Video: Kova azungumzia sakata la Jerry Muro

Mkuu Maggid! ujumbe ni nzito na inauzunisha na kusikitisha na kwa upande wa Jerry kweli yuko kwenye kipindi kigumu na kizito kwa upande mwingine kwa waliobaki (wanahabari) wajue wapo kwenye mapambano wasirudi nyuma hayo ni mapito ya hali ya hewa, kuna kiangazi, kipupwe, masika hivyo vyote ni vipindi vya mipito vya majira ya hali ya hewa. Daima mapambano mbele kamwe wasirudi nyuma
 
Tungalie hii ngoma. Ila mdundo wake mkubwa sana!
Tanzania sio kuna miujiza au vituko ila ni kichaa, nimesafiri kutoka Mwanza kwenda shinyanga kwa gari njiani kuna Check Points za Jeshi Tukufu la Polisi zaidi ya Sita na zote zina polisi wenye SMG waliovaa ki Raia(Wasio na Vazi Rasmi) Wanaonekana kama Vibaka, Je utaweza kutambua Check Point ya Polisi au Majambazi.
Tena Wanakagua kuanzia Wasafiri mpaka kazi za Traffic.
 
Tanzania sio kuna miujiza au vituko ila ni kichaa, nimesafiri kutoka Mwanza kwenda shinyanga kwa gari njiani kuna Check Points za Jeshi Tukufu la Polisi zaidi ya Sita na zote zina polisi wenye SMG waliovaa ki Raia(Wasio na Vazi Rasmi) Wanaonekana kama Vibaka, Je utaweza kutambua Check Point ya Polisi au Majambazi.
Tena Wanakagua kuanzia Wasafiri mpaka kazi za Traffic.
ukitaka kujua Police hawatimizi wajibu wao ni pale nilipposafiri kwa gari la ofisi lenye namba za kibalozi toka Dar es salaam mpaka Kigoma, kweli hakuna polisi alienisimamisha wala nini, unafika mahala polisi anakupungia usimame ukipunguza mwendo akisoma namba za kijani anakuashiria uondoke, mimi nauliza wavunja sheria ni watu wenye magari binafsi tu ama ?
mimi naamini Rushwa iliostukiwa na Muro ndio chanzo cha yote yanayompata.
 
Muro aliyetinga ofisi za gazeti hili jana Jumatatu alisema kuwa, mpango mzima wa kukamatwa kwake ulisukwa na baadhi ya polisi ambao walimpigia simu kumjulisha kuwepo kwa mkutano wa waandishi wa habari kwenye Hoteli ya City Garden, Posta jijini Dar es Salaam.

Alisema kuwa, alipofika hotelini alimtafuta aliyempigia simu kabla hajashuka garini lakini haikupatikana na ghafla polisi mmoja alimgongea dirisha la gari yake na kumwita mzee mmoja ambapo alimuuliza, ‘Huyu ndiye Jerry Muro?'

Yule mzee alipojibu kuwa ndiye, Muro akashangazwa baada ya kuona askari sita wenye silaha wakimzunguka na alipowauliza kuna nini, wakamwambia anatuhumiwa kwa kuomba rushwa ya shilingi milioni 40 kwa yule mzee.
Aliongeza kuwa, aliwajibu kuwa alikwenda pale kwaajili ya mkutano wa waandishi wa habari na akawauliza kwamba, inawezekanaje aombe rushwa akiwa na kamera na ‘tepu' za kurekodia. Aliwataka askari hao wafuatane naye Polisi Kituo cha Kati kwenye usalama.

Uchunguzi wa UWAZI umeonesha kuwa sakata zima la kukamatwa kwa Muro limejaa utata.
Utata huo unadaiwa kunatokana na kuwepo kwa vipengele vitano visivyokuwa wazi vikiwemo: Weledi wa mtoa taarifa, Kujichanganya kwa taarifa, Kauli za mtoa taarifa, Kukamatwa kwa Muro na Maelezo ya Kamanda Kanda Maalum Dar es Salaam, Suleiman Kova.

Weledi wa mtoa taarifa
Uchunguzi wa gazeti hili umebaini kuwa mtoa taarifa huyo, Wage ni msomi ambaye alikuwa Mhasibu wa Wilaya Bagamoyo, hivyo kwa upeo wake ni wazi kuwa anaelewa majukumu na kazi za Jeshi la Polisi na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) ni yapi.

