UVCCM/Makonda hawajampiga Jaji Warioba

UVCCM/Makonda hawajampiga Jaji Warioba

mkuu, hawawezi, walijaribu wenyewe wakashindwa sasa wamekuja na nguvu ya UKAWA , bado wataishia kupigwa virungu tu.

Angalia. Wakati wanapigwa virungu ukae mbali. Manake fahari wawili wapambanapo ziumiazo nyasi. Unaweza ukawa wa mwisho kushangilia.
 
Wewe mbuzi na ccm yako mtahaibika vibaya. Kijana wenu aliyefanya uhuni wa kuandaa kundi la fujo kwa kulipwa na makonda haonekani chuoni mpaka sasa. Ninasoma nae darasa moja namba zake zimetajwa humu jf. Ujumbe aliokuwa akiusambaza mpaka sasa ninao. Soon naweka picha yake humu na atafukuzwa chuo baada ya kukamatwa na police atakapoonekana mazingira ya chuo. Na bado nyinyi sisiem mnakuwa wabishi kwa mambo mliyo yaandaa na kuyatekeleza wenyewe... Kijana wenu mpaka sasa hana chuo na kundi lake lote linasakwa.

Unatokwa povu kuitukana ccm, kwani aliyepigwa ni chadema?
 
Propaganda za ccm bhana,eti makonda alikuwa anamsaidia mzee warioba asipigwe!asipigwe na nani,ukawa au ccm?
eti mimi nilimsaidia mpachu asipigwe na kumsindikiza mpachu nyumbani!ww peke yako uliwezahe kuidhibiti mob ile yote isimpige mpachu,!?
kama unatunga uongo jaribu kuwa smart la sivyo unazidi ku disclose what you did that old mzee.
Eti makondo alumsaidia mzee warioba,of all the people makonda ndio atoke chini huku kwenda kumsaidia mzee,where was his gurds,police,au wajumbe wenzake,akina pole pole,butiku na watu wenye the same idiology kama yeye,you mean wote walimtelekeza mpaka makonda ndio akamsaidie?
pole sana kijana,bado upo shallow sana kwenye haya maswala,ukiwa shahidi wa huyu jamaa naweza nikakutwanga maswali mpaka ukakimbia.hopeless figure.
 
Kama mabango yalisema mmeisoma rasimu na kuielewa yanini mulifika ukumbini? jibu rahisi kwa mwelewa ambaye hana tamaa ya hela kama ilivyo kwa nyie mnaotetea ujinga na kuacha maslahi ya nchi mattani. Laana inawasubiri.
 
Mimi nikuulize swali. Wale walioshika mabango yanayoelezea kuwa katiba wameielewa na wenye maamuzi ni wananchi ndiyo wenye maamuzi ni vijana wa chadema? It doesnt make sence kama chadema wanaweza kufanya vurugu ilihali wao ndiyo wanaunga mkono maoni ya jaji warioba. Tell me
 
Vurugu zilianzishwa na Makonda hata akikataa vipi.Kwani hawezi organized watu halafu yeye akajifanya mtakatifu.Kule BMK kwenyewe alimtukana hayupo sasa pale yupo live ndio amuuonee huruma.
Huyu lazima laana zitampata huwezi taka mpiga babu yako upone.:A S-eek::A S-eek:
Kweli kizazi cha nyoka.

Kwanza lazima tujiulize swali muhimu: Huyo makonda alijikuta vipi pale ukumbini akimsikiliza Warioba ambaye amekuwa akimtukana siku zote? hapo mwenye akili hata kama ya mtoto wa miaka mitatu atajua kuna jambo.
 
kwani kuna sehemu MABANGO yaliwataja CHADEMA? na kwa nini useme CHADEMA na siyo UKAWA? hapa lazima kuna jambo unalijua unajaribu kukwepa, weka wazi wale walikuwa ni M4C waliojifanya CCM nini?

Kwa hiyo Makonda ni M4C maana ndio aliyeongoza hizo vurugu na Makonda alikimbilia kwa Warioba kama kinga yake hasiadhibiwe kwa alichokifanya cha kumrushia chupa Warioba.
 
Makonda Hajampiga Mzee Warioba.

Makonda alikuwa anasaidia mzee asipigwe Na aliomba Msaada huo wakusaidia Pasiwe Na Mapigano mule Ndani.

