Uwazi na usiri katika mahusiano kipi chafaa...?!

Mambo ya wazi VS siri yanatofautiana sana kati ya mtu na mtu, jamii na jamii, tamaduni na tamaduni.

So ni kufanya kile ambacho akili yako inaruhusu.
kuna jamii yoyote ya kiafrika inayoruhusu mambo ya ndoa kuanikwa anikwa hadharani?

naomba ufafanuzi mwenyekiti.
 
Kwangu mimi sioni sababu ya kuwa muwazi hadi nje kwa mambo ya mahusiano. Mahusiano ni kati ya watu wawili waloamua kushare maisha yao. Ni vizuri kuwa muwazi kwa mwenza wako lakin sidhani kama kuna umuhimu wa third party kujua kila kitu ktk mahusiano yenu. Kutunziana siri ni moja ya heshima ya wanamahusiano. Kama mmoja anatoa mambo nje hapo hakutakuwa na heshima. So kuwa muwazi ni vizuri lakini kwa mwenza wako tu siyo kwa watu wengine.
 
Kabisa Husninyo,mie nikikaa na kumueleza Excel mapungufu ya mpenzi Tuko,inakuwa rahisi sana Excel kutengeneza mazingira ya kuchepuka na mimi..
ila kwa hili sister jawilat n Husninyo,

kuna varification kutoka kwa mwanaume mmoja kwenda mwingine, sidhani kama wote watakuwa na interest za kuchepuka na bidada kisa tu yuko kwenye recession kwenye ndoa yake..

wapo wanaume wenye mawazo ujenzi kabisa ambayo hunusuru ndoa/mahusiano ya waliohusiana!

tusizamishe jahazi lote jamani..!
 
Last edited by a moderator:
Kuwa wawazi kwa nyinyi wawili ni jambo la kheri ila sasa kuwa wazi kwa hao wa nje ndo kuna matatizo hapo,
hivi unadhani ni kwanini wengi wa walio nje wanatumia advantage ya wapenzi walio kwenye matatizo kama chambo cha kuwagegeda?

ukiangalia wengi wa washauri wanaopewa/kuambiwa matatizo ya wapenzi huwa wana viwango vidogo sana kielimu, ama wengi wao huwa hawana elimu kabisa..

chunguza hili jawilat... mtu mwenye elimu yake nzuri, hawezi tumia mwanya wa matatizo ya mwenzie kupata haramu!

cc. Husninyo.
 
Last edited by a moderator:
point...

starehe nyingi za wanawake ni kusema mambo yao ya siri, hata kwa watu wasiowajua kiundani, ilimradi tu mmefahamiana within three minutes.!

hapo tu ndipo mnapomegwa mpaka na waganga wa kienyeji.

dogo uwe na heshma kidogo. swala la kuongea mambo ya ndani nahs ni la wanaume pia haswa wanapotaka waonewe huruma.
 
Ebu chukulia mkeo anarudi nyumbani amelewa anarudi usiku wa manane eeh..umemkalisha chini mmeongea ila kila siku anarudia eeh...utafanya siri ama utaomba msaada kwa watu wa nje?
Kwangu mimi sioni sababu ya kuwa muwazi hadi nje kwa mambo ya mahusiano. Mahusiano ni kati ya watu wawili waloamua kushare maisha yao. Ni vizuri kuwa muwazi kwa mwenza wako lakin sidhani kama kuna umuhimu wa third party kujua kila kitu ktk mahusiano yenu. Kutunziana siri ni moja ya heshima ya wanamahusiano. Kama mmoja anatoa mambo nje hapo hakutakuwa na heshima. So kuwa muwazi ni vizuri lakini kwa mwenza wako tu siyo kwa watu wengine.
 
Excel tabia ya mtu kula haramu haiwezi kubadilishwa na kiwango cha elimu ya mtu,
hivi unadhani ni kwanini wengi wa walio nje wanatumia advantage ya wapenzi walio kwenye matatizo kama chambo cha kuwagegeda?

ukiangalia wengi wa washauri wanaopewa/kuambiwa matatizo ya wapenzi huwa wana viwango vidogo sana kielimu, ama wengi wao huwa hawana elimu kabisa..

chunguza hili jawilat... mtu mwenye elimu yake nzuri, hawezi tumia mwanya wa matatizo ya mwenzie kupata haramu!

cc. Husninyo.
 
Last edited by a moderator:
ila kwa hili sister jawilat n Husninyo,

kuna varification kutoka kwa mwanaume mmoja kwenda mwingine, sidhani kama wote watakuwa na interest za kuchepuka na bidada kisa tu yuko kwenye recession kwenye ndoa yake..

wapo wanaume wenye mawazo ujenzi kabisa ambayo hunusuru ndoa/mahusiano ya waliohusiana!

tusizamishe jahazi lote jamani..!

hatusemi wote na ndio maana tukasema tuangalie na watu tunaowaeleza mambo yetu ya ndani. ndio maana wengi huelezea shida zao jf maana hakuna anaemjua.
 
Last edited by a moderator:
halafu ujue swala la kutoa siri hata kama upo single sio vizuri kuongea ongea matatzo yako
hapa Husninyo naomba niende kinyume na matakwa yako,

vijana wengi hasa wa jamii za kiafrika hushindwa kufanya maamuzi sahihi katika umri waliopo.. katika umri wa ujana, si vyema kuwa na siri nyingi moyoni...

mfano halisi ni hawa vijana wetu wengi wanapokuwa wamefeli katika masomo yao.. wengi huwa wanajinyonga kimya kimya tu kutokana na kuwa na siri mioyoni mwao!!..

hapo naomba niende kando na wewe kidogo-- lete hoja!

cc. Jawilat.
 