Ni wazi kuwa taarifa yoyote kuhusiana na rushwa, wanaopaswa kuweka mtego na kukamata watoa rushwa na wapokeaji ni maafisa wa Takukuru.

Kitendo cha Wage kupeleka taarifa za kudaiwa rushwa ya shilingi milioni 10 kwa polisi badala ya kwenda Takukuru tunaweza kufananisha na mtu aliyepigwa kisha akakimbilia kushitaki katika Kambi ya Jeshi la Wananchi badala ya kwenda polisi.
Swali hapa ni: Je, ni kweli kuwa Wage hakuwa akielewa ni wapi alipaswa kupeleka tuhuma hizo?

Kujichanganya kwa taarifa
Taarifa alizotoa Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Suleiman Kova, siku ya Jumapili iliyopita zinasema Muro alijitambulisha kwa Wage kuwa yeye ni Afisa wa Takukuru, hivyo apewe pesa ili asimfichue maovu yake.
Wakati huo huo, baadhi ya vyombo vya habari viliripoti kuwa Muro alikamatwa kufuatia polisi kuarifiwa na mfanyabiashara mmoja ambaye hakutajwa jina, kwamba amedaiwa rushwa. Je, taarifa ipi ni sahihi?

Kauli za mtoa taarifa
Mtoa taarifa wa tukio hilo Bw. Wage aliripotiwa na vyombo vya habari kuitaarifu polisi kuwa kuna watu waliomfuata, waliojitambulisha wanatokea Takukuru, wakimtaka awape sh. milioni 10 ili wasitoe taarifa zake za ufisadi zikiwemo za kumiliki nyumba za kifahari na akaunti zenye pesa nyingi, kwenye kipindi maalum katika runinga na baadaye kumchukulia hatua za kisheria.
Swali ni: Je, watu wa Takukuru hutangaza tuhuma za watu katika vyombo vya habari?

Kukamatwa kwa Muro
Kwa mujibu wa Kamanda Kova, baada ya kupokea taarifa ya Wage walikwenda katika Hoteli ya City Garden, sehemu ambayo inadaiwa mlalamikaji aliahidiana kukutana na Muro na wenzake ili awape pesa na walipofika hapo makachero wa polisi wanadai walishuhudia kumuona mtuhumiwa akija na gari lake kisha akamuita kwa ishara mlalamikaji.

Mlalamikaji akaonesha ishara kwa makachero aliokuwa nao kuwa aliyekuwa akimuomba rushwa amewasili, ndipo walipolizunguka gari na kumhoji Muro kama anafahamiana na Wage ambapo alikataa kumfahamu.

Kukataa huko, hata hivyo, kulipingwa na mlalamikaji ambaye alisema kuwa wanafahamiana na walishawahi kukutana Januari 28 na 29 mwaka huu Muro akiwa na wenzake ambao walimuomba pesa za rushwa na ushahidi akasema ni miwani yake na tishu ambavyo aliviacha katika gari la Muro.

Walipolikagua gari walivikuta vitu hivyo. Swali ni: Je, kwanini makachero hawakusubiri pesa itolewe ndipo wamkamate?
Kova naye

Kamanda Kova alisema aliarifiwa na mlalamikaji kuwa wanaomdai rushwa ni maofisa wa Takukuru. Swali ni: Je, kwanini hakuwasiliana na uongozi wa Takukuru ili watu hao wanaswe?
Wananchi je?

Ukiachilia maswali hayo, baadhi ya wananchi walioongea na Uwazi walidai kwamba, kukamatwa kwa Muro inawezekana ikawa ni mipango ya polisi baada ya mwandishi huyo kufichua uozo wa rushwa kwa baadhi ya askari wa jeshi hilo na kuichafua taswira yake.

"Hii itakuwa kwa sababu aliwaandika polisi tu. Unajua hata mwaka 1996 mwandishi wa IPP, mkoani Ruvuma marehemu Adam Mwaibabile aliwahi kukamatwa kwa tuhuma za kukutwa na nyaraka za serikali na akafungwa miezi sita lakini akakata rufaa na kushinda kesi huku taarifa kuwa alikosoa uozo fulani wa uongozi wa mkoa ikitajwa," alisema mwananchi aliyejitambulisha kwa jina moja la Hussein mkazi wa Mwenge Dar es Salaam.

