Sean Paul
JF-Expert Member
- Jun 16, 2013
- 807
- 2,106
Habari wana nzengo,
Sheria ya kupata kipimo cha vinasaba (DNA) hapa Tanzania ina mchakato mgumu kidogo. Ni kwamba ni ofisi maalum zinaweza kuomba kupata vipimo hivyo tu, katika kutekeleza majukumu yake. Either ni mahakama katika kutatua mgogoro, polisi katika uchunguzi, ofisi ya ustawi wa Jamii katika kutekeleza majukumu yake, mkuu wa wilaya n.k. Sheria inasema ili upate kipimo hicho ni lazima uende na barua kutoka moja ya vyombo hivyo. Si mtu tu binafsi ajiamulie kwenda. Wataalam wa sheria mnaweza kutusaidia vifungu.
Sababu kubwa inayosemwa serikali inazua kupima privately DNA ni kulinda maslahi ya mtoto kijamii.
Inasemekana hata ukienda kudai kipimo kujua mtoto ni wako au si wako....wengi huambiwa mtoto ni wako ili tu kumkinga mtoto yule na janga la kutokuwa na baba. Sawa, tunamlinda mtoto na malezi apate ya baba; je tunamtendea haki huyu mwanaume? Nonetheless, mbona mtu akimpa mwanafunzi mimba anafungwa miaka 30 jela? Huyu mtoto ambaye baba yake anakuwa jela kwa miaka hiyo mbona anakosa malezi ya baba? Na tuna uhakika mzazi huyu akitoka jela atakuwa na upendo na mtoto huyo?
Kwa maoni yangu hii sheria haitufai kwa hali ya sasa ya kimazingira. Tunaishi katika dunia yenye harakati haramu nyingi sana. Full of chaos, crazy world. Watu wamekuwa matapeli katika siasa, dini, ndoa, mahusiano, yaani kila mahali. Hakuna mahali binadamu upo comfortable, lolote linaweza kutokea popote usipopatarajia. Tunaishi kimachale machale mno.
Kitanda hakizai haramu. Kauli hii zamani ilikua na nguvu kwa sababu mkeo alikua na uwezo kupata mimba isiyo yako lakini akakata kabisa mawasiliano na huyo baba wa mtoto. Mnaishi kwa furaha na amani bila kelele. Zamani ilikua fahari kuwa na watoto wengi, mkeo akizaa mtoto ni wako tu unalea. Wazee waliweza kwenda sehemu wakaa miaka kadhaa, akirudi akakuta mke ana mtoto analea tu. Kwa dunia ya sasa hii ni liability isiyo na manufaa.
We umejivika upofu kitanda hakizai haramu, mkeo ana wasiliana vizuri kabisa na baba mtoto wake. Na kwa dunia hii ya generantion z upo uwezekano baadae mtoto akajua we siyo baba yake na akakukana mchana kweupe subject to hali yako ya baadae au ya huyo baba yake kibaiolojia. Mtoto yupo boarding, mama akienda kumuona anakwenda na mzazi mwenzie. Zawadi na pesa au hata ada jamaa anatoa vile vile. We umekwama mkeo akakudanganya amekopa kazini kumbe kachukua pesa kwa mzazi mwenzie.
Wanaume tuamke tulinde maslahi yetu. Amani na furaha ya moyo ni zawadi hakuna wa kukupa isipokuwa wewe mwenyewe. Sheria iweke mazingira mazuri ya kipimo hiki kiwe ruksa vile mtu atakavyo bila kumuathiri yeyote emotionally and physically.
Sean.