Last edited by a moderator:
kuua mtu dhambi kwa Mungu.
kumfanya bubu huwezi.
vumilia mkuu.
mimi hata nafsi yangu siiamini kiviiiiile
umepotea sana lakini besti... niambie bana, usifanye siri! lol.

si unajua tena mficha uchi hazai?
 
Hapo sawa na jf uzuri unakutana na majibu tafauti na ulivyotarajia..kwa hivyo hata uwanja wa kufikiri na kutoa maamuzi unapanuka..
hatusemi wote na ndio maana tukasema tuangalie na watu tunaowaeleza mambo yetu ya ndani. ndio maana wengi huelezea shida zao jf maana hakuna anaemjua.
 
hatusemi wote na ndio maana tukasema tuangalie na watu tunaowaeleza mambo yetu ya ndani. ndio maana wengi huelezea shida zao jf maana hakuna anaemjua.
ni kweli husninyo? hebu niambie, umeolewa ninyo?

jibu ni jibu, nasubiri kwa hamu hapa! lol.
 
Ebu chukulia mkeo anarudi nyumbani amelewa anarudi usiku wa manane eeh..umemkalisha chini mmeongea ila kila siku anarudia eeh...utafanya siri ama utaomba msaada kwa watu wa nje?
Swala la kukamatwa na pombe siyo la siri tena maana ni wangapi watakuwa wanamuona huko kwenye pombe. Pia kama amekuwa addicted na pombe na hataki kusikia ushauri wangu kama mwenza wake, namkalisha na wazazi wake, ikishindikana namchukua jawilat.lol. Anyway nikishndwa na wazazi wake atakuwa mzigo wangu ila michepuko itaanza.
 
Sasa Excel hayo ni mambo ambayo ukiangalia kuyaendesha mwenyewe inakuwa vigumu..lakini pia katika kutoa siri yale unayoona yatakuathiri kuyaweka wazi unayaacha tu moyoni,
hapa Husninyo naomba niende kinyume na matakwa yako,

vijana wengi hasa wa jamii za kiafrika hushindwa kufanya maamuzi sahihi katika umri waliopo.. katika umri wa ujana, si vyema kuwa na siri nyingi moyoni...

mfano halisi ni hawa vijana wetu wengi wanapokuwa wamefeli katika masomo yao.. wengi huwa wanajinyonga kimya kimya tu kutokana na kuwa na siri mioyoni mwao!!..

hapo naomba niende kando na wewe kidogo-- lete hoja!

cc. Jawilat.
 
Last edited by a moderator:
Excel tabia ya mtu kula haramu haiwezi kubadilishwa na kiwango cha elimu ya mtu,
hmm!

hivi ulishawahi kujiuliza jawilat, kwamba mtu yeyote tu mwenye elimu na uelewa wake, kwamba mtendwa atamweleje hasa pale tatizo litakapokuja kuwa solved? wataangalianaje kweli?

mfano wewe umeleta tatizo lako la chumbani kwangu kutoka kwa Tuko! bahati nzuri nikafanikiwa kukurestisha kwa mgegedo, unadhani tutaangalianaje pale majanga yakishaisha?!

kitanuka kimya kimya!
 
Last edited by a moderator:
hapa Husninyo naomba niende kinyume na matakwa yako,

vijana wengi hasa wa jamii za kiafrika hushindwa kufanya maamuzi sahihi katika umri waliopo.. katika umri wa ujana, si vyema kuwa na siri nyingi moyoni...

mfano halisi ni hawa vijana wetu wengi wanapokuwa wamefeli katika masomo yao.. wengi huwa wanajinyonga kimya kimya tu kutokana na kuwa na siri mioyoni mwao!!..

hapo naomba niende kando na wewe kidogo-- lete hoja!

cc. Jawilat.

nina mfano hai, kuna dada tulikuwa tunasoma nae alikuwa anapenda sana kuelezea mambo yake binafs ya kimaisha na changamoto ya kutokuwa na kazi. kuna mzee mambo safi akamtokea, kutumia shida za mwenzie kwa gia za kumsaidia. mzee kapewa cha mbavu, nikatonywa kuwa mzee alikuwa na lengo la kumsaidia bidada shida zake. ila yote hiyo ni sabb ya kujielezea elezea kwa watu.
 
Last edited by a moderator:
Sasa Excel hayo ni mambo ambayo ukiangalia kuyaendesha mwenyewe inakuwa vigumu..lakini pia katika kutoa siri yale unayoona yatakuathiri kuyaweka wazi unayaacha tu moyoni,
hivi ulipitia story moja hivi ya mke na mumewe ambaye jamaa alipata kimada nje akataka kumuacha mkewe baadae mkewe kutokana na ukimya wake na kutunza siri za ndani akaja kufa kwa kansa?

hadithi ile ilinifundisha mengi sana... siri zina mahali pake, uwazi pia!
 
nina mfano hai, kuna dada tulikuwa tunasoma nae alikuwa anapenda sana kuelezea mambo yake binafs ya kimaisha na changamoto ya kutokuwa na kazi. kuna mzee mambo safi akamtokea, kutumia shida za mwenzie kwa gia za kumsaidia. mzee kapewa cha mbavu, nikatonywa kuwa mzee alikuwa na lengo la kumsaidia bidada shida zake. ila yote hiyo ni sabb ya kujielezea elezea kwa watu.
kwa hiyo unataka kuhitimishaje?!
 
Hapo sawa na jf uzuri unakutana na majibu tafauti na ulivyotarajia..kwa hivyo hata uwanja wa kufikiri na kutoa maamuzi unapanuka..

kabisa.. ingawa wapo watakaodai picha. babu Dark City mkongwe wa ndoa akuje hapa.
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom