Visa vya Uchawi na Ushirikina Mkoani Kigoma Mwisho wa Reli

Chizi Maarifa

JF-Expert Member
Jul 29, 2013
10,468
23,744
Kigoma Visa vya Uchawi na Ushirikina.

Kigoma ni moja ya Mikoa ambayo inasifika kwa Uchawi nchini Tanzania. Huu mkoa kiasili una watu wachapa kazi sana. Si wazembe ukilinganisha na mikoa mingine yenye ushirikina kama Tanga,Pwani au Zanzibar.

Kigoma maeneo ambayo yanasifika sana kwa Uchawi ni Mwandiga, Ujiji,Mwamgongo n.k

Hapo Mwamgongo ni hatari sana karibu na Mbuga ya Gombe. Kunasifika na moja ya visa vya uchawi ni kimoja ambacho kilitokea mwaka 2020 ni kifo cha Diwani mmoja ambaye inasemekana alichukua Mke wa mtu.

Huyu Diwani ambaye allhamdulilah alikuwa na vijicent ilitokea akawa anatembea na mke wa raia mmoja kijijini hapo.

Yule bwana Raia alipata taarifa. Akanyamaza. Diwani akafikia hatua akaona aoe kabisa mke wa jamaa. Na mke akadai talaka ili akaolewe na Diwani.

Jamaa alimfuata Diwani na kumwambia kwa upole tu kuwa "Mheshimiwa najua unatembea na mke wangu, tafadhali usimwoe maana mimi ntapata shida kulea watoto hawa 6 nlio nao na nina mke mwingine. Uwe na uhusiano naye lakini usimuoe"

Diwani alijibu kwa jeuri tu kuwa "mkeo ndiye anayenilazimisha mzuie yeye siyo mimi"

Jamaa akamenda mpaka kwa viongozi wengine wa kijijini pale akitaka wakamsihi Diwani asimwoe mkewe. Diwani akakaza.

Mpaka jamaa akaenda kwa Rafiki mkubwa wa Diwani kumwomba amsihi rafiki yake asimwoe mkewe yeye atapata shida na watoto. Diwani akamtolea nje jamaa.

Basi jamaa akanyamaza. Siku moja Diwani akakutana na Jamaa Mitaa flani kuna Soko. Diwani akaanza mshambulia jamaa kwa maneno kuwa "nasikia unataka niroga..

Huniwezi,mimi mpaka kufika kuwa Diwani nmetoka mbali sana..." Akaendelea mbele na kumwambia haya nakupa mate na nyayo hii chukua." Akatema mate. Jamaa alimwambia tu Diwani "huo uchawi wa kuchukua mate na nyayo ni mdogo sana,wa watu ambao ni underdog/amateur"

Akaondoka zake. Baada ya siku chache tu Diwani akaanza kuumwa sukari ikapanda mara akaanguka ndo basi tena. Akafa.

Akazikwa. Baada ya siku chache wanafamilia yake wakawa wanamwona Diwani anakuja anagonga pale kwao kuwa afunguliwe mlango anateswa sana.

Diwani alikuwa amevaa pensi chafu.anagonga dirishani akisema anachapwa sana viboko. Afunguliwe.

Mke na watoto wakawa nao wanajawa woga.

Hili tukio lilitokea Mkoani Kigoma mwisho wa Reli.

Na watu wa Kigoma tofauti na Mikoa ya Pwani. Pwani mchawi wako mnaweza mkawa mnacheka naye na kula naye huku anakuroga.

Kigoma ukikorofishana na mtu anakwambia kabisa bila kuuma uma maneno "nitakuroga" hata hatumii sauti ya vitisho. Anakuambia kwa upole tu akikuahidi kuwa kweli atakuroga mbele za watu wengine.na anaenda kukuroga kweli.

Hiki ni moja ya kisa cha mambo ya Uchawi Kigoma.nitaleta Visa vingine vya Uchawi na Ushirikina Kigoma.

Kisa Cha Pili
Kuna jamaa mmoja alikuwa ana tatizo dogo tu na jirani yake shambani. Akawa anasema migomba flani ni ya kwake. yule mzee akamwambia hapana hili shina la Mgomba lipo shambani kwangu. Jamaa mbabe akasema ni lake na atakata.

Kweli ule mgomba mmoja ukazaa. Siku hiyo jamaa akaenda shambani akachonga chonga majani ili akate ndizi. Kunyanyua panga. Mkono ulipigwa ganzi haukushuka. Ukabaki juu na panga.

Akapiga kelele sana maana mkono ukawa kama unanyongwa hivi. Watu wakamchukua kumpeleka kwake. Mkono ulipooza.
 
