Vijana Fanyeni Michezo Ili Kuimarisha Afya Zenu na Kutimiza Malengo na Ndoto Zenu

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
1,898
942

NAIBU WAZIRI CHILO: VIJANA FANYENI MICHEZO ILI KUIMARISHA AFYA ZENU NA KUTIMIZA MALENGO NA NDOTO ZENU

Mbunge wa Jimbo la Uzini Muheshmiwa KHAMIS HAMZA CHILO Amewataka Vijana (Wanamichezo) wa Jimbo la Uzini kufanya Michezo kama sehemu ya Kuimarisha Afya zao na Kukuza Vipaji na Kitimiza Ndoto zao za kuchezea mpira kwenye Team Kubwa za Kitaifa na Kimataifa

Muheshmiwa KHAMIS HAMZA CHILO Amesema hayo alipokua akifunga Finali za Kombe la Ng'ombe kwa Vijana wa Jimbo la Uzini Ambao walifikia Finali ya Kombe hilo

Muheshmiwa KHAMIS HAMZA CHILO amewaambia Vijana hao Lengo la Kuanzisha kwa Kombe hilo ni kuwakusanya Vijana ili waweze kuendeleza Vipaji vyao na Kuwatimizia Ndoto zao ...

Muheshmiwa KHAMIS HAMZA CHILO Amesema wakati wanapita Wanaomba Kura waliwaahidi Vijana kua watakapowapa kura Watashirikana nao katika Kuinua Sekta ya Michezo kwa Vijana hao na Sasa ndicho kinachoonekana ndani ya Jimbo la Uzini

Nae Mwakilishi wa Jimbo la Uzini Muheshmiwa HAJI SHABAN WAZIRI alisema kua Vijana ndio Tegemeo la Taifa kwa hiyo Vijana waendelee kutoa Ushirikiano wao kwa Viongozi kwani Viongozi wao Tunafanya mambo Mengi ndani ya Jimbo la Uzini

Nae Rais wa Chama cha Mpira Zanzibar Ndugu SULEIMAN MAHMOUD JABIR aliwataka Vijana hao kucheza Mpira wa Kistaarabu kwani wote ni wamoja na Taifa Linawategemea hivo hawana haja ya Kugombana na Kufanyiana Fujo ...

Finaly hiyo haikupatikana Mshindi kwani mpaka dakika za Mwisho Team hizo zilitoka sare na hatimae Ng'ombe bado yupo Zizini anaendelea Kula Majani

Mtanange huo Utachezwa tena Siku ya Jumaapili kwenye Uwanja wa Blue Star Mwera ili Apataikanwe Mshindi na Apewe Ngombe wake na Zawadi nyengine...

UZINI HATUPOI WALA HATUBOI KAZI INAENDELEA
 

Attachments

  • WhatsApp Video 2023-07-31 at 08.26.18.mp4
    9.2 MB
Stress nnazopitia kwa Kukosa ajira ni zoezi tosha. Hebu anishauri mambo mengine ya kuniingizia kipato
 
Stress za maisha magumu na kukosa ajira baada ya kusoma kwa mkopo huku familia ikitegemea maajabu baada ya masomo yangu ni zoezi tosha.
 
Back
Top Bottom