Vijana tuna mengi ya kujifunza kutoka kwa Mzee Jakaya Kikwete na Edward Lowassa

kiroka

JF-Expert Member
Feb 28, 2018
355
1,856
I declare interest Mimi ni muumini wa Kikwete na Lowassa, Historia inaeleza kua hawa jamaa walikua marafiki wakubwa sana mpaka lilivokuja suala la Richmond inasemekana ndio lililowavuruga

Lakini pamoja na kugombana mmoja akiwa ni mwenyekiti wa CCM taifa mwingine akiwa mgombea urais wa chama pinzani lakini bado waliheshimiana hawajawahi kutukanana jukwaani ninachokumbuka Mimi kuhusu Lowassa kila akipanda jukwaani alikua anasema rafiki yangu kaharibu nchi wakati Jk alikua akisema mwenye Richmond chadema wanae hakuwahi kumwita Lowassa fisadi.

Natamani tupate mwandishi mmoja afanye interview na hawa jamaa aangalie Historia yao wapi wametoka mangapi wamefanya pamoja je nini kiliwagombanisha na status yao kwa Sasa ipoje, nadhani itakua documentary nzuri mno.
 
Natamani tupate mwandishi mmoja afanye interview na Hawa jamaa aangalie Historia yao wapi wametoka mangapi wamefanya pamoja je nini kiliwagombanisha na status yao kwa Sasa ipoje, nadhani itakua documentary nzuri mno.

Sent from my TECNO RA7 using JamiiForums mobile app
Naunga mkono hoja, itakuwa not only a good Documentary, but an interesting one.

Nalifanyia kazi hili wazo.

P
 
Kwa mtazamo wangu kilichokuwa kinawaunganisha ni maslahi.Ukiondoa maslahi hawajawahi kuwa marafiki hata kidogo.
Hakuna urafiki duniani usio wa kimaslahi. Urafiki maana yake ni maslahi.

Wakristo wana urafiki na YESU sababu ni njia ya kwenda mbinguni. Asingekuwa na mbingu huo urafiki ungeweza usiwepo.

Ukiondoa maslahi utakayopata kutoka kwa mtu anayeitwa rafiki huyo rafiki hawi rafiki tena anakuwa tu mtu unayemfahamu.
 
siipendi ccm bt hawa ni wanasiasa bora pamoja na madhaifu yao, wamedhihirisha siasa si kutoleana shombo wala kukoseana heshima, napendekeza kitungwe kitabu cha siasa chenye mlengo wa siasa safi za hawa mabwana kisha kifanywe mwongozo wa siasa zetu.
 
Serikali : Tumeongeza tozo ya mafuta ili kuinua uchumi wa nchi.

UVCCM : Huu ndo uzalendo lazima watu walipe hizi tozo ili Serikali ijenge miundombinu

Serikali : Tumepunguza tozo ya mafuta

UVCCM: Tunaipongeza sana Serikali kwa kupunguza tozo ya mafuta maana inawaumiza wananchi.
 
Naunga mkono hoja, itakuwa not only a good Documentary, but an interesting one.

Nalifanyia kazi hili wazo.

P
Fanya brother waandishi mnatakiwa muangalie vitu in different angles tuleteeni vitu tusivyofikiria kirahisi, Hawa jamaa umri unaenda wasije wakapotea kikaja kizazi kingne kikaona kama hapakua na watu

Sent from my TECNO RA7 using JamiiForums mobile app
 
Safari yao ilikua ya kimaslahi ilikua Kikwete aje amuachie kijiti Lowassa. Wazungu wanakwambia divide and rule kamati ya Fitna ya kina Sitta na Mwakyembe ikaja kuwavuruga hapo ndio Things fall apart Lowassa Uvumilivu ukamshinda akabwaga manyanga hakutaka kukomaa nao JK akapambana mwenyewe mpaka muhula wake ulipoisha wakati huo tayari JK alikua kashazungukwa na team Mwakyembe.
 
Kwa mtazamo wangu kilichokuwa kinawaunganisha ni maslahi.Ukiondoa maslahi hawajawahi kuwa marafiki hata kidogo.
Maslahi ndiyo chanzo cha maelewano, mahusiano na urafiki.
Urafiki hufa kwa kukosekana mambo hayo
 
richmond ni picha tu imetengenezwa.hakukua na kitu cha.namna hiyo.
kilichomponza lowasa ni tamaa ya uongozi tu basi.

na yule mkwele alimwambia hicho unachotaka hukipati labda nife kesho.
hapo ndio ulafiki ulipoishia.
ndio ujue mkwele sio mtu mzuri.
 
Back
Top Bottom