tumshukuru Mungu wameamua kutumia silaha za maombi na visomo, waacheni msiwazuie.. Hawana pengine pa kupumulia, hakuna mikutano ya kisiasa, hakuna kuandamana.... Hivi vitu husaidia mno kupunguza nyongo iliyozidi
Tendeni kwa weledi sana hakukuwa na haja ya kuzuia wachangia damu pale Temeke hospital.. Mambo mengine mbona ni ya kawaida mno?
Kuna ule wimbo wa Ney, ule wa WAPO... Baada tu ya Mwakyembe kuruhusu upigwe, haraka sana ule wimbo ukawa sio habari tena!
Visomo hivi ni njia mpya ya kushtua ya kupeleka ujumbe mkubwa...... Visipuuzwe! Visomo vikishindikana hali inaweza kuwa tofauti LAKINI visomo vikijibu hata kama ni coicedence? Tutegemee nini kama taifa?
Kumbe huwa viongozi wanatudanganya....Kukataza maombi ya wananchi/raia kutokana na imani zao ni jambo la kushangaza kidogo...Serikali haina dini, lakini wananchi wake wana dini, inashangaza serikali ambayo haiamini juu ya Imani inakataza watu wenye Imani kufanya mambo ya Kiimani.
Wanahofia nini hasa!
Kwa vyovyote vile, nchi inaendeshwa kwa mapenzi ya Mungu.Siamini visomo au maombi yatakuwa na matokeo yale ambayo wengi wanatarajia ndani ya muda mfupi. Lakini funzo kubwa ni kwamba kuna watu wengi sana wanalia mioyoni mwao kutokana na mengi yanayoendelea nchini. Kuanzia ukata mtaani, bomoa bomoa, kubanwa kwa uhuru wa kuongea na kukusanyika au kuandamana, mpaka tukio la Lissu kupigwa risasi.
Mambo haya sio madogo. Ktk hali ngumu ya maisha kama hii ungetegemea serikali ikupe moyo na sio ikupe sababu ya kuamini inahusika na kujeruhiwa kwa mtu. Maisha ya Lissu ni ya wanyonge walio wengi, ni ya kupigania wanaoonewa kuanzia vyuoni mpaka ktk migodi. Kushikamana kwa watanzania ktk hili kunaonyesha namna Tundu Lissu alivyoyaishi maisha ya wanyonge. Nadhani ni mmoja wa mawakili wanaoongoza kwa kufanya pro borno (kesi za bure) kwa ajili ya wanyonge.
Narudia kusema kwamba kuna funzo kwa vyombo vyetu vya dola. Kuna watu fulani ktk nchi lazima walindwe kutokana na ushawishi wao na mtaji wao kwa wananchi, lazima walindwe bila kujali kwamba wako vyama vya upinzani. Kwa kufanya hivyo unakuwa unailinda serikali iliyo madarakani dhidi ya chuki na hasira za wananchi. Serikali haiwezi kufanikiwa bila kuungwa mkono na wananchi.
Wizi wa mali zipi za Taifa? Ni huu usanii unaoendelea kwenye masuala ya madini? Hapa kinachofanyika zaidi ni kutafuta sifa. Mpaka sasa, tangu tuanze kuambiwa kuna wizi wa mali za Taifa, ni nini tulichopata au kulipwa, zaidi ya sisi kuwalipa ili kukomboa ndege?Hakuna dini hapo usanii Tz na inapangwa Sio eti kwamba Watz wamegusws. Wtz ni wasanii snaa. Wale wa kibiti Maombi gani yalitolewa. "usihukumu na hautahukumiwa@ sasa nani ana uhakika wa haya mambo. Mmekuuwa na majibu ya haraka sna. Kma mmepanga kabisa haya mambo. Ndo mnafanya watu wenye akili wafikirie mbali. Mbona hamkuwahi kusoma kwa wezi wa mali za Taifa kama ndo uzalendo. Usanii huu utawarudia. MUNGU HAJARIBIWI endeleeni tu kuligawa taifa.