Ndio imeshapitishwa sasa!una uzee mwingi sana
Kweli kanzu na hata kuvaa kininja sioni. Labda vyote haviruhusiwi?Kanzu ipo upande gani?!
Kwa hiyo wewe ndo una mambo ya kizamani km mababu zetu siyo??nyie wote mnaopinga naombeni niwaulize kitu kimoja, mavazi/dressing code ina impact gani na perfomance ya mtu kimasomo? mbona mna mambo ya kizamani sana, tena sio kizamani maana hata zamani mababu zetu walikuwa wanajifunga tu vipande vya ngozi kujisitiri sehemu za siri na makalio, ingekuwa kuvaa kuna uhusiano na kufaulu basi hata havard au Yale wangekuwa na hizo mambo(nimesema tu hapo kwa assumption hawana hizi mambo) , nyie mnaosema eti oh watu wanatega wenzao kwa nguo wanazovaa nyie ni perverts na mna tamaa zenu za ajabu tu ! acha mtu avae anavotaka kama chuo hakumfai natural selection itaamua tu ndio maana kuna wanaodiscontinue...
Yani mwanaume haruhusiwi jinsi?anazingua, hii karne ya 21 na watu wanaosoma hapo wanajielewa, sasa ndio nini wanaume kukatazwa kuvaa jeans
Iliyokuwepo kabla ni ya watumishi wa umma ambayo imebandikwa kwenye kila chuo au office za umma.Mbona hii sera UDSM naiona toka Mwaka 2013, uje ulaumu leo. Na hiyo picha ipo karibu kika chuo
Na hizo dressing code zisizo na maadili wakienda majumbani kwao huwa hawazivai.
Halafu kuna wanaume wanawataka wavae ovyo lakini kwenye kuoa wanawakataa hao hao waliokuwa wanawahimiza na kuwasifia wanapendeza wakiwa wamevaa huo upupu.
Some people's mind need rehabilitation + services that cost billions of us dollars.
Mlokole gani anatumia makuwadi kumtafutia wanafunzi hao hao?
Inasemekana mke alimkimbia siku nyingi.
Hapo kwenye jeans wamekosea jeans ni vazi zuri sana kwa mwanachuo hasa wanaume, mimi nafikiri wangesema aina vani ya jeans inayofaa.
nachopigania ni kuwa hiyo sheria haina maana kwakuwa hakuna case yoyote iliyotokea mtu kavaa vibaya hapo chuo, hakuna asiyejielewa hapo chuoni wote ni watu wazima na pale wanaenda kupewa elimu kwahiyo mtu hawezi kuvaa kiajabu, ila wao kuweka hiyo sheria inaminya hadi nguo ambazo hazina impact, mwanaume kuvaa jeans au kaptula au kofia ina tatizo gani? mwanamke kuvaa jeans ina tatizo gani? usijitoe ufahamu mzee nenda na reality bora waache vitu vilivyo since hakuna harm yoyote iliyotokea hapo chuoni upande wa mavazi....
Inawezekana hujatembea vyuo vingi,hiyo sera ipo almost vyuo Vyote sasa sijui hao VC nao na ni Waalimu Ama la.
Naomba waongeze na Marufuku wanafunzi kuvaa earphones kila saa,vitu vingine ni ulimbukeni na ushamba tu Wala sio sense ya civilization.
Hawezi kutafuta decent dressing wakati yeye binafsi si mtu decent! See the connection my friend !Ila kuwa VICE kaaminiwa na kafanyiwa vetting. Hayo mengine ni kibinadamu zaidi, ana desires sawa na wengine
Yes lazima tuvae kwa heshima bro, kwani mtu akivaa nusu uchi we unapata faida gani na je mtu akivaa kistaarab unapata hasara gani.
Naunga hoja mkono kwa 100%. Maana ndio maadili ya Kiafrika na civilized nation.. dressing code inajenga pia disciplined generation and moral future leaders..
Mkuu sijui exposure yako kuhusu vyuo lakini nikutaarifu tu kwa TZ Hakuna chuo chenye foreigners wengi Kama Mweka college
Mkuu naomba nikujibu hoja zako kama ifuatavyo,hoja kwamba UDSM ndio chuo cha kimataifa pekee sio kweli,almost vyuo Vyote nchini Vina foreigners vingine kuzidi hata UDSM fanya study ktk vyuo vya Mweka na Jordan.
Hoja kwamba namna ya uvaaji haiathiri taaluma ni upofu wa kufikiri Sawa sawa, mvaaji anaweza asiathirike yeye lakini akaathiri wengine hasa jinsia tofauti.
Halafu kama msomi lazima utambue kwamba kila nchi ina utamaduni wake na katika ulimwengu wa kibepari kuna kitu kinaitwa cultural imperialism,hao wazungu unaowaona na kuwatetea wavae wanavyotaka means wanaeneza utamaduni wao.
Sisi tuna utamaduni wetu na ni lazima tuupiganie,anayetaka kuja Kusoma lazima afuate taratibu zetu hata wewe Ukienda Uarabuni lazima ufuate tamaduni zao za kujisitiri.
Kila Taifa na tamaduni zake,kama umefuata shule,lakini lazima ufuate Bye Laws za uendeshaji wa Chuo.
We jamaa usifananishe maumbo ya kibantu na ya wazungu jaribu kutumia akili japo kidogo.