Vick Kamata: Utajiri hu unahitaji maelezo ya ziada

Vick Kamata: Utajiri hu unahitaji maelezo ya ziada

What's the big deal in your thread? Kuchakalika kote huko ulikosimulia tangu Mwalimu huko Kilimanjaro, Bongo Fleva, BoT etc wewe huoni Kuwa yuko focused?

Sent from my BlackBerry 8900 using JamiiForums
 
Mtoa mada usikuze vitu kumharibia huyu mama. X5 unaipata kwa m hamsini. Alteeza m nane. voxy kila mtu anajua yanauzwa kwa mafungu. Isitoshe mwenyewe umekiri huyu mama anasomesha watoto kibao maskini. Niambie kuna mbunge mwingine anafanya hivyo ? VK ana mgody big up VK. raha ya wa tz ninkuona migodi ikimilikiwa na wageni. mwanamama ameonyesha njia kwamba hata mtu aliyeyoka familia duni anaweza. Hivi. ngoja niulize kila mwanamke akifanikiwa lazima awe kitu ya mzee fulani ? Rwakatare nae ni kitu ya mzee fulani ? pigeni kazi acheni mambo ya kike. mtoa mada hapo ulipo hujawahi kumsaidia mtu hata siku moja.


Mkuu mtoa mada amenukuu gazeti.
Gazeti ndo halijawahi saidia! Teh


Sent from my iPhone using JamiiForums app.
 
Wabongo wengine wananishangaza sana.

Upande mmoja wanakumbatia mfumo wa soko huria, ambao unaruhusu utajiri wa mtu uwe siri yake na taasisi za kibenki / kodi, upande mwingine bado wanakumbatia kufuatiliana kwa habari za "utajiri wako umeupataje" kama bado tupo zama za kikomunisti.

Soko huria linampa mtu uhuru wa kuficha habari za jinsi alivyoupata utajiri wake, unless kuna reasonable doubt inayoweza kujenga kesi dhidi yake.

Akikwambia hawezi kukwambia chanzo cha utajiri wake kwa sababu ni "trade secret", akikwambia utaitumia njia hiyo hiyo na si tu kumpiku, bali kumharibia uwezo wake wa kuendelea kupata utajiri, utamjibu vipi?

Sitaki kupinga kabisa relevancy ya kuuliza utajiri wa watu. Lakini pia sitaki watu waanze kurudi kule kwenye tabia ya choyo ya "bora wote tuwe masikini, ukiweza kupata kidogo tu lazima tukuwekee a witchhunt kukuuliza umepataje utajiri".

Swali si amepataje utajiri.

Swali ni, je mna sababu ya kumuuliza hivyo bila ya kuuingilia uhuru wake wa faragha katika mambo ya kiuchumi?

Swali ni, kuna a reasonable amount of doubt/ suspicion to warrant the question in the first place?

Kuwa tajiri si kosa. Kuwa tajiri kwa njia zisizojulikana si kosa (kuna sababu ya ku protect trade secrets kama tulivyoona hapo juu).

Unless mnaweza kuonesha kosa sehemu, au mwenendo unaoweza kutikliwa shaka, hii habari nzima ni witchhunt tu inayoweza kuvikwa joho la wivu, choyo na kijicho.


Mkuu wivu...choyo ...kijicho ndio nini?

hivi vitu vipo?

vinapimwaje?
 
Vic hongera kama kweli una watoto 75 wasiojiweza unaowasomesha, hiyo tu kwangu inatosha kuona hata kama umehodhi ni halali, kwani kuna watu kila siku tunasikia wanauwa tembo,wanfunga mikataba ya madini na kuingia mikataba bubu. Inayowamasikisha watanzania na kujinufaisha wenyewe na kupeleka fedha zao nje ya nchi, utafikili hawafi, mama angu na hako ka mgodi we miliki tu kikubwa uongeze idadi ya kuwasaidia wenye uhitaji sio unaowahitaji ww, kama vipi tutakuchagua kwa kura next uchaguzi

Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums

WAMA part 2, anamuiga bi mkubwa.
 
Unatumia kigezo gani cha kufananishaje utajiri wa sugu na vick.

Mwambie bwana, hata status yao kwenye muziki ni tofauti sana. Sasa mpwa, tupiamo basi hata kapicha tuonage hilo gholofa. Kama hukuchukua jitahidi upite tena uturushie tuangalie macho tu
 
wanawake na maendeleo, tufanye kazi, tusonge mbele, yelele…yelele… hii sehemu ya mashairi ya wimbo wa staa wa muziki wa kizazi kipya na mbunge wa viti maalum (uvccm), geita, vicky kamata anayetajwa kuwa na utajiri balaa. Vicky amepata mafanikio makubwa ambayo kila mwanamke tanzania angependa kuyapata.

Kabla ya siasa, kabla ya bongo fleva kabla ya siasa aliishi maisha ya dhiki ambayo hakutegemea kama angekuja kupata mafanikio makubwa. Ni miongoni mwa watanzania waliozaliwa katika familia duni. Katika kutafuta ‘kutoka’ kimaisha, vicky amewahi kuwa mwanamuziki wa bongo fleva na kutunga nyimbo mbalimbali, wimbo wa wanawake na maendeleo ndiyo uliomtambulisha zaidi katika jamii. “nimezaliwa kwenye familia duni, nimeishi maisha ya dhiki sana, mbali na muziki, nimewahi kuwa mwalimu wa shule ya msingi kule moshi (kilimanjaro) katika harakati za kusaka maisha, baadaye nilikwenda morogoro. “kila kitu kinabadilika kama ukimwamini mungu,” alisema vicky mwenye watoto wawili, revocatus na glory (jina la baba halikutajwa).

Mafanikio yaanza mwaka 2006, vicky alifanikiwa kuajiriwa na benki kuu ya tanzania (bot) akiwa ni afisa uhusiano. Mwaka 2010, vicky alifanikiwa kuwa mbunge wa viti maalum akiuwakilisha mkoa wa geita.

Mjengo wa ghorofa mbili akiwa mbunge, mheshimiwa vicky ameingia kwenye orodha ya wanawake mabilionea nchini kwa kuangusha mjengo wa kifahari wa ghorofa mbili sinza jijini dar es salaam wenye thamani ya shilingi bilioni moja na milioni mia nne. Ndani ya ghorofa hilo kuna bwawa la kisasa la kuogelea ‘swimming pool’ ambalo linatumiwa na familia yake.

Magari yake sasa kama walivyo matajiri wengine, mheshimiwa huyo anamiliki magari manne ya kifahari, yote yakiwa na thamani ya shilingi milioni 261. Ana toyota voxy- noah ambalo alilitoa sokoni kwa shilingi milioni 16. Kamata pia anamiliki bmw x5 likiwa na thamani ya shilingi milioni 130. Mara nyingi anapokwenda bungeni, vicky hutembelea gari linalomudu mikiki ya barabarani, toyota land cruiser ‘vx’ ambalo lina thamani ya shilingi milioni 90. Pia mwanamama huyo ana gari aina ya toyota altezza alilolinunua kwa shilingi milioni 25.

Anamiliki mgodi wa dhahabu wakati hayo yakiwa wazi, chanzo makini kilidai kuwa, mheshimiwa huyo amenunua mgodi wa dhahabu geita, jambo ambalo ni sehemu kubwa ya mafanikio yake. “vicky amenunua mgodi wa dhahabu geita, mimi ni mtu wangu wa karibu, hapendi kusema mafanikio yake wala watu wajue lakini ukweli ndiyo huo. Eneo ni kubwa, muda si mrefu uchimbaji utaanza,” kilisema chanzo cha habari.

Ana shamba la ekari 157 utajiri wa mheshimiwa huyo unaendelea kuanikwa kuwa, ni pamoja na shamba lenye ekari 150, kisarawe, mkoa wa pwani. Pia ana shamba la miti kibamba, dar lenye ekari 7. Ni mfugaji mbali na mambo mengine, vicky ni mfugaji kama ilivyo asili ya wasukuma. Anafuga ndege aina ya kanga, kuku wa kisasa na mbuzi.

Anasomesha watoto wasiojiweza katika mambo ambayo huenda yanachangia kuchota baraka, mheshimiwa vicky anawalipia ada ya sekondari watoto yatima, walemavu na wasiojiweza kimaisha, idadi yao ikifikia 75.

Kipato chake kikoje?

Dodoso zinaonesha kwamba, kwa kazi ya uheshimiwa, kwa mwezi anaingiza shilingi milioni 15 ukijumlisha posho zote za ubunge, ujumbe wa kamati ya bunge na mshahara.

Amfunika anne makinda uchunguzi uliofanywa na gazeti hili umebaini kuwa, jumba la kifahari la vicky kamata linalifunika lile la bosi wake ambaye ni spika wa bunge, mheshimiwa anne makinda. Yeye nyumba yake ipo kijitonyama.

Ulinzi nyumbani kwake usipime uwazi lilipata bahati ya kufika nyumbani kwa vicky na kukumbana na ulinzi wa mitambo ya kisasa ya kuzuia wezi na majambazi kwa saa 24. Ili mgeni aingie ndani ya geti huhojiwa na walinzi kwa dakika zisizopungua kumi.

Hi ndiyo ccm inayowatetea masikini na wakulima nawanyonge.

umesahau fanikio moja

bfriend wake ni nani??ungepata hili jibu usingekuja na haya yote ungejua yemtokea wapi!!
Fanya research utupe hili fanikio uliloliruka
 
- Kaka wacha majungu na siasa za makengeza sio nyie mliotuambia hapa kwamba utajiri wa Sugu ni halali maana alikuwa muimbaji wa muziki sasa hapa tofauti ni nini hasa ya hawa wanamuziki wawili kuwa na utajiri unaofanana? Sometimes mnakuwa na siasa za kuchekesha tulipouliza hapa kuhusu utajiri wa Sugu mlisema ni mwanamuziki sasa what is the problem hapa?

Le Mutuz

We mgogo sugu ana mgodi wa dhahabu? Acha izo bana
 
Bongo kuna tajiri? Hakuna hata mtu anayemiliki ndege yake binafsi hapa.basi tu tunazidiana katika matumizi ya vipato
 
ukiona hivyo ujue kuna multiple utilisation of herself na national cake nayo inaliwa vibaya.

bi kidude kaimba miaka mingapi, hajatoka!

how about this, VK? life is not so easy like that!

Lazima akaguliwe tu...
 
Serikali ya Tanzania imelala pamoja na tiss yake. Unapopata habari kama izi awe sugu awe nani ni lazima kufuatilia na kuzifanyia kazi hata kama Kamata anatembea na rais lakini ijulikane amepataje utajiri huo. Na kujua je hizi/hizo mali alizonazo ni zake na amezipataje. Kamata amekuwa afisa uhusiano wa bot na 2010 akawa mbunge, kwa mali inayozungumziwa ni karibu bilioni mbili. Jamani wadanganyika wapo waliokaa bungeni zaidi ya miaka 30 lakini hawana utajiri wa haraka kiasi hicho. Acheni maneno inatakiwa serikali ifanye kazi kutokana na habari ndio maana ya kuwa na waandishi wa habari. Huyo sijui Lemutuz hana lolote hawezi kusema kuwa mwacheni bila kufuatiliwa. Hivi wewe Lemutuz umeishi kweli Marekani au ulikuwa upo upo tu pale Marekani lakini ujui ulimwengu inakwendaje. Hapa ndipo ninapoilaumu tena serikali kutumia pesa za walalahoi kuwapeleka watoto wa wakubwa kusoma nje. Na kurudi kichwa ikiwa tupu kama huyu. Nilitegemea angekuwa mstari wa mbele kukemea na hata kutoa ushauri kumbe kichwa ni pumba kabisa

Simple, ameingia BOT mwaka 2006 na sasa ni mbunge,na ana mali inayozungumziwa ni karibu bilioni mbili. Jumla ya miaka aliyoka kwenye ajira ya maana ni miaka minane (BOT na Ubunge). Basi pato alilowekeza (acha kuhesabu alizoweka bank na anazotumia) alilipata kwa spidi ya kiwango cha Tshs 250 millioni kwa mwaka au Tshs laki 685 kwa siku au Tshs 29,000 kwa saa au Tshs 500 kwa dakika. Inatia moyo!!!
 
sawa sasa vile vile tuanze kumtathmini na JOYCE MUKYA vile vile naona siku hizi trip za Dubai kibao....
 
Back
Top Bottom