Video: Tundu Lissu atoa ufafanuzi wa hoja aliyoitoa Babati Aprili 26, 2024 kumjibu Fatma Karume kuhusu 'Ubaguzi na Muungano wetu'

Zanzibar wenzetu wapo dunia nyingine ,hasa huwaga najiuliza inakuwaje wenzetu bei zao za mfano simu, laptops, fridge na electronics Kwa jumla wanauza Kwa bei mzuri kuliko huku kwetu.
 
Sawa, lakini fahamu kuwa haikuwa lawama kwako. Unapofanya 'sweeping statement' kama ulivyofanya, inakuwa ngumu sana kutetea hoja unayoiwasilisha.
Hiyo siyo "sweeping statement" au "general statement" kama ulivyosema hapo awali ndugu Kalamu...

Nilichokiandika ndiyo ukweli wenyewe kwa sababu huu muungano umri wake ni miaka 60 sasa. Hilo lina ubishi brother?

Mimi nikafikiri kwa kuwa huu ni mjadala, mtu yeyote anaweza kutupia mawazo mbadala yakiwa ktk mrengo wowote kukosoa, kukubaliana na hata kukejeli.

Na ndiyo maana nikakushauri kuwa unaweza kurekebisha palipo na kasoro kwa kuweka mawazo yako..

Hakukuwa na ubaya wowote kama na wewe ungesema, kuwa, matatizo ya muungano yalikuwa intensified zaidi baada ya Zanzibar kuwa na katiba yao mwaka 1984...

However, I appreciate for being thoughtful...
 
Dodoma ninayoizungumzia ni ile aliyoizungumzia Lissu katika Video. Kama hujaisikiliza hiyo video (ipo kwenye uzi huu), tafadhali isikilze kwanza ndio twende pamoja. Katoa mfano wa idadi wapiga kura wa Dodoma na wabunge wake akilinganisha na wale wapga kura wa Zanzibar na wabunge wake. Kazi kwako, ndio urudi tujadiliane.
Sifa za majimbo ya uchaguzi muulize Lissu, kwa maana mimi nikiziorodhesha hutridhika. Ngoja huyo mchungaji Lissu aseme hadharani. Ndio utajua kuwa una mchungaji BAGUZI, na hana tofauti na wale makaburu wa A. kusini ktk miaka ya 1960. Aende Ubelgiji akaishi huko.
 
Hoja yako ni nini hapa?

Au huna bundle (MB) kufungua na kusikiliza video na kuelewa kilichozungumzwa?

Majibu ya maswali yote uliyouliza yamo kwenye maelezo ya TL kwenye video clip hiyo. Sikiliza tena, acha uvivu..
Sina shida na bando, lipo bila kikomo. Nimeiasikiliza video yoteee, na kuelewa jinsi alivyokuwa mbaguzi. Hakika nakwambia, kosa CHADEMA mtalifanya ni kumchagua Lissu kuwa mgombea wenu wa urais 2025. Hana point zaidi ya kuzungumzia UBAGUZI.

Watanzania wanataka kusikia jinsi akiwa rais atawatatulia matatizo ya miundu mbinu, Pembejeo, rushwa, tatizo la ajira, mikopo kwa wanafunzi, huduma za afya- bima, Mwendokasi, umeme, maji n.k.
Lissu anatumia siku nzima kuzungumzia UBAGUZI. Loooooooo!
 
Kama wewe ni Daktari, endele na kazi ya utabibu. Ila ushauri wangu uanze kwanza kupima akili ya Lissu.
Kuhusu changamoto za katiba: Katiba zetu zote mbili zina changamoto na ndio maana Tulikuwa na Tume ya Warioba. Na huwezi kubadili katiba ya Muungano kwa mapendekezo yale ya Tume ya Warioba bila kubadili katiba ya Zzibar. Kwenye hili sinatatizo.

Tatizo la Lissu ni jinsi anavyolielezea Hilo tatizo kiubaguzi baguzi. Tatizo hilo limeelezewa na viongozi wengi, kwanini sikuwaita wao wabaguzi. Achana hoja hii, hoja zake nyingi maelezo yake yameelemea kwenye ubaguzi. Kama mwanasiasa ni lazima achague lugha nzuri la kuwakilisha tatizo na awe mkweli kitaaluma yake na kama mwanasiasa. Huyu ni mbaguzi namba 1 Tanzania, sipati neno jingine mbadala.
 
Huyu mwamba ni harari
 
Rais Samia amewahi kusikika akisema yeye ni MZANZIBARI. Kwa hiyo sio ubaguzi kusema Raisi ni Mzanzibari, kwasababu haya yeye mwenyewe anajivunia kuwa Mzanzibari.
Ndugu usiturudishe nyuma au kututoa katika mada. Kwani wewe hujivunii mkoa uliotoka, au wilaya, tarafa. Kwani ni dhambi kusema Nyerere anatokea Butiama, au Mkapa kusini, au Kikwete Pwani? Ngoja nisipoteze muda hapa.