Vijana wa Chadema wamewapiga sana Vijana wa CCM wamepasuka mpaka sasa Jana Usiku Saa 3 ndio nilitoka kuwatoa Hospitali kutibiwa majerehara.
Vurugu ilianzishwa Na Vijana wa CDM Kwa Kuanza Kumpiga Mama aliekuwa amekaa Mbele Kabisa alipigwa Na Kuangukia ktk Jukwaa Kuu.

Picha inayosambazwa inamuonyesha Makonda Na Warioba Na Watu kusema Kuwa Makonda Alikuwa akimpiga Mzee Sio Kweli Bali Alikuwa Akimsaidia Kutoka Nje ambapo Makonda Na Warioba walikuwa wamejificha Pale Jukwaa Kuu Baada ya Viti Kuamza Kurushwa Ukumbini Pale.

Ndugu Amon Mpanju Alikuwa akipigwa Na Wahuni wa CDM Mimi Na Makonda Tumemtetea Asiumizwe kwani Ni Mlemavu wa Macho kwani Haoni Wapi Akimbie Na Afanye nini Lakini Vijana Hawa Walinishangaza Sana Kwa Kuona Vijana Hawana Nidhamu wala Heshima Wala Huruma yakuwaonea Walemavu Huruma.

Mpanju Katangaziwa Vita pale Ukumbini kuwa watampiga yeye Na Makonda Na Vijana Wengine Na Kweli walipigwa kama Askari wasingefika Pale Kiukweli Sijui Pangekuwa Na Mauwaji gani au Majeruhi Kwa Kiasi Gani.
Picha zinaonyesha Warioba Na Makonda kama wanavutana Move ile Walipokuwa wait oka Nje Na Askari walikuwa wakimchukua Warioba Na Kumficha sehemu ambayo Askari walimlinda, Makonda, Mpanju Na Wale Watoa Mada wote waliwekwa chini ya Ukinzi.

Baada ya Mdaharo Kuhairishwa Jaji warioba aliondoka Kwa kusindikizwa Na Askari akiwa Na Wenzie.

Makonda Aliondoka akiwa Na Askari pia .

Mimi Nilibakia na Amon Mpanju Aliekuwa Mjumbe wa Bunge LA Katiba toka Kundi LA Walemavu Amon Alikuwa akitishiwa Na Alipigwa pia.
Nilibakia Pale nae Na Kuhakikisha Kaondoka Salama Nilimpandisha Gari Na Kumsindikiza Nyumbani Kwake Akiwa Salama.

Nilifatilia Makonda kapelekwa wapi Nimesikitishwa sana Na Kitendo cha Kuona Makonda Kapewa Sifa mbaya yakumpiga Mzee Warioba Na Kusema Makonda Kaleta Vurugu Ukumbini, Na Vijana Walioleta Vurugu Na Kupiga Watu Wote Hawajakamatwa Na Wala Sijawakuta Kituoni.

Kuna Vijana Walikamatwa tulifanikiwa Kuwatoa Kituoni Na Kuondoka Nyumbani Na Walioumizwa walipata Matibabu Na Kuondoka Nyumbani pia.

Kinachofanyika si Chema Kabisa Kwa Taifa letu kwani tunapanda Mbegu ya Ajabu sana Na Itatusumbua sana kama Taifa.

Yuliona Libya walianza Hivi hivi Kimasihara Kwa kuwarubuni Vijana Kufanya Mambo yakishenzi Na Kihuni Na Kupiga watu wakafanikiwa Kuitoa Serikali iliyokuwa Madarakani Kwa Mapinduzi, Kitendo kile Mpaka Leo Kinaitafuna Libya vibaya Mno.
Nchi haijatulia Na Sidhani kama Itatulia kwani Hawajui Serikali ilifikia Pale Kwa Hekima Na Busara Zipi, Walioko Libya Leo wanajuta.
Nawasowasi Na Hizi Movement zinazoanzishwa Na Viongozi wetu Nchini Tanzania.

