Uwazi na usiri katika mahusiano kipi chafaa...?!

Na mara nyingi muafaka huwa ni kati ya "achana naye maisha yataenda tu"au "mvumilie ndo maisha"..hapo kwenye achana nae huwa pana wepesi wa kutimia kwa baadhi ya wanandoa na kuna ndoa zinavunjika kutokana na kuyasema matatizo yao kwa watu wengine..
Mdogo wangu Husninyo, ukongwe sina kwa sababu kila siku inayopita ni shule tosha....

Hata hivyo, mleta mada katuchanganya...kaongea uwazi kati ya wanandoa, na kaumiz na uwazi wa kueleza mambo ya nadani kwa watu wa nje.

Naamini uwazi katika ndoa ni jambo muhimu sana (ingawa si kwa watu wote, kwa hiyo watu wawe mbayu wayu), hata hivyo siamini katika kueleza mambo ya ndani kwa watu wa nje. Labda kama imefikia mahali ambapo hakuna jinsi bali kutafuta mwafaka kwa kushirikisha watu wa nje.

Vinginevyo ni aibu kuonge onge hovyo mambo ya ndani!!
 
Last edited by a moderator:
Ndo maana nikasema wenye msaada! Sasa yeye akisambaza ni juu yake coz mi ntakuwa nimesolve tatizo langu . Obvious mpk nikushirikishe tatizo langu ninakuamini sana zaid ya sana!
 
Hapo inabidi upime upepo kwamba je hili nikiweka wazi nawezapata suluhu ama ntaangukia pua? % kubwa ya kuwa muwaz ni kwamba unapunguza mzigo moyon mwako na pengine kupata suluhu mrad uangalie na aina yawatu katika kuelezea mambo yako
 
Shosti unakuja unaniambia mzigo wa ndoa yako..ushauri wangu kwako twende nikupeleke kwa mganga tukamtie kwenye chupa,eeh hapo umeniamini na kuona ni mtu wa karibu,kwa stress na kuchoswa na matatizo unaungana na mie haoo tunaenda kwa mganga..kesho kutwa mumeo anakuwa zezeta ni nani wa kulaumiwa hapo?

Nilitarajia uwe unajua ni kipi cha kusema hadharani na kipi sio cha kusema

Lakini pamoja na kuanzisha huu uzi bado sijajua kama unajua au hujui au unataka tujadili ili wengine wajue ni yapi ya kusemwa na yapi sio ya kusemwa

Lakini pia kitendo cha kusema hapa yale ambayo yanatakiwa yasemwe na yapi yasisemwe tutakuwa tumeharibu tayari

Yale ya kusemwa nje sawa lakini yale ambayo hayatakiwi kusemwa nje tukiyasema hapa tutakuwa tayari tumeharibu

Ila sidhani kama mambo haya yana kanuni inayofanana ila kuna mengi wengi wanaweza kukubali kuwa haya sio ya kusema lakini siyo yote!
 
Kiufupi ni hivi Eiyer yale mambo yanayotesa ndani ya ndoa/mahusiano yanafaida zozote kuyaweka wazi?inaweza ikasaidia ndoa/mahusiano kudumu?...

hayo wanayaweza wazungu. maana kichepuka anarudi kwq mwenzi wake na kusema. Jana I had sex. but only sex. I love you. na Mwenzi wake anamkumbatia na kumpa pole. je nyie njemba za kiafrika mnaweza hapo? alamsiki
 
Unamaanisha nini unaposema yanayotesa?

Nashindwa kujua cha kuchangia kwasababu hujawa specific!
 
Haha hapo utakua unatafuta kuwa chongo,
hayo wanayaweza wazungu. maana kichepuka anarudi kwq mwenzi wake na kusema. Jana I had sex. but only sex. I love you. na Mwenzi wake anamkumbatia na kumpa pole. je nyie njemba za kiafrika mnaweza hapo? alamsiki
 
umepotea sana lakini besti... niambie bana, usifanye siri! lol.

si unajua tena mficha uchi hazai?

I live like a nocturnal bird at flight,
That leaves its nest,
At dawn, diligently working hard,
Searching for its daily bread.

On my return journey at night,
Like tigers at the carcass, for buses we fight,
Avoiding to arrive home late hours,
Lest our honeys become furious at us.

I arrive home at mid-night, tired,
Only to find my honey, like a little bird,
In bed enjoying fantastic adventures,
In the world of hopes and dreams.

