ChoiceVariable
JF-Expert Member
- May 23, 2017
- 82,063
- 87,976
Natoa wito Kwa serikali kuipandisha hadhi Manispaa ya Geita kuwa Jiji kwani Ina vigezo stahiki.
Ukiacha vigezo vya ujumla lakini Geita imekishi vigezo muhimu zaidi vya Mapato ya ndani ambapo Kwa mwaka wa fedha 2015/26 imefanikiwa kukusanya zaidi ya Bilioni 27.Mapato haya ni zaidi ya Majiji ya Mbeya & Tanga.
Aisha Manispaa ya Geita Kwa Sasa inakadiriwa kuwa na watu takribani Laki 5 ambao wanakidhi kupewa hadhi ya Jiji.
Mkuu wa Mkoa wa Geita Mhe. Martine Shigela ameipongeza Halmashauri ya Manispaa ya Geita kwa kufanikiwa kukusanya zaidi ya shilingi bilioni 27 katika mwaka wa fedha 2025/2026 sambamba na kuendelea kupata hati safi ya ukaguzi kutoka kwa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG).
Shigela ametoa pongezi hizo Juni 29, 2026 kwenye kikao maalumu cha Baraza la Madiwani Manispaa ya Geita cha kusikiliza na kujadili taarifa ya CAG kwa mwaka wa fedha 2024/2025 ambapo amesema mafanikio hayo yanaonesha nidhamu ya matumizi ya fedha za umma, uwazi katika usimamizi wa rasilimali pamoja na kuimarika kwa ukusanyaji wa mapato ya ndani.
Mkaguzi Mkuu wa nje wa Mkoa wa Geita ambae ni Mwakilishi wa Mdhibiti na mkaguzi Mkuu wa hesabu za serikali CAG Pastory Massawe amesema licha ya Halmashauri hiyo kupata hati safi ameitaka kuanza kujipanga kuelekea mwaka mwingine wa ukaguzi wa 2025/2026 ili kupunguza hoja za ukaguzi
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Manispaa ya Geita Yefred Myenzi amesema makusanyo ya zaidi ya shilingi bilioni 27 ni ongezeko la shilingi bilioni 13 ikilinganishwa na kipindi cha miaka miwili iliyopita nakwamba halmashauri hiyo itaendelea kubuni na kuimarisha vyanzo vipya vya mapato.
View: https://www.instagram.com/reel/DaPPGXIC2Jo/?igsh=MXdkb3VnbzdhbTFmdA==
My Take
Geita ni Mkoa wa 6 Kwa Uchumi Mkubwa Tanzania (GDP) so inakidhi vigezo vyote
Vigezo na Masharti viwe vinafuatwa badala ya mambo ya Kisiasa.