By Peter Dafi


Unaweza Kuona Picha hizi Ukitizama Kwa Maini utaona Makonda akimsaidia Amon Mpanju Mlemavu wa Macho.
Unaweza Kuniona Hapo Pia Nimevaa Koti la Dark blue nikisaidia Amon asiumizwe pia
Nawapa Angalizo tu.View attachment 198770


Moving Camera zilizokuwa zinaenda Live hazikuzimwa Ziliendelea Kurecord Matukio Yote Mule Ndani.
Sasa Mjiulize Kwanini ITV hawajaonyesha Makonda Na Vijana wa Chama Wakimpiga Warioba Na Kuleta Vurugu Mule?
Kwanini Watumie Picha tu za Still Na Video wasionyeshe.?View attachment 198772
What ever the case , mmekitia aibu chama chetu CCM kwa kutetea na kufanya fujo, mahali pa kutumia akili.
Na fujo hizo hazisaidii sana kuelezea umahiri wa katiba mpya.
SHAME ON YOU!
 
na hata video na picha za mnato zote hakuna sehemu zinaonesha Makonda akimpiga Waryoba, sijui uzushi huu unalenga kumfanya nini Makonda.

ndugu mimi nilikuwepo uctufanye wajinga. makonda kampiga mzee kweli.
 
Kama mabango yalisema mmeisoma rasimu na kuielewa yanini mulifika ukumbini? jibu rahisi kwa mwelewa ambaye hana tamaa ya hela kama ilivyo kwa nyie mnaotetea ujinga na kuacha maslahi ya nchi mattani. Laana inawasubiri.

Wote wamelaaniwa kutoka kwa mwenyekiti wao hadi mlamba viatu. Wanadai wameielewa, wamefuata nini pale ukumbini? Hata panzi ana akili kuliko hawa viumbe.
 
Kwa hiyo unadhani Siasa ya Kupigana ikianza mtabaki salama!!!!!.Lipumba ameshawahamasisha vijana wafanye mazoezi ya Viungo wewe unachochea kuni kwa kuunga mkono Waryoba kupigwa.Ni vizuri CCM mkaondoka madarakani kwa Amani bila kusubiri damu imwagike kwanza.
mkuu ccm haiwezi ikatoka madarakani bila damu za watanzania kumwagika kamwe!
 
Asante sana mkuu, kamwe tusikubali hawa wahuni kuja na uongo wao kisa tu wantetee huyo mhuni na mjinnga anayepiga wazee
Unajua hawa vijana wa ccm ni ovyo Sana mwanzo mwisho Mimi nipo kwenye tukio makonda baada ya hali ya hewa kuchafuka pale alikimbilia jukwaa kuu kujiokoa ndipo huyo jamaa ambaye huwa anahudhulia malumbano ya hoja Itv kumtoa jaji na mlinzi wa hotel akampokea mlangoni Kama unavyo ona kwenye picha na ndipo makonda akawa anajificha kwa pembeni kwa jaji warioba ndipo watu walipomchomoa nakumpa kichapo cha maana na sauti zilikuwa zikisikika huyu mpuuzi amekuja kuvuruga mdahalo wetu yani wamekula kodi zetu alafu analeta ujinga hapa piga ua kabisa huku watu wakimshushia kipigo kweli kweli.
Kwa ufupi ccm wamepoteza dira
 
Wwe na vilaza wenzio ndo mnaweza kuamini ujinga wko mimi binafsi nimechunguza nimeona wwe kwanza ni muongo kwenye pic umesema unaonekana umevaa koti la blue light anaeonekana ni warioba acha kutafuta umaarufu kwanjia ya ujanja ujanja.
 
Wewe mbuzi na ccm yako mtahaibika vibaya. Kijana wenu aliyefanya uhuni wa kuandaa kundi la fujo kwa kulipwa na makonda haonekani chuoni mpaka sasa. Ninasoma nae darasa moja namba zake zimetajwa humu jf. Ujumbe aliokuwa akiusambaza mpaka sasa ninao. Soon naweka picha yake humu na atafukuzwa chuo baada ya kukamatwa na police atakapoonekana mazingira ya chuo. Na bado nyinyi sisiem mnakuwa wabishi kwa mambo mliyo yaandaa na kuyatekeleza wenyewe... Kijana wenu mpaka sasa hana chuo na kundi lake lote linasakwa.
mkuu kwa vile alitumwa na chama kilichopo ikulu atapewa chuo kingine! Chezea ccm wewe, hicho sio chama bali ni genge la mafia!
 
PeterDafi, kwamba makonda ndiye aliye mwokoa Warioba akamwokoa Mpanju........??? Nani aliye pigwa kwanza kati ya Warioba na Mpanju mpaka huyo muokoaji (makonda) apate muda wa kuokoa mmoja mmoja?
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom