Bavaria
JF-Expert Member
- Jun 14, 2011
- 53,109
- 53,631
Habari za wakati huu..?
Katika maisha yetu ya kiafrika tumelelewa kuwa wasiri haswa katika mambo ya mahusiano..yani hata kama jambo linaumiza wewe litunze moyoni kuna siku mambo yatakuwa sawa,..
..kwa upande mwingine kumekuwa na utamaduni mpya wa wapenzi/wanandoa kupenda kuanika/expose mambo yao hadharani yaani hata kama ni pungufu mdogo tu mtu anauanika hadharani bila ya kujali..
...karibuni tujadili ni kipi ambacho chaweza kusitiri mahusiano kwa muda mrefu kati ya usiri na uwazi/kuanika matatizo hadharani,
..ni nini faida za kuwa na siri katika ndoa/mahusiano..
Na nini faida za kuwa na uwazi katika mahusiano..hasa wa kwa watu wa nje ya yale mahusiano,
karibuni ladydoctor, Excel, The Boss, passionlady watu8 Eiyer, Karucee, picha toka kwa Tyta, Bulldog Munkari King'asti HARUFU Kongosho Tuko kokutuna,. Na wanaMMU woote...
Dada Jawilat goja nichangie kwa mfano wa moja ya mahusiano yangu nlowahi kuwa nayo.
Back in the college, i had a girl, i loved her from the first sight (They say there is no love at the first sight but am a believer of the theory), The girl we dated from first year day one up to the last semester of the third year. We broke up because she was older to me and she was in hurry for a marriage.
Maisha yetu yalikuwa ya kugombana sana kwasababu kila mmoja alitaka kuwa juu ya mwenzake, kuna vitu alikuwa akitaka mimi sitaki na viceversa, haipiti siku bila kupishana maneno au mmoja akamuuzi mwenzie ila before we go to bed we must meet and say sorry for eachother. Na Nilichompendea sana huyu girl alikuwa hamuambii mtu yeyote matatizo yetu, hata dada yake ambae alikuwa ndo best friend wake. Nilikuja kugundua hilo wakati nikikutana na marafiki zake, wananisifia nimekuwa mpole na kumthamini rafiki yao. Kumbe deep inside our relationship was in trouble.
Hadi mwaka wa tatu mambo yalipoanza kunizidia niliamua kumuelezea dada ake ambaye alishangaa sana kwanini tumekaa kipindi chote tunagombana na hatusemi. Hapo ndo huyo girl akasema sio kila mtu anatakiwa kujua what we are doing because its none of their business, alikasirika sana nilivyomwambia dada ake.
Bahati mabaya yule msichana tuliachana nae kwa wema (alikuwa mkubwa kwangu na ilikuwa ngumu kuweka our differences pembeni) na hajawahi kumwambia mtu yeyote kuwa tumeachana na hata marafiki zake waliogundua kuwa tumeachana hajawahi kuwapa sababu. Na most of people walokuwa wanaifahamu couple yetu wananisema vibaya kuwa nimemwacha mtoto wa watu lakini ukweli ni kwamba hakuna anaejua ukweli kwanini tumeachana na exactly lini tumeachana. Sasa hivi yupo tu na ofisi yake bahati mbaya hajaolewa ila nahisi mwaka huu ataolewa tu. And i really thank her for showing me how to handle relationships privately.
Inshort, sio kila mtu anatakiwa ajue kuhusu mahusiano yenu, iwe furaha, iwe huzuni. Kuwa na marafiki inaruhusiwa na unaweza kuwaambia zile ishu ambazo zipo too general na sio personal stuffs. Marafiki wakishajua weakness kuhusu nyie inakuwa rahisi sana kuwatenganisha au kuwaumiza.
Be careful with friends, not everyone is worthy to be one.