Uwazi na usiri katika mahusiano kipi chafaa...?!

Uwazi na usiri katika mahusiano kipi chafaa...?!

Kwanini Umfiche Mwenzio kwa jambo ambalo lina mustakabali kwenye mahusiano yenu?
Huo usiri ndo chanzo cha maumivu
 
Daudi1 hauoni kwamba kusema mambo yanayokuumiza katika ndoa inaweza kusaidia kupunguza moto wa uchungu kifuani na pengine kupata suluhisho kutoka kwa wale unaowaambia?
Unawaambia wangapi? kuna watu umepewa wa kuwaambia yanayokusibu wa kwanza kabisa ni wasimamizi wa ndoa yako hao wanabeba nafasi ya ulezi wa ndoa,wazazi na hata aliyewafungisha hiyo ndoa kama ni mchungaji padri au shehe hao ndo wenye ruhusa ya kujua maswahibu yanayokukumba lakini pia si yote wote wanastaili kujua ni baadhi ya mambo ambayo unaona hauwezi kuyatatua unahitaji msaada mengine unaweza kuyamaliza mwenyewe kwa kuongea na muhusika.

Sasa kuna wengine hata madogo tu basi majirani watajua hata kama hela ya matumizi anatoa mwanamke basi utasikia mpaka mtaa wa pili sasa lile suala la umoja linakuwa wapi,wengine mmekosana kidogo tu huyo anaenda kutangaza kila mtu na staili yake wengine wanakimbilia huku yote ni kkusema je huko kunapunguza tatizo au kunaongeza mwisho mtakuja kuijkuta mnazozana kwenye sosho media kila mtu akitumia Id fake,kama unampenda utamtunzia siri,kuna wanawake wengine mpaka unaweza ukajiuliza huyu niliumbiwa mimi au nimempora wa mwenzangu
 
Kwa mtazamo wangu nasema Usiri unafaa sana na Usiri ndio utaoleta stara ndani ya uhusiano/ndoa, na hata kwa marafiki wa karibu au hata rafiki mmoja wa karibu sana ambaye wewe unamwamini kukutunzia siri hapaswi kuyafahamu yenu ya ndani, maana unaweza sema rafiki yangu namwamini atanitunzia siri - huyo huyo uliyemwamini akafichua siri kwa mmoja mwingine anaemwamini kinachofuata hapo siri hakuna tena sababu kwa hulka za kibinaadamu ipo siku na yeye atayatoa nje. Vizuri kusuluhisha tofauti zenu au kuyamaliza yenu ya ndani ninyi wawili bila ya kuhusisha maswala yenu kwa watu wa nje.

Wanaposema ndoa ni pamoja na kuvumiliana hawajakosea, sababu hata kutunziana siri zenu za ndani ni moja ya uvumiliano.

Labda tofauti zitakapokuwa kubwa sana kiasi cha kutaka kuweka ndoa yenu hatarini ni bora kuwashirikisha wazee,wazazi au watu wazima wenye busara zao.
 
:behindsofa:sitaki ugomvi mie

bila shaka hawa ni wakazi wa mwambao.. wazaramo, wakwere, wandengereko, wasambaa nk!

jamii hizi hazina siri kulingana na tamaduni zao za kila siku. upo kongosho?

I stand to be corrected.
 
Back
Top Bottom