Mazishi ya mtoto anayedaiwa kuuliwa kwa kuchapwa na mwalimu yaahirishwa. Mwili wake unaendelea kufanyiwa uchunguzi

Suley2019

JF-Expert Member
Oct 7, 2019
1,817
4,566


Maziko ya Mwanafunzi Jonathan Makanyaga (6) wa darasa la kwanza Shule ya msingi Mrupanga, Rau Kusini mkoani Kilimanjaro yameshindikana kufanyika leo baada ya Polisi kuiambia Familia kuwa uchunguzi wa mwili bado haujakamilika.

Kamanda wa Polisi Mkoani Kilimanjaro amesema baada ya Familia kuwa na mashaka kuhusu kifo cha Mtoto wao, wamelazimika kuomba Madaktari kutoka Dar es salaam kwa ajili ya uchunguzi mwingine na hivyo uwezekano wa kuupumzisha mwili huo leo umeshindikana kutokana na malalamiko yaliyopo.

Hadi muda huu mwili huo haujawasili nyumbani hapo na Watu wameanza kuondoka hadi hapo watakapopata tarehe nyingine ya kuzika.

Hatua hiyo inajiri huku Jeshi la Polisi Kilimanjaro likiwashikilia Waalimu watano wa Shule ya Msingi Mrupanga iliyopo Kata ya Rau Kusini, Kilimanjaro kwa tuhuma za mauaji ya Mtoto huyo anayedaiwa kuchapwa na Walimu wa Field baada ya kuchelewa kushika namba ya kuhesabiwa asubuhi.

Imedaiwa kuwa Waalimu hao walimchapa February 28,2024 na kupelekea Mtoto huyo kupata maumivu na kuwaishwa Hospitali ya KCMC ambako ilipofika March 11,2024 alifariki.

Pia soma:
- DOKEZO - Mwanangu ameuawa kwa kupigwa na Mwalimu lakini kesi inazungushwa
 
Sema tuache masikhara , walimu wa kibongo wanachapa masela. NDIO MAANA ENZI ZETU TUKIMALIZA TULIKUWA TUNAANDIKA ( AKUMBUKWE NIGGA BISHOP aka mtaalamu wa kujaladia )
 
Vijijini watoto wengi wanakimbia shule Kwa sababu hii

Walimu wapo full of stress.....ni wachache ambao wako na karama ya ualimu
 
Dunia inebadirika, waalimu wakubali kubadirika, vile viboko tukivyokua tunachapwa sisi ukiwaletea watoto wa sasa hivi unaweza kuua nusu ya darasa.
Waalimu waache kuchapa , watoto wa siku hizi ni wabovu wabovu
 
Sasa kuchelewa tu ndio umchape mtoto hadi umuue ? Hawa walimu wengine wamechanganyikiwa na maisha jamani
 
Matokeo ya kufanya kazi usiyoipenda ndio hayo. Angeipenda kazi hiyo angekuwa kama mzazi kwa mtoto huyo mdogo.
 
Walimu acheni tabia hizo mtafungwa bure .matoto yenyewe ya kipindi hiki yanamaradhi kama yote fimbo moja analala jumla kesi kwako.
 
Kumpiga mtoto mpaka ngumi za tumboni huyo mwalimu alikuwa na tatizo la afya ya akili.
 
Back
Top Bottom