Uwekezaji katika maeneo muhimu na ya kimkakati ya biashara yawe chini ya udhibiti wa Serikali. Ya Kariakoo yanaweza kujirudia kwingineko.

KARLO MWILAPWA

JF-Expert Member
Apr 10, 2019
2,590
4,603
Nianze kwa kusema kwamba kama Serikali ingekuwa na umiliki wa moja kwa moja wa eneo la Kariakoo ,hakika tusishuhudia mgomo wenye kuumiza walaji kama inavyoshuhudiwa.

Huu ndio ushauri wangu kwa serikali yangu sikivu, sekta binafsi zinasaidia kwa kiasi kusaidia kukua kwa uchumi lakini sekta binafsi haziwezi kufanya Taifa liwe na uchumi huru kwa sababu ya kukosa uwezo wa kufanya maamuzi.

Hapa nitajikita kwenye tatizo lililotokea karibuni la mgomo wa wafanyabiashara Kariakoo. Bila kujua athari za moja kwa moja za mgomo wao kwenye uchumi wakatekeleza walichofanya,na sipo kuwalaumu kwa wasichofanya na nalaumu matokeo ya kiichofanyika kwamba walaji wameumizwa kwa kiwango kikubwa.

Moja ya Majukumu ya Serikali ni kulinda maslahi ya walaji iwe wa bidhaa au huduma na walaji hao ni wanachi. Ndio maana ikitokea changamoto inayohusu walaji na wazalishaji ,serikali inaingilia kati na lengo ni kumsaidia mlaji.

Kwa mtazamo wangu, Serikali inatakiwa kuwa na udhibiti wa moja kwa moja wa maeneo yote ya kimkakati ya kibiashara na uwekezaji ili kulinda walaji kutaabishwa.

Udhibiti huo uwe kwa namna gani? Katika miji inayopangwa na viwanja vinavyotolewa maeneo yanayotengwa kwa ajili ya biashara, uwekezaji au viwanda yawe chini ya Serikali. Na yeyote anayetaka eneo katika maeneo hayo awe kama anaazimishwa na Serikali na sio kupewa umiliki. Uwekezaji wowote utakaofanywa na aliyeomba maeneo kwenye maeneo uwe ni uwekezaji unaoweza kudhibitiwa na Serikali moja kwa moja yaani ni kusema kwamba aliyepo hapo ni mpangaji tu. Na huu ndio udhibiti ninaoushauri uwe nayo.

Hata sasa bado Serikali haijachelewa juu ya udhibiti katika maeneo ya kimkakati ya uwekezaji, biashara na viwanda. Hii itasaidia serikali kuwa na uwezo wa kudhibiti mfumuko wa Bei, migomo na Hali ya biashara na uwekezaji bila nguvu kubwa.
 
Ushavuta ugoro sasa unapiga chafya tu, Kwahiyo kwa akili zako serikali imiliki nyumba zote za kariakoo?
 
Ushavuta ugoro sasa unapiga chafya tu, Kwahiyo kwa akili zako serikali imiliki nyumba zote za kariakoo?
Soma taratibu la sivyo wewe ni mnufaika wa mgomo wenye kutuumiza walaji. Udhibiti ninaosema hapa ni kuwa na umiliki wa maeneo ya kimkakati ya biashara na uwekezaji, yeyote atakayetaka kufanya biashara kwa sharti la kuweka jengo lake eneo hili huyo mtu anakuwa ni kama mpangaji na Serikali ndio mmiliki. Jengo linakuwa lako lakini serikali ndio inapanga mipango yote na namna ya uendeshaji wa maeneo hayo. Ni hayo tu
 
Unaelewa maana ya kodi ya Ardhi? halafu utashangaa mtu kama huyu eti naye ana degree.

Watu wa aina yako ndio mkipewa Madaraka mnaleta maamuzi ya kipuuzi kabisa kwa uwezo wenu Mdogo wa kuchanganuwa mambo.
 
Pengine huelewi kwa sababu ya ugumu wa kutokuelewa au umegoma kuelewa. Basi niseme hivi ili uelewe vizuri 'maeneo yaliyopangwa kama ya biashara yasigawiwe na badala yake yawe ni ya Serikali na uwekezaji wowote utakaofanyika ndani yake utatambulika kama ni wa serikali" Sheria sio Msahafu au Biblia
 
Hata sasa bado Serikali haijachelewa juu ya udhibiti katika maeneo ya kimkakati ya uwekezaji, biashara na viwanda. Hii itasaidia serikali kuwa na uwezo wa kudhibiti mfumuko wa Bei, migomo na Hali ya biashara na uwekezaji bila nguvu kubwa.
... ungemalizia vizuri - hata "wenzetu" China wanafanya hivyo. Finally, weka na namba ya simu kurahisisha mawasiliano.
 
Pengine huelewi kwa sababu ya ugumu wa kutokuelewa au umegoma kuelewa. Basi niseme hivi ili uelewe vizuri 'maeneo yaliyopangwa kama ya biashara yasigawiwe na badala yake yawe ni ya Serikali na uwekezaji wowote utakaofanyika ndani yake utatambulika kama ni wa serikali" Sheria sio Msahafu au Biblia
Huna akili.
 
Attachments

  • FB_IMG_1684239908004.jpg
    FB_IMG_1684239908004.jpg
    45 KB · Views: 1
Back
Top Bottom