Visa gani pombe ilikufanyia hutasahau?

Visa gani pombe ilikufanyia hutasahau?

Nlienda mkoa flani kikazi. Jamaa yangu akanialika weekend kwake. Nikaenda akanitoa out tukapige maji. Nlikunywa karibia crate zima la beer safari. Baadaye anasema nikaanza kuongea kwa uchungu sana nikilia kwa kumuonea huruma kuwa jamaa hajajenga ila anakunywa beer daily. Nlimsema sana bahati mbaya tulipokuwa pale alileta na mchepuko wake na mchepuko akaja na rafiki yake. Jamaa alijisikia aibu sana.

Bahati mbaya alikuwa amenitaka siku hiyo nikalale kwake ilikuwa Ijumaa.tuliporudi kwake nikaitisha kikao. Nikamsema sana mbele ya mke wake kuwa hafanyi mambo ya maendeleo anaendekeza mademu tu na pombe. Nikamwambia nisimuone tena na wale mademu aliowaleta pale bar

Nikaanza kumsema na shemeji yangu kuwa naye amekuwa hatumii akili. Anawaza kujilemba tu muda wote. Badala wasave pesa wafanye maisha. Wanazaa kma mbwa....watoto watano na bado hawajasettle.

Kesho yake asubuhi jamaa aliomba anirudishe guest. Hatukuwahi wasiliana tena mpaka leo.
Dah[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]

Sent from my SM-A207F using JamiiForums mobile app
 
Nlienda mkoa flani kikazi. Jamaa yangu akanialika weekend kwake. Nikaenda akanitoa out tukapige maji. Nlikunywa karibia crate zima la beer safari. Baadaye anasema nikaanza kuongea kwa uchungu sana nikilia kwa kumuonea huruma kuwa jamaa hajajenga ila anakunywa beer daily. Nlimsema sana bahati mbaya tulipokuwa pale alileta na mchepuko wake na mchepuko akaja na rafiki yake. Jamaa alijisikia aibu sana.

Bahati mbaya alikuwa amenitaka siku hiyo nikalale kwake ilikuwa Ijumaa.tuliporudi kwake nikaitisha kikao. Nikamsema sana mbele ya mke wake kuwa hafanyi mambo ya maendeleo anaendekeza mademu tu na pombe. Nikamwambia nisimuone tena na wale mademu aliowaleta pale bar

Nikaanza kumsema na shemeji yangu kuwa naye amekuwa hatumii akili. Anawaza kujilemba tu muda wote. Badala wasave pesa wafanye maisha. Wanazaa kma mbwa....watoto watano na bado hawajasettle.

Kesho yake asubuhi jamaa aliomba anirudishe guest. Hatukuwahi wasiliana tena mpaka leo.
Ila qmmkk hii ndio kiboko.. 🤣🤣🤣

Mnazaana kama mbwa.. 🤣🤣🤣

Ukweli mchungu... 🤣🤣🤣
 
Hakuna pombe haina hangover jombaa, nimejaribu pombe nyingi sana nilizoambiwa hazina hangover, hali ni ile ile! Kinacholeta hangover sio jina la pombe but ni ile alcohol
Pombe kali hazina hang over ukilinganisha na beer, mimi nikinywa beer dah asubui nakuwa na hang over mpaka ninywe kahawa ndio napata afueni ila nikipiga kitu kali naamka fresh kabisa
 
Pombe kali hazina hang over ukilinganisha na beer, mimi nikinywa beer dah asubui nakuwa na hang over mpaka ninywe kahawa ndio napata afueni ila nikipiga kitu kali naamka fresh kabisa
Mzee baba hangover ni mtu na mtu na pia kiasi unachotumia na ulaji wako.....

Pombe zote zishanichapa hangover....
 
Nlienda mkoa flani kikazi. Jamaa yangu akanialika weekend kwake. Nikaenda akanitoa out tukapige maji. Nlikunywa karibia crate zima la beer safari. Baadaye anasema nikaanza kuongea kwa uchungu sana nikilia kwa kumuonea huruma kuwa jamaa hajajenga ila anakunywa beer daily. Nlimsema sana bahati mbaya tulipokuwa pale alileta na mchepuko wake na mchepuko akaja na rafiki yake. Jamaa alijisikia aibu sana.

Bahati mbaya alikuwa amenitaka siku hiyo nikalale kwake ilikuwa Ijumaa.tuliporudi kwake nikaitisha kikao. Nikamsema sana mbele ya mke wake kuwa hafanyi mambo ya maendeleo anaendekeza mademu tu na pombe. Nikamwambia nisimuone tena na wale mademu aliowaleta pale bar

Nikaanza kumsema na shemeji yangu kuwa naye amekuwa hatumii akili. Anawaza kujilemba tu muda wote. Badala wasave pesa wafanye maisha. Wanazaa kma mbwa....watoto watano na bado hawajasettle.

Kesho yake asubuhi jamaa aliomba anirudishe guest. Hatukuwahi wasiliana tena mpaka leo.
Nmecheka sana. Uliacha ugomvi wa maana.
 
Mzee baba hangover ni mtu na mtu na pia kiasi unachotumia na ulaji wako.....

Pombe zote zishanichapa hangover....
True ni ulaji wako na muda uliotumia kupumzika,ukiwa umekula vizuri na ukipata mda mrefu wa kupumzika huwezi pata hangover,lakini hukula vizuri na mda wa kupumzika ni mchache lazima ikutandike.
 
[emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3]falaaa sanaa
Shukarani ya punda mateke lakini ulimpa ukweli wake na akuambiaye ukweli wa maendeleo ni mtu mzuri.Hapa ndipo ninaposhindwaga kuacha pombe maana pombe inakufanya unaongea kilicho rohoni kwako bila kuficha.Ndio maana watu wanasemaga walevi sio wanafiki kama vijiwe vya kahawa.Big up bro ulifanya vyema
 
Nawapa mkasa mwingine wa pombe, nikiwa peke yangu familia wameenda likizo ya christmas, nilikunywa pombe siku tatu bila kula ndani namtuma bodaboda tu, wife anapiga simu nashindwa hata kuichukua kwenye sofa nimelala chini kwa carpeti, anamtuma mtu hata sijafunga mlango hali mbaya hatari kuamka siwezi, nikabebwa siku tatu hospital nimewekewa drip natetemeka kama simu iko vibration. Nilipotoka nikaenda kuchukua k-vant ndogo kuweka mwili sawa. Si mikasa ya kufurahisha lakini naikumbuka sana.
Eti k vant ya kuweka mwili sawa......
 
Tarehe 20 nitatimiza miezi mitatu bila kunywa pombe....

Miezi mitatu bila kufanya ngono.
Miezi mitatu bila kula wanga (ugali na wali)

Itakua miezi mitatu natimiza kilo 75 kutoka kilo 96.....

Super....
Hongera Sana mkuu. Pombe nimeweza kuacha ni miezi 9 sasa, Ila kuacha kula wanga nashindwa maana ndio vyakula vinavyotuzunguka kwa zaidi ya 60%.
Niko na 95kg natamani nipungue angalau niwe na 80kg au less. Nimejaribu kufanya jogging na mazoezi mengine madogo madogo lakini bado.
 
Ni kweli wanga ndio chakula kikuu... Unaweza kupunguza portion tu kama ulikua unakula kilo 2 basi punguza kwa kilo moja na nafasi iliyobaki jazia na maji na matunda.....

Usiku usile wanga kabsa, jaribu kula nyama/protein na matunda kwa wingi...
 
Asante sana mkuu. Hebu niianze mapema kwa kujipa miezi 2 kwanza.
 
Binafsi nakunywa pombe mara mojamoja, naweza kupitisha mwezi sijanywa ila nikinywa huwa nalipiza siku ambazo sikunywa kabisa. Hii imenikuta wiki chache zilizopita tulikuwa na event na marafiki tunaotoka sehemu moja, kwenye pombe mbuzi anahusika nilisimamia kitengo.

Nilikunywa mpaka K Vant nikaiona kama soda, nakuja kustuka pombe imenizidi kiasi hata kutembea ilikuwa noma. Sifanyi fujo nikilewa kila mtu alifurahi lakini balaa lipo kwa ndugu zangu kujua kuwa ninakunywa. Busara ilitumika simu yangu nikaicha kwa mtu niipate nikiwa fresh.

Ase nilifanya safari ya saa 1 na nusu peke yangu nikiwa nimelewa na sijui nilifikaje nyumbani, kuja kustuka ni asubuhi niko kitandani tatizo limebaki kwa ndugu zangu. Wakati nimeacha simu kwa rafiki nilipigiwa jamaa akapokea na kuwaambia niko kwenye matatizo ile kitu ilizua taharuki watu hawajalala kuulizia hali yangu maana mimi sikupatikana tena.

Hii kitu imeniweka sehemu mbaya sana hakuna mtu anataka kunielewa tena. Ukweli nimekwama nimeamua kuacha pombe maana naona itanigombanisha na ndugu.
Nilimwita bossy malaya
 
Juzi kati, kuna rafiki yangu, alitoka kwao kusalimia na alikuwa kalewa chakari. Baada ya kufika mjini mida ya saa mbili usiku alinitafuta na nikamuelekeza nilipo. Baada ya kufika aliendelea kunywa na baada ya muda mfupi alienda chooni kujisaidia. Huko chooni alivua koti na kulitundika ukutani. Simu na wallet aliviweka ktk koti. Baada ya kujisaidia alisahau kuvaa koti lake akaja moja kwa moja mezani. Baada ya dakika ishirini ndio anashtuka kuwa kasahau koti chooni. Ilibidi aende chooni ambako alilikuta koti lake lakini simu na wallet havikuwepo!
 
Hujafika Tukuyu mkuu
Nimesoma manow, nimefanya kazi kidogo kama miezi 6 pale nssf, nimelima viazi ntokela bado siifahamu tukuyu mkuu?? Baridi kidogo ipo mwakaleli, unakuja ntokela hapa kuna baridi na ukiwa unapanda namba one kuja isyonje... mbeya kuna baridi kuliko tukuyu mkuu...
 
Kiwira, katumba, tukuyu mjini mpaka huku ushirika kuna baridi gani mkuu?
 
Daah!! Ouyaaa Wee. Pombe sio Poa.

Nina VISA vingi sana yaani sanaa maana sijui hata nielezee kipi niache kipi lakini kuna kimoja hicho sitakisahau Maisha.

Kipindi flani miaka ya nyuma sana nlikua Vijijini, Mkoani huko Kikazi. Sasa mimi ni yule mtu wa kujichanganya sana alafu siwezagi kunywa mwenyewe hata nikienda sehemu naweza kuanza mwenyewe lakini baada ya muda tu nakuwa nimeshazoeana na nliowakuta kisha tunaendelea kuenjoy mdogomdogo.

One day wikiendi hivi Saturday flani hivi imetulia. Nikatoka Ofisini mapema maana ni nusu siku nikaeda home nikaoga fresh nikachange Mkanda nje nikatupia T-Shirt na Jeans nikaenda Road.

Nikaenda kutulia Bar moja kubwa hivi ina Counter 1 barabarani huku nje na ndani mwisho kabisa kuna Counter ya 2 hapo katikati ndiyo watu wanakaa. Mimi nikawa nimetulia counter ya barabarani huku nakula vyedi (Safari) huku nacheki Magari yanapita, mengine yanaingia Bar, na mengine yanatoka napata burdani tosha kabisa.

Mpaka inafika saa 1 nshakula vyedi kama 6 hivi nikaona kama sielewi nikamchombeza Dada wa Counter amuite mtu wa Jikon alafu alivyorudi nikamzingua... Aaf kama vipi anipe K nichachue kama Maskhara vile nlikula Mvua za Matusi pale kejeli na kubinuliwa mdomo alinisema sana na kuniambia mimi namdhalilisha na kumuona Malaya mara yeye hajiuzi maneno mengi yakamtoka; nikaona isiwe kesi nikamwambia Sorry basi kunywa Bia na mimi nipe Bia nimeshakuelewa... Am sorry. Akapoa na mda huo nshamugiza Jamaa Mbavu Portion 2 na Ndizi 4.

