Visa gani pombe ilikufanyia hutasahau?

Visa gani pombe ilikufanyia hutasahau?

Nimezoea Gongo na naona bia zinanichelewesha kupata steam. Nakula Sana nyama wakuu, nikishapata gongo natamani kusikia harufu za damu ya nyama
 
Nimezoea Gongo na naona bia zinanichelewesha kupata steam.Nakula Sana nyama wakuu,nikishapata gongo natamani kusikia harufu za damu ya nyama
Nimeshaharibu kazi tena aisee chezea gambe upuuzi huu aliyenifundisha pombe alaaniwe
 
Binafsi nakunywa pombe mara mojamoja, naweza kupitisha mwezi sijanywa ila nikinywa huwa nalipiza siku ambazo sikunywa kabisa. Hii imenikuta wiki chache zilizopita tulikuwa na event na marafiki tunaotoka sehemu moja, kwenye pombe mbuzi anahusika nilisimamia kitengo.

Nilikunywa mpaka K Vant nikaiona kama soda, nakuja kustuka pombe imenizidi kiasi hata kutembea ilikuwa noma. Sifanyi fujo nikilewa kila mtu alifurahi lakini balaa lipo kwa ndugu zangu kujua kuwa ninakunywa. Busara ilitumika simu yangu nikaicha kwa mtu niipate nikiwa fresh.

Ase nilifanya safari ya saa 1 na nusu peke yangu nikiwa nimelewa na sijui nilifikaje nyumbani, kuja kustuka ni asubuhi niko kitandani tatizo limebaki kwa ndugu zangu. Wakati nimeacha simu kwa rafiki nilipigiwa jamaa akapokea na kuwaambia niko kwenye matatizo ile kitu ilizua taharuki watu hawajalala kuulizia hali yangu maana mimi sikupatikana tena.

Hii kitu imeniweka sehemu mbaya sana hakuna mtu anataka kunielewa tena. Ukweli nimekwama nimeamua kuacha pombe maana naona itanigombanisha na ndugu.

Pombe inafanya visa, visa anafanya mnywaji kwa kuzidisha pombe. Pombe kama Pombe haina shida yoyote ni kinywaji.
 
Ndy asubuhi nashtuliwa na muhudumu,,tahamaki nimelala na mrembo,,
Nataka nianze demu ,,kachelewa Chuo,,
Huku muhudumu katusimamia nje..pale hata tako 7 nisingepiga..
Nilijilaumu sana kulewa..
Mbaya hiyo mwite tena
 
Siku ambayo siwezi isahau ni siku nimekunywa pombe kisha nikaenda zangu home Ile nimeingia kulala mkojo ukanibana ikabidi nitoke chumbani nikakojoe baada ya kuenda chooni nikaenda jikoni kukojoa alafu nikaludi zangu kulala kesho yake asubuh ebanaeeeeee Sito sahau
Duuh kweli pombe siyo chai,mnaipendea nn mpaka inakutoa akili hivi?
 
Iweje wanywaji wengine hawalewi? Ni pombe gani ambayo inalewesha kwa haraka? Kwanini wanywaji wengine wanaenda kujisaidia mara kwa mara, na wengine hawaendi kujisaidia wanapokunywa?

Kuna semi kuwa mhudumu wa bar akitaka mteja wake alewe na apoteze chaneli huwa wanachanganya na Ugoro?
 
Kuna siku nikiwa bachela ndio nimeanza anza kazi Nina pea moja tu ya viatu vizuri vya kuendea mjini na kazini.

Sasa Niko Sinza usiku nimeutwika Niko bwii narudi zangu home huku mvua imenyesha mchana na imeshaacha. Kuna ka mbalamwezi kwa mbali. Mbele yangu kukawa na bonge la dimbwi, Basi na zile pombe like dimbwi nikadhani ndio palipo kauka. Nikaliingia jumla na viatu na soksi na suruali.

Kesho yake sikutoka kwenda kazini maana sikua na viatu vingine nikashinda nimeanika viatu. Kabla havijakauka mvua ikashuka Tena. Na siku ya pili Tena sikwenda kazini nikiwa nakausha viatu.

Siku ya tatu nilipofika kazini mkwara niliowekewa ilibidi niache pombe.
 
Back
Top Bottom