I'll tell you more,
Meanwhile there is a foe,
Who needs my full attention,
For his total elimination.
 
Shosti unakuja unaniambia mzigo wa ndoa yako..ushauri wangu kwako twende nikupeleke kwa mganga tukamtie kwenye chupa,eeh hapo umeniamini na kuona ni mtu wa karibu,kwa stress na kuchoswa na matatizo unaungana na mie haoo tunaenda kwa mganga..kesho kutwa mumeo anakuwa zezeta ni nani wa kulaumiwa hapo?

Mwee hapo majanga sasa,ndomana nivema kua makini nawatu. Ila uwaz unasaidia bana
 
nimekusoma mzee. halafu siku hizi nimekuwa mdogo wako sio mjukuu??!!! mbona unaniongezea distance hivo? loh.

Kumbe wewe bado mtoto......Kwa wajukuu, Babu huwa ana majina mengi sana...hata kumwita mjukuu mchumba ni kawaida tu!

Na mara nyingi muafaka huwa ni kati ya "achana naye maisha yataenda tu"au "mvumilie ndo maisha"..hapo kwenye achana nae huwa pana wepesi wa kutimia kwa baadhi ya wanandoa na kuna ndoa zinavunjika kutokana na kuyasema matatizo yao kwa watu wengine..

Binafsi naamini mambo ya ndani yanazungumzwa ndani. Ni pale tu unaposhindwa kukubaliana mnapohitaji wasuluhishi. Kuongea ongea eti kupunguza stree nikuzalisha matatizo mengine!

Nilitarajia uwe unajua ni kipi cha kusema hadharani na kipi sio cha kusema

Lakini pamoja na kuanzisha huu uzi bado sijajua kama unajua au hujui au unataka tujadili ili wengine wajue ni yapi ya kusemwa na yapi sio ya kusemwa

Lakini pia kitendo cha kusema hapa yale ambayo yanatakiwa yasemwe na yapi yasisemwe tutakuwa tumeharibu tayari

Yale ya kusemwa nje sawa lakini yale ambayo hayatakiwi kusemwa nje tukiyasema hapa tutakuwa tayari tumeharibu

Ila sidhani kama mambo haya yana kanuni inayofanana ila kuna mengi wengi wanaweza kukubali kuwa haya sio ya kusema lakini siyo yote!

Toka mwanzo nilisema kuwa hii mada imchanganya maembe na malimao...kuna mjadala wa uwazi katika ndoa. Hili naliunga mkono kwa nguvu zangu zote. Ila kuna huu mjadala mwingine ambao naona kama una utoto fulani, wa kuongea matatizo ya ndoa kwa watu wa nje. Kama ulivyosema, huo hauna tija hata kidogo kwani mwisho wake ni matatizo zaidi!
 
Dark City, shkamoo kaka.
hebu lala unategea zamu kwa bibi. Ama ndo unakula kodi zetu kwenye spring?

Hahahahahahah,

Na wewe ilikuwa unafanya nini saa hizi? Mbona ule muda wa mambo yako unayoyatukuza sana ulikuwa bado??

Mie na Bibi tulikuwa kwenye mkesha bwana!!
 
Toka mwanzo nilisema kuwa hii mada imchanganya maembe na malimao...kuna mjadala wa uwazi katika ndoa. Hili naliunga mkono kwa nguvu zangu zote. Ila kuna huu mjadala mwingine ambao naona kama una utoto fulani, wa kuongea matatizo ya ndoa kwa watu wa nje. Kama ulivyosema, huo hauna tija hata kidogo kwani mwisho wake ni matatizo zaidi!
Mkuu hapo kwenye huo uwazi ndipo kwenye shida

Mtoa mada nadhani hajui mpaka wa huo "uwazi"
Yaani hata pnapoanzia na kuishia huo uwazi hajui

Angejua asingeanzisha huu uzi

Ndoa inahitaji ue umepevuka kifikra bila hivyo kesho tu unarudi nyumbani au utakuja hapa JF kulaumu wanando wote duniani kumbe tatizo ni lako!
 
Nadhani hayo ndiyo yanayowasumbua vijana wetu. Wanataka kuingiza mambo ya ndoa kwenye chats zao za whasap.

Ndiyo maana wengine hawakai kuona 1st aniversary ya ndoa zao!

Wengine tunanusa nusa Golden Jubilee!
 
Mkuu hii ni khatari sana

Ngoja tuone tutakapoishia!
 
Back
Top Bottom