Wakati naendelea na chupa zangu akawa anahudumia wateja wengine na wahudumu wanakuja pale counter kuchukua vinywaji lakini ananiangalia kwa hasira alafu anatikisha kichwa kama anasikitika hivi, mimi kwakua nshaharibu nikawa sina habari nampiga kijicho pembe nampotezea tu. Mara muda sio mrefu msosi ukaja mixer kachumbari nini Ndizi zimeremba sahani ya Bati ile pembe kwa pembe nikanawa nikamwambia jamaa amnawishe na yeye aje kula ila aongeze kwanza Bia 2 kama mwanzo mimi na yeye aikua anakunywa Eagle(Ndege) alafu ndiyo tuendelee. Akaniangalia Akatabasam huku anasikitika kama hataki vile.

Wakati tunaendelea kula pale yeye yuko ndani mimi niko nje viti virefu akaniangalia tena ila sasahivi akanikazia macho hivi nikamuuliza vipi umekabwa au akacheka akaniuliza Uko Serious, Kweli!!? Mimi nikatabasamu nikapiga funda kumezea nyama nikamjibu Ndiyo au ulijua nakuzingua!!? Tukaendelea kudonoa menu.

Tukiwa tunakribia kumaliza, nikamwachia sahani akae nayo ndan kule amalizia kabisa, namuona anakenua tu, Jamaa akaja nikanawa nikalipa nikaendelea kula Mma.[emoji97]

Ghafla naona napewa kirisit nikatahamaki vipi tena nikamuangalia na kumuuliza kwani nimekuomba Bill? Akaniambia kwa ishara Fungua usome... Daah!! Nikafungua nakuta ameandika "...Asa ntakupea wapi, tunafunga saa 10 leo." Nikacheka... Nikakichanachana kile kirisitk nkakitupa. Nikatulia. Mule Kaunta akanza kuhaha Mara atoke aingie ananifanyia Ishara ya Mikono akimaanish VIPI SASA!!? Nikamjibu Niongezee Bia alafu uje.

Akaongeza aaf, akanisogelea nikamwambia; "WEWE MTU MZIMA, UNANIULIZAJE MASWALI YA KITOTO HIVO." Nikaendelea na vyupa vyangu nakula monde tu... Akang'ata kidole akaendelea kuwahudumia wengine. Mara akakaa kwenye kiti chake pale ndani akawazaa alafu akatoka kisha akarudi akandika kirisit kingine; "... Ukiona amekuja mhudumu counter humu na mimi nimetoka basi uje ChaKike mwisho kabisa." Akanipa nikakisoma Chap nikamuoneshe Ngumi yenye Dole Gumba nikimaanisha Fresh! nimekusoma.

~ Itaendelea~

Lakini palepale Counter wakati Jamaa wa jikoni ananinawisha baada ya kumaliza kuna Mwamba alikuja akasalimia akakaa juu pale Kaunta nikawa katika kuongea nae na kumdodosa nikagundua ni Wajina yaani wakuitwa jina langu basi katika storystory nikamwambia Dada muongezee Bia ingiza bill yangu; Mwamba alikua anakunywa Plisner(Bia inanukaga Vibaya hii) fresh tukaendelea na story kama Mabest tunaojuana kumbe tumekutana palepale tena night hiyo hiyo.

Huku na huku Mwamba akanipanga kuna Mama Ntilie mmoja bonge wemepanga wakutane hapo ila kama fresh amchek aje na Msaidizi wake ili na mimi nisiwe mnyonge nikamwambia fresh utakua umenifaa aisee!! Tukacheka... Akampandia hewani na ile nokia six button akampanga aje na yule aliyemuhudumia yeye Mchana alivyoenda kula pale. Bonge akakubali. Baada tu ya kumaliza kuongea nae akaanza kumsifia huyo Msaidizi na kuniambia ni yaani Chombo ya Kwenda Aaf hata yeye ndiyo alikua anamtaka sema nini Big kampenda mwenyewe tu kwahiyo wacha aishi nae kwanza. Daah!! Kwa jinsi Mwamba alivyonipanga nikamwambia Dada wa Counter amuongeze Plisner ingine maana amenifurahisha Mwamba akawa ana Bia ya 3 Mpya ya pili iko nusu na ya kwanza keshamaliza.