Kuna siku nilikiwa kibondo pale wilaya ya kgm sasa kuna guest nifikia (jina lina anza na miku...) sasa umefika ucku mda wa kulala nikavyua ngua zangu nikazitupa chini tu, asubu kuamka nikakuta nguo zimeloanishwa maji yani ukizikamua zinatoa maji na hakuna mvua iliyonyesha wala maji waliyoingia ndan chumba kizima likuwa kikavu na chumba kilikukuwa sio self labda kusema maji yametoka chooni kuingia ndani na chumba nilifunga na funguo kwa ndani!

Sitisahau lile tukio
 
Kuna siku nilikiwa kibondo pale wilaya ya kgm sasa kuna guest nifikia (jina lina anza na miku...) sasa umefika ucku mda wa kulala nikavyua ngua zangu nikazitupa chini tu.... asbu kuamka nikakuta nguo zimeloanishwa maji yani ukizikamua zinatoa maji na hakuna mvua iliyonyesha wala maji waliyoingia ndan chumba kizima likuwa kikavu na chumba kilikukuwa sio self labda kusema maji yametoka chooni kuingia ndani na chumba nilifunga na funguo kwa ndani..!!!

Sitisahau lile tukio
Ulitokaje ndani?
 
Kumbe Zanzimba nao hawajambo.

Anyway Mimi mwenyewe niliwahi kupanga nyumba moja na mama kutoka kigoma aisee yule mama nimchawi Sana kama niuchawi basi anadegree au master kabisa kwani alikuwa na uwezo wa kujigeuza paka, kumuingia mtu mwilini mwake na kumuamlisha afanye atakayo yeye.

Nakumbuka Sana Sana alikuwa anamtumia mjukuu wake kufanya uchawi pia alikuwa na uwezo wakufarakanisha yaani jambo dogo unakuta hamuelewani.

Kuna kipindi niliwahi muona anatoka gheto kwetu kupitia mlangoni ikiwa tulifunga na ilikuwa usiku, alinifanyia vitimbi Sana yule mama mpaka nahama pale Kuna vitu alivipandikiza kwenye Kitanda changu kwani nikawa nikilala Kuna hali Fulani ilikua inanizonga na kujikuta nakata tamaa ya kuishi wakati mwingine nakuwa na Hasira Sana na kuanza kuongea pekeangu, aisee sitasahau alichonifanyia yule mama wa kiha.
 
Kigoma ishi kama haupo,kuna jamaa mmoja alimzingua mwenyeji kwenye mambo hayo hayo ya mwanamke.Basi bwana siku jamaa katoka huko na baiskeri kapita chini ya mti tawi likakatika likampiga kiunoni,jamaa kapooza kuanzia kiunoni kushuka chini
Kule hawataki kabisa ujuaji Kabisa yaani. Kuwa tu mpole achana na ubabe
 
Kuna siku nilikiwa kibondo pale wilaya ya kgm sasa kuna guest nifikia (jina lina anza na miku...) sasa umefika ucku mda wa kulala nikavyua ngua zangu nikazitupa chini tu.... asbu kuamka nikakuta nguo zimeloanishwa maji yani ukizikamua zinatoa maji na hakuna mvua iliyonyesha wala maji waliyoingia ndan chumba kizima likuwa kikavu na chumba kilikukuwa sio self labda kusema maji yametoka chooni kuingia ndani na chumba nilifunga na funguo kwa ndani..!!!

Sitisahau lile tukio
Jamaa waliendea kuvulia usiku bila shaka....uliuliza wenyeji?
 
Kumbe Zanzimba nao hawajambo,
Anyway Mimi mwenyewe niliwahi kupanga nyumba moja na mama kutoka kigoma aisee yule mama nimchawi Sana kama niuchawi basi anadegree au master kabisa kwani alikuwa na uwezo wa kujigeuza paka, kumuingia mtu mwilini mwake na kumuamlisha afanye atakayo yeye
Nakumbuka Sana Sana alikuwa anamtumia mjukuu wake kufanya uchawi pia alikuwa na uwezo wakufarakanisha yaani jambo dogo unakuta hamuelewani.

Kuna kipindi niliwahi muona anatoka gheto kwetu kupitia mlangoni ikiwa tulifunga na ilikuwa usiku, alinifanyia vitimbi Sana yule mama mpaka nahama pale Kuna vitu alivipandikiza kwenye Kitanda changu kwani nikawa nikilala Kuna hali Fulani ilikua inanizonga na kujikuta nakata tamaa ya kuishi wakati mwingine nakuwa na Hasira Sana na kuanza kuongea pekeangu, aisee sitasahau alichonifanyia yule mama wa kiha.
Mlikuwa wote wapangaji au yeye ni mwenye nyumba?
 
Back
Top Bottom