Mwingine naye alidai kuwa Muro ametegwa kutokana na ujasiri wake wa kuripoti rushwa ambayo ni njama inayofanywa na baadhi ya polisi kama alivyofanyiwa mwandishi wa Nipashe, Zephania Msendo, mwaka 2004 baada ya kuripoti habari mfululizo kuhusu uozo uliokuwa ukiihusu Takukuru ambapo alitiwa hatiani na kufungwa miaka mitatu.

Hata hivyo, akiongea na waandishi wa habari jana Jumatatu, Kamanda Kova alisema polisi bado wanaendelea na uchunguzi wa tukio hilo na faili lake watalipeleka kwa Mkurugenzi wa Mashitaka kwa maamuzi.

Na kuhusiana na polisi kutumika kumkamata Muro badala ya Takukuru alieleza kwamba, hakuna ubaya juu ya hilo kwani, Takukuru ni taasisi ndogo kuliko jeshi lake.

Alisema kuwa licha ya Muro kukana kumfahamu Wage, picha za mwandishi huyo akiwa na mlalamikaji wakizungumza kwenye hotelini, siku chache kabla ya kukamatwa zinaonekana kwenye mitambo ya CCTV, kitu ambacho wengi wamedai kuwa alikuwa anafuatiliwa.

Kuona mahojiano kamili kati ya Uwazi na Jerry Muro tembelea mtandao wa Global Publishers unaopatikana kwa anuani ya www.globalpublisherstz.com
 
Kama hamjawahi kuona mtu anaongopa, anajikanyaga, ni Muro wa jana usiku kwenye kipindi alichokiasisi yeye mwenyewe. Kashfa hii labda izimwe kisiasa tu.
 
Hiyo miwani aliicha kwenye gari lini? Na alipanda gari ya Muro akienda wapi mpaka akaacha miwani humo?
 
Muro ni mtangazaji kijana ambaye anaisaidia jamii kwenye mapambano ya rushwa na wiki iliyopita aligonga kwenye vichwa vya habari kwa tuhuma za kulazimisha rushwa toka kwa afisa mfukuzwa wa Wilaya ya Bagamoyo!

Afande wa kanda maalum wa Dar Kova majuzi alihaidi kuliongelea suala hilo kwa upana siku inayofuatia na jana mbele ya waandishi wa habari akaanza kuzizungumzia tuhuma za kijana Muro.

Lkn badala ya kuanza kuziongelea tuhuma za kupokea na kuomba rushwa zilizovumishwa kuwa Muro alilazimisha apewe;badala yake kwa urefu kabisa Kamanda Kova akaanza kueleza jinsi polisi walivyomkamata mtangazaji Maro miwani yake meusi,bunduki waliyokiri baadae kama anamiliki kihalali; lkn wakasema kuwa alikutwa pia na pingu anazotuhumiwa kuwa hana kibali cha kuzimiliki na Kamanda Kova hata akatumia "masaa mengi" kuelezea kosa la kukamatwa na pingu na wala hakusema lolote kuhusu kosa kubwa la rushwa kama wengi tulivyotabiri!

Swali langu kwa kamanda Kova,je alikusanya waandishi wa habari lukuki kutueleza watz kuhusu kupokea rushwa kwa mtangazaji Muro au alikuja kutueleza jinsi ambavyo walimkamata mtngazaji Muro anamiliki pingu kinyume cha sheria?

Bila ya jibu anuwai nitahusisha na ukamatwaji huu wa Mtangazaji Muro na juhudi zake binafsi za kupambana na mafisadi!
 
Sitaki kuamini kuwa Muro alifuata rushwa ya milioni 10, nakataa, mimi niliangalia kipindi chake Usiku wa habari nakukatalia Wildcard eti alijichanganya HAPANAAAAAAAAAA nakataa, ofcourse Muro never expected all that from our police kwa hiyo bado yuko kwenye shock tena big time shock. Siamini kama ni mjingaaaaa kiasi hicho eti aende City Garden mwenyewe kufuata milioni 10, please give us a break. Hata kama ana njaa asingefanya hivyooooo siyo mjinga kiasi hicho. Of course anahitaji pesa, hakuna mtu asiyetaka pesa, Jerry Muro simjui ila naamini siyo TAJIRI kwa hiyo 10 m ni big money kwake na kwangu pia, ila bado nakataa aliifuata hiyo pesa.
Maggid, tafakari yako IMENIGUSA SANA!!! Kazi ipo....
 
