Jerry Muro amlipua Masha

nngu007

JF-Expert Member
Aug 2, 2010
15,862
5,797

Thursday, 18 August 2011 22:24
Nora Damian

ALIYEKUWA Mtangazaji wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC), Jerry Muro, anayekabiliwa na kesi ya kuomba rushwa ya Sh10 milioni, ameieleza mahakama kuwa aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Ndani, Lawrence Masha, alimtisha kuwa hatochomoka katika sakata hilo.

Muro alieleza hayo jana katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu alipoanza kujitetea kwa mara ya kwanza dhidi ya tuhuma zinazomkabili.Katika utetezi wake uliodumu kwa saa tatu akiongozwa na mawakili wake, Majura Magafu na Richard Rweyongeza, Muro alidai kwamba Masha alisema mwisho wa kesi hiyo unampeleka yeye (Muro) kaburini.

Alisema siku chache baada ya yeye kukamatwa, Masha akiwa waziri alimfuata ofisini kwake TBC Mikocheni na kumtupia bahasha ikiwa na maneno ya vitisho."Masha alinifuata ofisini, nikaenda kuongea naye lakini ghafla nilipoingia tu kwenye chumba cha mkutano alinitupia bahasha ya rangi ya kaki," alizidi kutoa madai yake Muro na kuongeza:

"Nilizifungua bahasha hizo na kukuta picha tatu za CCTV ambazo Masha aliniambia ni za kwangu, aliniambia kaka umekwisha, mimi naondoka na wewe lazima utaondoka."Hata hivyo, picha hizo ambazo zilitolewa na upande wa mashitaka kama kielelezo katika kesi hiyo, Muro alizipinga akisema hakuna sura yake na kinachoonekana ni maumbo tu ya watu watatu ambao hata sura zao hazifahamiki.

Alidai mahakamani hapo kwamba, Masha alimwambia (Muro) aitishe mkutano wa waandishi wa habari na kusema Jeshi la Polisi halijamuonea, ila wamegongana tu kwenye utendaji wa kazi, lakini yeye hakufanya hivyo.

Muro ambaye kesi yake imekuwa ikivuta hisia za watu, alidai kuwa baada ya kuanza kuripoti habari za uchunguzi amekumbana na zaidi ya matukio 15 yanayohatarisha usalama wake na kwamba, licha ya kuyaripoti polisi hakuna hata moja lililofanyiwa kazi.

Alidai kutokana na matukio hayo, bosi wake wa awali Mwenyekiti Mtendaji wa Kampuni za IPP Reginald Mengi aliamua kumnunulia bastola ili imsaidie katika usalama wake na kwamba, aliwahi kuitumia."Hata pingu niliamua kununua ili inisaidie pale ninapoona nimebanwa, nimkamate mwenyewe mhalifu, kwa sababu nilisharipoti matukio mengi polisi, lakini hakuna lililozaa matunda," alidai Muro.

Mtangazaji huyo alidai watuhumiwa anaoshtakiwa nao hawafahamu na kwamba, hajawahi kuwaona na hata Wage anayetajwa kwenye hati ya mashitaka kuwa alimuomba rushwa hamfahamu.

Alidai kuwa habari zilizomletea matatizo ni zile zinazohusu askari polisi wa Kikosi cha Usalama Barabarani kufanya ufisadi katika Uwanja wa Ndege wa Mwalimu Nyerere, biashara ya uchangudoa, rushwa kwenye rumbesa Njombe na uchunguzi wa raia wa Korea aliyekuwa amemilikishwa eneo kubwa la ardhi huko Bagamoyo, mkoani Pwani.

Aliendelea kudai mahakamani hapo kwamba, baada ya uchunguzi kuhusiana na suala la raia huyo wa Korea baadhi ya watu walimpigia simu na kumfuata ofisini na kumshawishi achukue rushwa ya Sh60 milioni, ili aachane na habari hiyo, lakini alikataa na kuirusha habari hiyo hewani.

Muro alisema hakuwahi kumuomba Wage rushwa ili asirushe habari zake za ufisadi, kwa sababu mtu huyo tayari alishavuliwa madaraka na Waziri Mkuu Mizengo Pinda, hivyo kwake (Muro) hakuwa habari.

Aliongeza kwamba, hata baada ya kufikishwa mahakamani na kushtakiwa bado ameendelea kupata majanga mengi yakiwemo kuachishwa kazi, kukosa zawadi yake ya Dola za Marekani 4,000 zilizotokana na kupewa Tuzo ya Mwandishi bora na Baraza la Habari (MCT), kukosa nafasi ya kwenda kusoma katika Chuo Kikuu cha Tumaini na kufukuzwa kwenye nyumba aliyokuwa amepanga.

"Kabla ya kuachishwa kazi nilikuwa nalipwa pesa kidogo, lakini walipomuondoa Tido hata kile kidogo nikawa sipati na hata zawadi yangu ya MCT hadi leo sijapewa," alidai Muro.

Aliendelea kudai kuwa, ndani ya Jeshi la Polisi wako wanaomkandamiza na wanaoendelea kumuandama na kwamba, mwisho wa kesi hiyo unampeleka yeye kaburini.

Muro aliiomba mahakama imuachie huru kwa sababu hakutenda kosa lolote na kudai kuwa ni njama watu wachache wenye lengo la kutaka kumwangamiza.Hakimu Frank Moshi anayesikiliza kesi hiyo aliiahirisha hadi Septemba 27. mwaka huu washtakiwa wengine watakapoendelea kujitetea.

Mbali ya Muro washtakiwa wengine katika kesi hiyo ni Edmund Kapama na Deogratias Mgasa ambao kwa pamoja wanadaiwa kumuomba rushwa Wage aliyekuwa Mhasibu wa Halmashauri hiyo ya Bagamoyo.Kapama na Mgasa pia wanadaiwa kujifanya maofisa wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru).
 
