Drifter
JF-Expert Member
- Jan 4, 2010
- 4,436
- 4,151
I declare interest Mimi ni muumini wa Kikwete na Lowassa, Historia inaeleza kua hawa jamaa walikua marafiki wakubwa sana mpaka lilivokuja suala la Richmond inasemekana ndio lililowavuruga
Lakini pamoja na kugombana mmoja akiwa ni mwenyekiti wa CCM taifa mwingine akiwa mgombea urais wa chama pinzani lakini bado waliheshimiana hawajawahi kutukanana jukwaani ninachokumbuka Mimi kuhusu Lowassa kila akipanda jukwaani alikua anasema rafiki yangu kaharibu nchi wakati Jk alikua akisema mwenye Richmond chadema wanae hakuwahi kumwita Lowassa fisadi.
Natamani tupate mwandishi mmoja afanye interview na hawa jamaa aangalie Historia yao wapi wametoka mangapi wamefanya pamoja je nini kiliwagombanisha na status yao kwa Sasa ipoje, nadhani itakua documentary nzuri mno.
Sent from my TECNO RA7 using JamiiForums mobile app
Angalia kwa upana zaidi.
Katika huo “ustaarabu” wao katika harakati zao za kisiasa, hawa wawili ni miongoni mwa vinara walioasisi na kuneemesha ufisadi mkuu wa kimfumo ndani ya serikali na CCM yake.
Enzi zao ndipo mikono ya Ikulu ilikuwa ikionekana wazi katika dili kubwa kubwa nchini. CCM iligeuzwa chombo cha wafanyabishara hasa watu kati (middle men/agents of the state) kufanya yao bila bugdha na fursa kadhaa za uongozi wa kisiasa serikalini zikawa kwa ajili ya wawezeshaji, washikaji na michepuko.
Richmond ilikuwa dili yao wote, ila Msoga, aliyekuwa smart zaidi kisiasa, akaona fursa kumuangushia jumba bovu mwenzake akose sifa za kugombea uRais awamu inayofuata. Kama roho mbaya vile.
Hicho kitabu kikiandikwa, itapendeza zaidi kikipewa title ya: “The Classic Partners in Crime”.