Sikiliza video ya Lissu vizuri akiwa umasaini utaelewa tunachompinga? na utaelewa kwanini tunamwita Mbaguzi. Bila kusikiliza video hiyo ya awali, hutaweza kujadili uzi huu, kwani utakuwa umeikosa point kubwa iliyozua hisia za watanzania mpaka kumwita mbaguzi.
 
Ajira za watendaji kata 2019 Moja ya vigezo vya kuajiliwa ilikuwa ni lazima uwe na kadi ya chama cha mapinduzi (mwanachama) na katibu wa wizara ndiye alishughurikia huo Sasa ndii ubaguzi kamili achana na hizo nyingine ni porojo za CCM
 
Tatizo la Lissu ni jinsi anavyolielezea Hilo tatizo kiubaguzi baguzi.
Justify huo ubaguzi wake..
Tatizo hilo limeelezewa na viongozi wengi, kwanini sikuwaita wao wabaguzi.
√ Viongozi gani hao wengi walioeleza la muungano?

√ Na kama hao "viongozi wengi" kwa mujibu wako wameelezea tatizo hilo kama anavyoelezea Tundu Lissu na bado hukuwaita wabaguzi kama unavyosema, leo kimekupata nini kumwita huyu mwamba kuwa ni mbaguzi?

√ Au una confusion fulani🤔?

√ Kwa akili yako wewe, unadhani watu wanahitaji maelezo au vitendo?
Achana hoja hii, hoja zake nyingi maelezo yake yameelemea kwenye ubaguzi.
Narudia tena kukuambia.

Hebu Justify hoja yako kwa uthibitisho na mifano ya ubaguzi huku ukikumbuka kuwa msingi wa matatizo ya muungano wetu ni YA KIKATIBA kila anachosema Tundu Lissu reference yake ni KATIBA ya JMT (1977) na ya ZANZIBAR (1984).. Hata Uzanzibari wa Rais Samia Suluhu Hassan unatajwa ktk katiba..
Kama mwanasiasa ni lazima achague lugha nzuri la kuwakilisha tatizo
Lugha nzuri na mbadala ya kusema kuwa "Rais Samia Suluhu ni Mzanzibari" unadhani ni ipi? Hebu tufundishe na sisi tuelewe..
na awe mkweli kitaaluma yake na kama mwanasiasa.
Ukweli upi wa ziada unaofikiri hakuusema zaidi ya ukweli wa kunukuu ibara za katiba ya JMT na Zanzibar?

Unajua kuwa hueleweki ndugu Zawadi Ngoda??
Huyu ni mbaguzi namba 1 Tanzania, sipati neno jingine mbadala.
Narudia tena, acha kupayuka na kubwatuka tu kama mbwa koko..

Justify ubaguzi wake kwa kuzingatia misingi ya katiba ya Tanzania na Zanzibar..!
 
Vita mnapigana na nani ebu ficha ujinga wako
 
Critical analysis za hivi Zina miss Tanzania. Ilitakiwa awepo mwingine mwenye counter analysis Ili kuwe na balanced opinion...

Taifa lisilo na critical thinkers will never stand the test of time...Tuanze sasa kujifunza kuwa na critical thinking kwakuondoa zile siasa ambazo ni dominant kwenye nchi za kijamaa...Watu walizoezwa kumezeshwa maoni ya watu bila kuzifanyia critical analysis...Hapa ndipo JKN aliteleza. Ki detain wote wenye different perspective Kinyume Cha kile anacho amaini yeye...Akijiwekea ulinzi i.e Katiba (ambayo ndiyo mpaka sasa Kila mtawala akionja hataki kubadili aendelee kuonja sifa ya ki Mungu huku duniani), ya yeye kusema anachotaka wakati wowote bila kuwajibika Kwa yeyote, na ...Ilitegemea hisani yake wengine kupata hiyo privilege and only when ni mpendwa wake...This was a very bad precedence aliyo I set na ndiyo sababu ya watanzania kuwa jinsi hii Leo, wapo passive Kwa Kila kitu
 
Kwa mara ya kwanza Lisu ameni inspire, anaonyesha critical thinking ya hali ya juu. Kimoja tu sikipendi Kwa Lisu na CHADEMA ni kutafuta alliance na mataifa beberu, but then nikijiweka kwenye nafasi yake angefanyaje wakati huku nako tuna wakoloni weusi wamefanya state capture?

Waafrika na watanzania tupo kwenye dilemma isiyomithilika ni Mungu mwenyewe atusaidie!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…