Aisee kama hali yenyewe ndo hii basi kuna kila sababu ya kuamini kwamba hii kesi ilitengenezwa ili kulipiza kisasi na inaonekana kama walioumbuliwa na vipindi vyake ndio wameamua kummaliza tena kwa kushirikiana na polisi ambao ni washiriki wakubwa wa ufisadi kutokana na ripoti za Jeri Muro.
Ushiriki wa Lau Masha unazidi kuongeza uzito katika kesi hii, si ajabu kukuta serikali imeshiriki kikamilifu kutengenezea hii kesi kwa nia ya kummaliza na kumnyamazisha kabisa.
Jambo jingine linalonishangaza ni aliposema hata kile kidogo alichokuwa akipata TBC baada ya kuondoka Tido macho kimesitishwa,ina maana hakuwa na mkataba wa ajira tbc alikuwa anapiga deiwaka ama alikuwa nao isipokuwa Mshana kaamua kumchinjia baharini!? Kwakweli jamaa akipangua hii kesi sijui kama atathubutu kuwagusa tena hawa mafisadi,ila namuombea kila la kheri ashinde kesi yake.
 
Babu seya tayari anakula ugali maharage, na muro anusia huko. Jamani uhuru hapa tz haupo. Hii sio haki. Mungu akuongoze kaka Muro. Kipindi chako kile cha TBC kimekuwa cha kijinga tu nw dayz.
 
This case will not take you to death Muro,i prophesy for you!
Just keep praying for God is advocate of the poor and oppressed.
he can make you a hero out of this case.
 
Tamaa mbaya sana na inaponza siku zote, huwezi kufanya kazi kama hiyo alafu ukawa na tamaa ya ndogo ndogo alafu ukadumu, nadhani watu waangalie jinsi ya kumsaidia maana kapata ajali kazini.
 
Hii ni hatari kwa Nchi yetu, Namfahamu Lau Masha ni mtu wa kumuogopa anapenda kweli Madaraka ni Dikteta kweli, anajua kudharau watu amesahau alikotoka

Nchi yetu ikiwa na watu kama Lau Masha that's the end of it... Angalia Jeshi letu la Polisi ndio limeweka hiyo kesi na kumlimbikizia Mafaili ya Uongo

Tunakwenda kubaya, Lau alipokuwa US alisomba Credit Card na kuzitumia zote na hakulipa hata kidogo akakimbilia Bongo Huyu mtu ni wa kuchunga Sana...
 
Sema wewe kiazi, nikisema mimi mhogo wauchungu.............

Well kapewa Pistol haushangai sasa akimpiga risasi mtu bila kumuua kaimfunga pingu na kumuacha au kumchukua kwa usalama wake ni mbaya?

Anajua wabaya wake wakimvamia hawata taka awe hai, Jamani pingu ni moja ya tool ya kujikinga, watu wengi nchi za magharibi wana Pistol na Pingu Pia kumzuia mhalifu asikimbie ni vibaya kwa huyo Jerry kuwa nazo?

Nyie kweli mna damu ya uonevu, Mmeona story yake wabaya wake ni watu wetu wa usalama wa Taifa...
 
Well kapewa Pistol haushangai sasa akimpiga risasi mtu bila kumuua kaimfunga pingu na kumuacha au kumchukua kwa usalama wake ni mbaya?

Anajua wabaya wake wakimvamia hawata taka awe hai, Jamani pingu ni moja ya tool ya kujikinga, watu wengi nchi za magharibi wana Pistol na Pingu Pia kumzuia mhalifu asikimbie ni vibaya kwa huyo Jerry kuwa nazo?

Nyie kweli mna damu ya uonevu, Mmeona story yake wabaya wake ni watu wetu wa usalama wa Taifa...

Siku zote mbaya wako ni wewe mwenyewe
 
Ki kweli nchi hii haina sheria yoyote ipoipo tu. Katika hali ya kawaida kama sheria za kweli zingekuwepo watu wangejiuliza kwamba hivi kesi hii ilikuwa wapi wakati kabla hajarusha vipindi vile?

Laiti kama tungekuwa na watetezi wa kweli suala hili lisingekuwa hata na nafasi ya kuwapotezea watu muda wao na hasa mpiganaji Muro, na suala tunalotakiwa kujiuliza ni kwamba wale waliomulikwa na Muro walichukuliwa hatua gani?

Nauliza hivi kwa sababu kufukuzwa kazi pekee haitoshi hasa ikizingatiwa kwamba kama walifukuzwa kutokana na ushahidi uliopatikina kutokana na kazi za Muro wangepaswa kuwa na shauri la kujibu mahakamani.

Bahati mbaya ni kwamba inasemekana kwamba kuna uwakala na mgao unaopatikana baada ya kuwabambika watu makosa barabarani hata baadhi ya ma RPC (kama sio wote) wanasemekana kuhusika na yatokanayo, hivyo alichofanya Muro ni kwamba alijeruhi watoto wapendwa na mawakala wa wakubwa ndani ya jeshi la polisi.

Nchi ya viongozi mafisadi tuombe mungu, tufanye kazi na tuache ushabiki. Anachofanyiwa Muro ni moja tu ya maonevu mengi wanayofanyiwa wapiganaji wa kweli mbalimbali ndani ya nchi hii.

Tufanye kazi bila woga kama Muro tutaja kumbukwa kwa kazi tunazolifanyia taifa na sio kwa unafiki na kujipendekeza kwa mafisadi.
 
nchi hii sasa inaonekana ni nchi ya dili kwa wageni wakati sisi wenyewe tunamalizanan
 
Back
Top Bottom