BARD AI
JF-Expert Member
- Jul 24, 2018
- 3,376
- 8,120
Rais Mstaafu wa awamu ya nne, Jakaya Kikwete ametoa kauli hiyo baada ya kufika kutoa pole ya Msiba nyumbani kwa Waziri Mkuu Mstaafu, Hayati Edward Lowassa aliyefariki dunia Februari 10, 2024 wakati akipata matibabu katika Hospitali ya Moyo (JKCI).
Akizungumzia kiongozi huyo, Kikwete amesema Mwaka 2005 tulipoteuliwa kugombea Urais, mwenzangu akaja kuwa Waziri Mkuu tukapata changamoto katikati mwenzangu ikabidi akae pembeni, tukaendelea kuwa pamoja kuwa marafiki na kushirikiana kwa kila linalowezekana"
Kikwete ameongeza kuwa Lowassa ametoa mchango mkubwa katika taifa na yaliyotokea ni changamoto katika maisha lakini hayafuti mema na mazuri aliyofanya kwaajili ya nchi.