Vibanda vilivyowekwa kando ya barabara Jijini Dar es Salaam kuondolewa

Kuna maamuzi wakati mwingine magumu lakini katika hili naunga mkono 100% na sio Dar tu iwe miji mingine yote mikubwa ni lazima tuanze sehemu na tuwe serious katika hili kuwe na muendelezo.
 
Kwa taarifa yako JPM kabla hajafariki ziara yake ya mwisho Dar alishaongelea hili kuwa kuna uganganyifu wenye maduka wanafunga ila bidhaa wanawapa watu kuuza nje na serikali wanapoteza pesa nyingi katika kodi za maduka. Hoja yako ya pile kuwe eti wawekezaji hawana limit sio kweli Mama kasema ziko taratibu za kuajiri lakini kuna key positions mwekezaji anahaki ya kuweka watu anaowaamini yeye na nafasi zingine ziende kwa mujibu wa taratibu. Na katika hili kusema hakuna ajira wakija wawekezaji sasa wasipokuja ajira zitatoka wapi? Majiji yote hawaruhusu vibanda hovyo mtaani waende soko lao la wamachinga mtu unashindwa hata kutembea barabarani.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…