UVCCM/Makonda hawajampiga Jaji Warioba

UVCCM/Makonda hawajampiga Jaji Warioba

kwani kuna sehemu MABANGO yaliwataja CHADEMA? na kwa nini useme CHADEMA na siyo UKAWA? hapa lazima kuna jambo unalijua unajaribu kukwepa, weka wazi wale walikuwa ni M4C waliojifanya CCM nini?
Mleta uzi amewataja chadema eti ndiyo waliokuwa wanawapiga vijana wa ccm. Kwa hiyo fuatilia huyu mtoa mada kuna kitu anachofahamu zaidi kwa sababu anawajua vijana wa ccm na pia anawajua vijana wa chadema. Lakini maswali yangu mbona hayajibiwi?

 
Makonda Hajampiga Mzee Warioba.

Makonda alikuwa anasaidia mzee asipigwe Na aliomba Msaada huo wakusaidia Pasiwe Na Mapigano mule Ndani.

Vijana wa Chadema wamewapiga sana Vijana wa CCM wamepasuka mpaka sasa Jana Usiku Saa 3 ndio nilitoka kuwatoa Hospitali kutibiwa majerehara.
Vurugu ilianzishwa Na Vijana wa CDM Kwa Kuanza Kumpiga Mama aliekuwa amekaa Mbele Kabisa alipigwa Na Kuangukia ktk Jukwaa Kuu.


Picha inayosambazwa inamuonyesha Makonda Na Warioba Na Watu kusema Kuwa Makonda Alikuwa akimpiga Mzee Sio Kweli Bali Alikuwa Akimsaidia Kutoka Nje ambapo Makonda Na Warioba walikuwa wamejificha Pale Jukwaa Kuu Baada ya Viti Kuamza Kurushwa Ukumbini Pale.

Ndugu Amon Mpanju Alikuwa akipigwa Na Wahuni wa CDM Mimi Na Makonda Tumemtetea Asiumizwe kwani Ni Mlemavu wa Macho kwani Haoni Wapi Akimbie Na Afanye nini Lakini Vijana Hawa Walinishangaza Sana Kwa Kuona Vijana Hawana Nidhamu wala Heshima Wala Huruma yakuwaonea Walemavu Huruma.

Mpanju Katangaziwa Vita pale Ukumbini kuwa watampiga yeye Na Makonda Na Vijana Wengine Na Kweli walipigwa kama Askari wasingefika Pale Kiukweli Sijui Pangekuwa Na Mauwaji gani au Majeruhi Kwa Kiasi Gani.
Picha zinaonyesha Warioba Na Makonda kama wanavutana Move ile Walipokuwa wait oka Nje Na Askari walikuwa wakimchukua Warioba Na Kumficha sehemu ambayo Askari walimlinda, Makonda, Mpanju Na Wale Watoa Mada wote waliwekwa chini ya Ukinzi.

Baada ya Mdaharo Kuhairishwa Jaji warioba aliondoka Kwa kusindikizwa Na Askari akiwa Na Wenzie.

Makonda Aliondoka akiwa Na Askari pia .

Mimi Nilibakia na Amon Mpanju Aliekuwa Mjumbe wa Bunge LA Katiba toka Kundi LA Walemavu Amon Alikuwa akitishiwa Na Alipigwa pia.
Nilibakia Pale nae Na Kuhakikisha Kaondoka Salama Nilimpandisha Gari Na Kumsindikiza Nyumbani Kwake Akiwa Salama.

Nilifatilia Makonda kapelekwa wapi Nimesikitishwa sana Na Kitendo cha Kuona Makonda Kapewa Sifa mbaya yakumpiga Mzee Warioba Na Kusema Makonda Kaleta Vurugu Ukumbini, Na Vijana Walioleta Vurugu Na Kupiga Watu Wote Hawajakamatwa Na Wala Sijawakuta Kituoni.

Kuna Vijana Walikamatwa tulifanikiwa Kuwatoa Kituoni Na Kuondoka Nyumbani Na Walioumizwa walipata Matibabu Na Kuondoka Nyumbani pia.

Kinachofanyika si Chema Kabisa Kwa Taifa letu kwani tunapanda Mbegu ya Ajabu sana Na Itatusumbua sana kama Taifa.

Yuliona Libya walianza Hivi hivi Kimasihara Kwa kuwarubuni Vijana Kufanya Mambo yakishenzi Na Kihuni Na Kupiga watu wakafanikiwa Kuitoa Serikali iliyokuwa Madarakani Kwa Mapinduzi, Kitendo kile Mpaka Leo Kinaitafuna Libya vibaya Mno.
Nchi haijatulia Na Sidhani kama Itatulia kwani Hawajui Serikali ilifikia Pale Kwa Hekima Na Busara Zipi, Walioko Libya Leo wanajuta.
Nawasowasi Na Hizi Movement zinazoanzishwa Na Viongozi wetu Nchini Tanzania.
Sasa ilikuaje vijana wa Chadema waanzishe vurugu halafu polisi wasweke vijana wa CCM.?
Na mlijuaje kua hao ni vijana wa CCM hadi mkaenda kuwatoa polisi Usiku Usiku.!
 
Watanzanaia hawawezi kuacha WARYOBA na WANAHARAKATI wanaligawa taifa vipande vipande eti kwa kuogopa kuambiwa wanakimaliza chama, 2015 tutaona nani anakwisha CCM au UKAWA, manake CHADEMA imeshakufa, bado UKAWA.

Kwa hiyo unadhani Siasa ya Kupigana ikianza mtabaki salama!!!!!.Lipumba ameshawahamasisha vijana wafanye mazoezi ya Viungo wewe unachochea kuni kwa kuunga mkono Waryoba kupigwa.Ni vizuri CCM mkaondoka madarakani kwa Amani bila kusubiri damu imwagike kwanza.
 
Hoja dhaifu haijibiwi. Jitegemee kimawazo na kifikra. Usitumike
Hembu yaorodheshe hapa mambo makuu 4 yaliyoondolewa na BMK kwa mujibu wa Warioba alivyosema jana!na lipi liliwaudhi wanaccm la uchochezi.Tuone kweli kama Nape hawatumii nyie vijana wa buku 7 thatha MSALANI
 
Last edited by a moderator:
kwa jinsi upepo wa katiba ulivyo cdm wanamuunga mkono mzee warioba wakati ccm wanamponda na kumdharau, kama makonda alikuwa anamuokoa jaji warioba asipigwe, je ni nan alitaka kumpiga au alimpiga jaji warioba kati ya cdm wanaomuunga mkono na ccm wasiomuunga mkono? mleta mada umesema vjana wengine walikamatwa na polisi ukaenda kuwatoa, ni vijana wa ccm au cdm? kwani watuhumiwa ndo huwa wanapelekwa polisi! bado huna hoja yenye mashiko ya kutuconfince ya kwamba makonda/ccm hawakuhusika kumfanyia fujo mzee wetu! kama ccm mmeshindwa kuheshimu mawazo ya jaji warioba ingawa yanatofautiana na mawazo yenu vp mtaheshimu mawazo ya lupumba, mbatia au slaa? vp ile dhana ya uongo ya nchi ye2 ina aman hivi ni kweli kuna aman kama m2 anamfanyia fujo waziri mkuu/jaji mkuu mstaafu? haya yote aliyataka 6, yeye ndo atakuwa chanzo cha machafuko! ahsanten.
 
Jamani mbona Chabruma amepotea Jukwani siyo kawaida yake Nyuzi kama hizi zipite bila kuweka neno! Si Bure.:A S 109:
 
Hoja dhaifu mno

😂😂😂😂 wewe mbona hutoi hoja hata moja????


Kazi kuandika sentensi zisizokuwa na mashiko😠😠😠😠😡😡😡😡😡😡😡
 
kwani kuna sehemu MABANGO yaliwataja CHADEMA? na kwa nini useme CHADEMA na siyo UKAWA? hapa lazima kuna jambo unalijua unajaribu kukwepa, weka wazi wale walikuwa ni M4C waliojifanya CCM nini?

Wewe mbuzi na ccm yako mtahaibika vibaya. Kijana wenu aliyefanya uhuni wa kuandaa kundi la fujo kwa kulipwa na makonda haonekani chuoni mpaka sasa. Ninasoma nae darasa moja namba zake zimetajwa humu jf. Ujumbe aliokuwa akiusambaza mpaka sasa ninao. Soon naweka picha yake humu na atafukuzwa chuo baada ya kukamatwa na police atakapoonekana mazingira ya chuo. Na bado nyinyi sisiem mnakuwa wabishi kwa mambo mliyo yaandaa na kuyatekeleza wenyewe... Kijana wenu mpaka sasa hana chuo na kundi lake lote linasakwa.
 
Acheni umbea ukwl umejulikana vurugu ziliratibiwa na huyo Makonda na Sitta, ccm nyie ndo mnaipeleka nchii kwenye vita, ila mm msimamo wng na ushaur NCHI HII YA TANZANIA CCM INAJIFANYA SN NDO WENYE NCHII HII NA MKO JUU YA SHERIA BILA YA KUCHAPANA HAKA KANCHI KAMWE HATUTAHESHIMIANA!! Ni heri aman inayopigania utu wa Mwanaadam kuliko aman inayopumbaza utu wa Mwanaadam na kuudhalilisha, Tuchapene tu ili tuheshimiane na ipo cku Nchi hii kuongozwa kwa ubabe na kauli za Viongoz wa CCM za kinafki huku wakisema piga tu kwl tutapigana ili tushike adabu, Pumbafu kbs, pumbafu si tusi ila ccm ni wapumbafu....
 
Vurugu zilianzishwa na Makonda hata akikataa vipi.Kwani hawezi organized watu halafu yeye akajifanya mtakatifu.Kule BMK kwenyewe alimtukana hayupo sasa pale yupo live ndio amuuonee huruma.
Huyu lazima laana zitampata huwezi taka mpiga babu yako upone.:A S-eek::A S-eek:
Kweli kizazi cha nyoka.
 
Nadhani mletamada ni mwanachama wa kuajiriwa na unaijua CCM kwa barazani tu. Warioba ni Makamo wa kwanza wa Rais na PM mstaafu wadhifa ambao si Sitta wala Lowasa aliyeufikia. Kitendo cha mtoto makonda kimemwingiza kwenye kumbukumbu za kiserikali kama mtu hatari na humtofautishi na yule ALIYEMSOGELEA JK na kumvuta MGUU pale kirumba. Na usidhani kwa kitendo hiki serikali itamchekea hata kama iko kimya hadi sasa!
 
By Peter Dafi


Unaweza Kuona Picha hizi Ukitizama Kwa Maini utaona Makonda akimsaidia Amon Mpanju Mlemavu wa Macho.
Unaweza Kuniona Hapo Pia Nimevaa Koti la Dark blue nikisaidia Amon asiumizwe pia
Nawapa Angalizo tu.View attachment 198770


Moving Camera zilizokuwa zinaenda Live hazikuzimwa Ziliendelea Kurecord Matukio Yote Mule Ndani.
Sasa Mjiulize Kwanini ITV hawajaonyesha Makonda Na Vijana wa Chama Wakimpiga Warioba Na Kuleta Vurugu Mule?
Kwanini Watumie Picha tu za Still Na Video wasionyeshe.?View attachment 198772

Hiki KISA kinafurhisha na ni kizuri kama kitasimuliwa kwa watoto wadogo.

Mtu (Makonda) aliyeratibu vurugu, kwenda kumsaidia mtu(Warioba) ambaye vurugu hizo alikuwa anamlenga yeye!?

Kweli CCM ina SPIN DOCTORS sawa na akina El-Sahaf (Yule waziri wa habari wa Saddamu Hussein)
 
Back
Top Bottom