benzemah
JF-Expert Member
- Nov 19, 2014
- 1,504
- 3,035
Vipimo vya vinasaba (DNA) vya mwili wa mtoto Mabirika Wilson (8), aliyefariki dunia Aprili 16 mwaka huu wilayani Magu, pamoja vya wazazi wake, vimeonesha ni mtoto wao.
Uchunguzi huo unapingana na madai ya awali kwamba mtoto huyo amekutwa akiwa hai katika wilaya nyingine ya Kwimba mkoani hapo.
Vipimo hivyo vilivyofanywa na wataalamu wa afya kutoka Kitengo cha 'Forensic' wakishirikiana na wataalamu kutoka Ofisi' ya Mkemia wa Serikali baada ya kupata kibali cha kufukua mwili na kuufanyia vipimo kutoka mahakamani, vimeonesha kuwa mtoto aliveokotwa wilayani Kwimba Aprili 27 hana uhusiano na wazazi hao, hivyo mtoto wao halisi ni yule aliyeugua na kufariki dunia Aprili 16,. mwaka huu.

Hayo yalibainishwa mwishoni mwa wiki na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Wilbroad Mutafungwa, aliyesema kuwa baada ya kubaini ukweli huo, jeshi linawashikilia wazazi wa moto huyo ambao ni Wilson Bulabo (35) na Helena Robert (33) kwa kufanya udanganyifu na kuzua taharuki katika jamii, wakitaka kujipatia mtoto aliyeokotwa ilhali siyo mtoto wao.
"Haiwezekani kwa kipindi cha siku 10 tu wazazi wawe tayari wamemsahau mtoto wao ambaye wamekaa naye kwa kipindi cha miaka minane na kuanza 'kumfananisha na mtoto ambaye sio wao. "Hivyo, baada ya uchunguzi wa kina kufanyika, watafikishwa mahakamani kujibu mashtaka mbalimbali, ikiwa ni pamoja na kuzua taharuki katika jamii na kuaminisha watu juu ya ufufuko wa mtoto wao," alisema Kamanda Mutafungwa.
Kamanda huyo alisema kuwa baada ya mtoto huyo kuhojiwa katika hali ya utulivu, alijitambulisha kwa jina moja la Mussa, hivyo kuwataka wazazi ambao watakuwa walipotelewa na mtoto kufika kituoni huko kumtambua kwa kuwa kwa sasa anahifadhiwa katika moja ya kituo cha kulelea watoto ambacho hakuwa tayari kukiweka wazi kwa sababu za kiuchunguzi.
Mwenyekitt wa Kijiji cha Mwangika, Jeremaniuss Masala, alisema kuwa baada ya kumpata moto huyo, walitangaza ili kuwapata ndugu zake na walipotokea wazazi hao na kueleza juu ya mtoto wao kufariki dunia na kudai huyo ndiye moto aliyefariki, wakaamua kushirikisha vyombo vya sheria kuondoa utata huo ambao ungesababisha madhara kutokana na kuhusishwa na ushirikina.