Naomba niconclude(Nachoka kuandika): Nlijikuta nimekula Madem wote wa3 kizembe sana kwasababu yule wa Kaunta kule Toi nlienda nikapiga kimoja cha Mkwezi kirefu cha kishujaa cha kushika ukuta alafu pale hatukukaa sana walivyokuja wale Bonge na Msaidizi kumbe ni mtu na Shangazi yake tukawapiga bia kadhaa kila mtu tu nikalipa Bill yangu na jamaa akalipa yake tukaondoka Mwamba akatupeleka Kilabuni moja hivi Mashambani sio mbali na pale wanauza Pombe kwenye Makopo ya Chooni yale sema Makubwa na Madogo kama yale ya kuuzia Mbege. Alafu sijui ilikua Pombe gani ile ipo kama Mbege sema inarangj ya Maziwa na Mafuta kwa juu (kama uhudumiwe Maziwa ya Moto yenye Cream alafu yaanze kupoa kwenye Kikombe) ule utando sasa na machicha kidogo kwa juu kama uchafu hivi umechanganyika na mafuta unapuliza unakunywa.

Haina kushea kila mtu na mtuwe, Mwamba akaagiza Kubwa 2 mimi nikatoa Buku 2 na Mwamba akatoa Buku Jero kumbe Lile kopo Dogo ni Buku na lile Kubwa Ni Buku Jero; Mimi nimebigwa na Butwaa lakini sielewi wale wenzangu inaonekaga ndiyo Pigo zao kwasababu Bi Mkubwa( Hawa ni wale waMama wanakuuzia huku wamevaa Kanga/ Vitenge viwili tu kiunoni na kifuani tu. Aaf, wanakuaga aidha Mnene Sana au Mwembamba sana kisha Ni weusiii kama Mkaa sijawi ona Mweupe mimi) alivyoleta nini mixer wanaongea Kilugha mara onja ndiyo unipe mara ya leo mbona kama kali sijui machicha yamefanyaje ivoo yaani. Asa kwasababu pale Bar hawakuwa wamekunywa kivilee kama sisi waliyafakamia yale Mapombe pale mixer yule Bonge akaongezaa na Kopo dogo lile la Buku tukiwa tumekaa upenuni kwenye Benchi hivi tumezunguka duara tukifuatana na Mabenji mengine.

Mwamba alizima pale pale ikabidi mimi niondoke nao wote wawili mpaka kwangu njia nzima tunaimba nyimbo za kilugha mimi nafanya kuitikia tu. Asubuhi, Bonge alitapika Uvunguni sijui hata sina kumbukumbu yaani alitapikaje Uvunguni ambako hakufikiki hata, huku Chumba kizima kinanuka puya la Pombe za Kienyeji aaf yule Shangazi yake na yeye alikua hataki kuondoka... Eti kapapenda ghetto. Mimi sasa ndiyo sifai Kichwa Kinauma, Naskia Kiu kishenzi na huku Mdomoni sasa sijui nlikua najiskiaje ni chefuchefu sio kichefuchefu, machicha kama nimekula Mchanga vile na uso unang'aa kama nimeoga Mafuta. Mimi nimeamka na Boxer na wao kila mmoja ana Pensi lake kubwa lina mifuko yenye zipu huku Vifua wazi hivi nikawatoa hela kidogo wakaondoka, Siwajui na wao hawanijui mpka leo maana walitaka wapike Chai na mimi nlikua sina Chombo chochote ndani basi walivyotoka saa 5 hiyo kweupe kabisa Majirani na wapangaji wengine kama vile waliambiana Wageni rasmi wanatoka wakawa wamejipanga nje wawaone... Daah!! Aibu ile sitaisahau kamwe.
 
Back
Top Bottom