Jana nilikuwa namsikiliza huyo Kamanda Kova hata sijaelewa alikuwa anongea vitu gani
maneno yako yako ni mazito na ya simanzi

Nami sijamwelewa kabisa huyo bwana wangemletea ule mtambo wa kupima maneno unayoyatamka wakati alipokuwa akiongea na wandishi wa habari ndipo mgejua kuwa kova na huwa anababaisha tu. Nimemsikia leo pia kupitia Clouds FM akiongelea pingu yani utajua tu msomi ni nani kama mtu ulie soma katika hali ile tete huwezi stick kwa point ya kuhoji pingu!!!!! ati mwandishi wa habari haruhusiwi kuwa na pingu, ivi J.Muro angekuwa amemkamata mharifu wanae mtafuta hao police wanagerikumbuka kumhoji J.Muro hizo pinguuuu???

Wao watujibu kwanini hilo tukio liko kiutata zaidi na halina maelezo yaliyo nyookaaa??? Investigations za Police wa kibongo ni hovyo hovyo sana huwa zina mambo behind either wana lao jambo au kumsaidia mtu au kumkandamiza mtu na sio kutafuta haki na ndio maaana wananchi huwachukia police.

Mfano Habari ile ya Arusha yule dada alie uwawa gatini kwake njiro ati baaada ya siku 2 ivi kukatokea majibizano ya risasi kati ya police na majambazi eneo wa mianzini soweto na wakauwawa majambazi wawili na wakasema mmoja wapo alihusika na mauji ya yule dada how? kithibitisho ni ile bastora iliyoyumika ndio waliyokutwa nayo how? what if aliye uwa nae alimwazima jambazi mwingine??

Suggestion: Police wote warudishe nyumba za kambini labda hapo ndipo wataelewa kufanya kazi huku changanyikeni tutakuja toana roho siku mmoja subirini.

 
Uzushiiiiiiiiiiiiiiii mtupuuuuuuuuuuu, police wetu wanaendelea kuchemkaaaaaa this time KOVA anachemkaaaaaa tena. Hii haijatulia duuuuuu police jipangeni upyaaa.

Viongozi wetu wa serikali punguzeni matumizi yasiyo ya muhimu, baneni matumizi, acheni UFISADI jamani tupeleke polisi shule, vyuoni, tuwapeleke mpaka nchi za nje China, Germany, USA, wakasome, naamini kabisaaaa polisi wengi walisoma shule za akina KAYUMBA, nadhani mnaeelewa, kwa hiyo wanahitaji ELIMU KUBWAA WANAHITAJI ELIMU YA WATU WAZIMA. Polisi waliosoma shule nzuri za St..bla bla., St. bla bla, St. bla bla ni wachacheeeeeee sanaaaaaa.
Tupeleke walimu, polisi, doctors, nurses, wakasome. Kesi ya Muro inaoonyesha kabisaa polisi wanahitaji kwenda shule zaidi na zaidi...
 
Anajikanganyaje embu tuambie we Wildbad, na wewe mwenzao nini hata mtoto ukimsumulia hii hadithi atakupatia jibu stahili, sema ukweli acha ukoplo wako,kama wangekua wanajiamini wakeenda moja kwa moja mahakamani kesi ngapi wanazipitisha kwa mwanasheria wa serikali hili limeshawavundia wanatafuta sababu ya kulizima acheni kukurupuka fanyeni kazi kwa kutumi taaluma na si simulizi
 
NI wazi kabisa Polisi wana mkono wao mkubwa tu katika tukio hili, SIna imani kabisa na Jeshi la Polisi tokea zamani, wanawabambikia raia wema kesi nyingi tuu, mungu naye hajaribiwi jamani hili litawatokea puani polisi hawa, sasa la rushwa limeshindikana mkazo ni PINGU, hahahahaha KOVA KOVA KOVA KOVA, MSALABA WA DHAMBI NI MAUTI BABA
 
Jeshi la Polisi limejaa ubabaishaji na dhuluma. Siamini chochote wanachosema hawa polisi, kwanza wanajidhalilisha kwa kukomalia ishu ya kipuuzi kama hiyo hadi kwa viongozi wa juu hivyo. Wananchi wananyanyasika hawana usalama wao wako bize kupiga siasa.

Usishangae kukuta kwamba Jerry alikuwa na story nyeti fulani ya kufichua wakawahi kumnyamazisha. Kama jeshi na serikali ingekuwa na upeo wangejua kabisa kwamba kwa kumnyamazisha mwanaharakati kunaua credibility yao tu. Kwa mtu aliyejingea heshima ya kazi yake kama Jerry, ingebidi polisi ifanye kazi ya ziada kupata kidhibiti kilicho wazi ndio njia pekee ya mtu yeyote kuwasikiliza otherwise haya mambo yao ya pingu na miwani ni upishi mtupu.

Tumechoka kuonewa na polisi kwa kodi zetu wenyewe. Tumechoka.
 
Sitaki kuamini kuwa Muro alifuata rushwa ya milioni 10, nakataa, ..............please give us a break. Hata kama ana njaa asingefanya hivyooooo siyo mjinga kiasi hicho. Of course anahitaji pesa, hakuna mtu asiyetaka pesa, Jerry Muro simjui ila naamini siyo TAJIRI kwa hiyo 10 m ni big money kwake na kwangu pia, ila bado nakataa aliifuata hiyo pesa..
Maggid, tafakari yako IMENIGUSA SANA!!! Kazi ipo....

To honestly mpwaa hakuna anae kubaliana na hao mapolice kwa wanachokisema Tanzania nzima kasoro hao mapolice wanaopenda chuki na watu, Kweli mtu mahili hawezi pokea rusha kishamba namna hiyo, hata kama ni mimi huniweki mtegoni kiasi hicho!

Kuna kipengere fulani Wage aliulizwa na police ndie huyu J.Muro akasema ndio na J.Muro alimkana pale pale hata kama ni mimi nakukana 7*70 maisha yangu kweli. Hapo ita leta hisia fulani kuwa kuna leak police walipata na wakajua J.muro anafuatilia huko bagamoyo na wao wakamfuata muhusika na wakamconvince nae akakubali kwani alijua fika labda ataponea hapo ila sasa ndio moto ameuanzisha inakula kwake mazima na serikali watu wa hazina wataanza kuichunguza ofice yake huko bagamoyo.

Hawa police wetu wanazidi kutuonyesha ni jinsi gani hawako capable na utendaji kazi wao. ivi huwa hawana mtu anayejua kureport mbele ya waandishi wa habari kila siku ni kova tu yeye anadhani kutolewa kwa runinga ndio fashion au?? kutoa habari you have to be smart na iyo position yapaswa mtu kuajiriwa ndani ya jeshi la police sio kuja tu na kubwabwaja mbele ya waandishi wa habari na umma unakuchambua uwezo wako wa kuongea pia kwa vyombo vya habari
 
KOVA kchemsha, nadhani walioko chini yake wamemdanganya kama Zombe alivyodanganywa wakati ule, Jerry alituhumiwa kupokea rushwa kubwaaaa, sasa suala si rushwa tena ni pingu, mwe KOVA give us a break!!!!!!!!!!!
 
Huwa nawaambia kuwa hii nchi ipo kwenye maajabu ya dunia kwa vituko na vioja!! Haya sasa mnaona ya Jerry.....
Mnaona ya Liyumba na mashahidi wa serikali.............
 
Jana nilikuwa namsikiliza huyo Kamanda Kova hata sijaelewa alikuwa anongea vitu gani
maneno yako yako ni mazito na ya simanzi
Yule mpenda sifa hutakaa kuja kumwelewa. Ndo maana mara nyingine huwa nakwepa kuangalia TV. Unakutana na mambo ya kijinga kijinga yanaelezewa kwa kupambwa na watu wakubwa mpaka unashangaa hivi sisi tunafikiria nini? Ndiyo hivyo kweli tulivyo?
What goes around comes around! Naona kama wameamua kumfix huyu kijana tu kwa ajiri ya corruption zao.
 
Back
Top Bottom