Uwazi na usiri katika mahusiano kipi chafaa...?!

Uwazi na usiri katika mahusiano kipi chafaa...?!

Usiusemee moyo wa mtu...
hmm!

hivi ulishawahi kujiuliza jawilat, kwamba mtu yeyote tu mwenye elimu na uelewa wake, kwamba mtendwa atamweleje hasa pale tatizo litakapokuja kuwa solved? wataangalianaje kweli?

mfano wewe umeleta tatizo lako la chumbani kwangu kutoka kwa Tuko! bahati nzuri nikafanikiwa kukurestisha kwa mgegedo, unadhani tutaangalianaje pale majanga yakishaisha?!

kitanuka kimya kimya!
 
Last edited by a moderator:
Sasa kuchepuka niyo suluhu ya matatizo yenu?na vipi mchepuko nao ukiwa na matatizo yake utauanika wazi ama unatafuta mchepuko mwingine?
Swala la kukamatwa na pombe siyo la siri tena maana ni wangapi watakuwa wanamuona huko kwenye pombe. Pia kama amekuwa addicted na pombe na hataki kusikia ushauri wangu kama mwenza wake, namkalisha na wazazi wake, ikishindikana namchukua jawilat.lol. Anyway nikishndwa na wazazi wake atakuwa mzigo wangu ila michepuko itaanza.
 
Nilipitia Excel hata sasa kuna watu wanakufa kwa msongo wa mawazo kwa kutunza mambo mazito na ya kuumiza..
hivi ulipitia story moja hivi ya mke na mumewe ambaye jamaa alipata kimada nje akataka kumuacha mkewe baadae mkewe kutokana na ukimya wake na kutunza siri za ndani akaja kufa kwa kansa?

hadithi ile ilinifundisha mengi sana... siri zina mahali pake, uwazi pia!
 
Last edited by a moderator:
Weeee, kuna jamii zina slogan 'usininyime neno...'

Hadi wanamme wao vifua panzi, hawawezi kukaa na neno utadhani wamelisha radio.

kuna jamii yoyote ya kiafrika inayoruhusu mambo ya ndoa kuanikwa anikwa hadharani?

naomba ufafanuzi mwenyekiti.
 
Last edited by a moderator:
Weeee, kuna jamii zina slogan 'usininyime neno...'

Hadi wanamme wao vifua panzi, hawawezi kukaa na neno utadhani wamelisha radio.

bila shaka hawa ni wakazi wa mwambao.. wazaramo, wakwere, wandengereko, wasambaa nk!

jamii hizi hazina siri kulingana na tamaduni zao za kila siku. upo kongosho?

I stand to be corrected.
 
Excel mie simo..
bila shaka hawa ni wakazi wa mwambao.. wazaramo, wakwere, wandengereko, wasambaa nk!

jamii hizi hazina siri kulingana na tamaduni zao za kila siku. upo kongosho?

I stand to be corrected.
 
Last edited by a moderator:
Nilipitia Excel hata sasa kuna watu wanakufa kwa msongo wa mawazo kwa kutunza mambo mazito na ya kuumiza..
unajua jawilat, kuna vitu vya kuweka siri endapo mtaongea wawili ndani mkaelewana, lakini endapo mmoja wenu ataonekana ni kichwa jiwe, hataki kupondeka kwa kumsikiliza mmwenzie, unadhani dawa yake itakuwa ni ipi?

simaanishi kwamba hii iwe ni public announcement!
 
Sasa kuchepuka niyo suluhu ya matatizo yenu?na vipi mchepuko nao ukiwa na matatizo yake utauanika wazi ama unatafuta mchepuko mwingine?

Sasa Jawilat kama yeye anaanza kunizingua kwa kuuninyima haki yangu, si natafuta kwingine?? pia nimekuambia kuchepuka kutafuata hasa baada ya mipango ya kumrudisha katika hali ya kawaida kushindikana.
 
Haha Kongosho wa wapi hao?

kuna mmoja nilipanda nae bus wakat nasafiri, hadi tunashuka nilikuwa nishajua ana watoto wangapi, mwngne wa nje ya ndoa.. mke aliemuoa hakuwa chaguo lake, (madai hakutaka kuoa ngozi nyeusi)... .. kazi anayofanya na mpaka mahusiano yake ya nyuma bila kusahau namba za simu alinipatia. usishangae wapo wengi tu.
 
Last edited by a moderator:
Husninyo huyo nshakutana naye..mpaka idadi ya mabao anayopiga kwa mkewe anasimulia..anajisifia kabisa mpaka michepuko inavyomkatia mauno..nikasema huyu sio mzima wallah!
kuna mmoja nilipanda nae bus wakat nasafiri, hadi tunashuka nilikuwa nishajua ana watoto wangapi, mwngne wa nje ya ndoa.. mke aliemuoa hakuwa chaguo lake, (madai hakutaka kuoa ngozi nyeusi)... .. kazi anayofanya na mpaka mahusiano yake ya nyuma bila kusahau namba za simu alinipatia. usishangae wapo wengi tu.
 
MankaM..hapa hatuzungumzii ukweli..ila usiri na uwazi.

Hivyo vinaenda pamoja. Usiri utumike panajohitajika lakin pia uwazi unatumika mahali pake. nadhan uwazi ni mzuri sana lakin unatakiwa uwe na mipaka
 
Last edited by a moderator:
Kabla hamja jibu kitu hebu mrudi katika maandiko kwa kila mwenye imani haijalishi dhehebu hakuna maneno laana iliyo kemewa kama.kutoa siri ya ndani asa kama mungu amekemea na kuita ni laana asa kitugani mnacho taka kujadili na jambo lipo wazi na hii tabia ya kutoa siri za ndani waafrika tumeitoa wapi zaidi.ya kuwaiha westn wasiokuwa na dini wala mila wala desturi tuache tabia hizo za kuiha mbo yasio kwenda na utaratibu alio.tuwekea mfalme wa milele hata desturi zetu hazikubalinai nayo
 
Ila LILENDI kuna mambo mengine kuyatunza chumbani yanataka kifua haswaa...la sivyo unajikuta unayasema na mwisho wa siku kuishia kuwaza huyu mtu ashamwambia fulani na fulani...!usiri una faida zake..

Ulaya huko watu wanajiua sana kwa sababu hawana wa kumhadithia matatizo yao. Huku Africa tuna bahati ya kuwa na watu lukuki wa kuwaeleza matatizo yako wakasikiliza.... jirani, mfanyakazi mwenzio, saluni nk... Sometimes ukisema tatizo kwa mtu unakuwa kama umetua mzigo fulani hivi...
 
Last edited by a moderator:
Kiss our son for me...unatokka na hasira hukoo unaanza kumwagaa ooh jamani sijui huyu mwanaume hivi na vile hirizi kiunoni inapumua,ooh sijui ana hichi ana kile..kesho unamkuta shostiyo na mumeo samakisamaki.!ulale salama,

But unakuwa umeondoa stress za zamani... na kukaribisha mpya
 
Nilipitia Excel hata sasa kuna watu wanakufa kwa msongo wa mawazo kwa kutunza mambo mazito na ya kuumiza..

Marijan Rajabu aliimba hakuna komandoo wa shida... kuzifungia shida moyoni mwako ni kuzupa nafasi ya kukuumiza... zitoe watu wakusaidie kupambana nazo...
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom