SoC03 Utumishi wa Umma: Je, muda umefika sasa wa mwananchi kuwa na nguvu ya kisheria kumtoa mtumishi asiyewejibika ipasavyo?

Stories of Change - 2023 Competition

Jerry Farms

Member
Jul 18, 2022
30
29
Mei mosi oyee!

Ajira katika utumishi wa umma imekua ni ndoto ya wasomi na wasio wasomi wengi hapa nchini, wengi wa watu hawa hulenga ama kupata kipato na wengine kuhudumu kwa kutoa huduma takwa na wananchi. Serikali kwa kulitambua hilo imekua ikitoa ajira za muda mrefu ama muda mfupi lengo likiwa kuweza kukithi malengo pangwa ya kimaendeleo nchini, katika ajira hizi hupatikana watu wenye kariba na tabia mbalimbali.

Mwananchi pasi na hiyana punde ahitajipo huduma husogelea ofisi za umma akiwa na lengo la kupatiwa huduma ahitajiyo, hapa ndipo hukutana na watumishi aina mbili.

MTUMISHI MWENYE MAADILI NA KUWAJIBIKA IPASAVYO
Hawa ni aina ya watumishi walioingia katika utumishi kipaumbele namba moja ikiwa ni kutoa huduma pasi na ubaguzi wa ki hali, kidini, kiitikadi na kimlengo. Hawa nawapewe kongole kwao.

MTUMISHI ASIYE TENDA KAMA APASAVYO KUTENDA
Hawa ni aina ya watumishi waliojaa kiburi, husda na wasiojali nini kimewaweka maofisini. Watumishi aina hii wamekua wakilalamikiwa na wananchi kwa ukubwa tambuka. Idara mbali mbali za umma zimekua zikilalamikiwa na wananchi mfano baadhi ni pamoja na; Ardhi, ulinzi, afya usafirishaji n.k.....katika idara hizi hali ya ubadhirifu, rushwa na upendeleo vimekua vikitajwa wazi wazi na wananchi pamoja na ofisi ya mkaguzi mkuu wa serikali( rejea machapisho mbali mbali ya ofisi ya CAG).

SULUHISHO
Yafuatayo ni baadhi ya mapendekezo ya nini vifanyike kutatua changamoto za uwajibikaji duni wa watumishi wa umma na watumishi katika sekta binafsi.

MKATABA WA KISHERIA KATI YA MUAJIRIWA NA MUAJILI(SERIKALI NA MWANANCHI)
Mkataba huu usiwe tu unaohusisha pande mbili yaani serikali na mtumishi bali sasa umpe nguvu ya kisheria mwananchi ya kumtoa katika utumishi wa umma yule asiyetenda kwa kadri ya makubaliano. Hapa paundwe mfumo rasmi utakaomuwezesha mwananchi kujua hatua stahiki anazopaswa kuzifata pindi mtumishiwa umma anaposhindwa kutoa huduma stahiki. Mfumo huu uwe wa wazi na elimu itolewe kwa mwananchi ili awe na ufahamu wa hatua tajwa.

MWANANCHI AWE NA NGUVU YA KUSHTAKI NA KUDAI FIDIA PINDI APATAPO HASARA KUTOKANA NA UTOLEWAJI WA HUDUMA HAFIFU
Hii itawafanya watumishi kuzidisha umakini zaidi katika utoaji wa huduma kwa wananchi, boss wa mtumishi wa umma awe ni mwanachi mwenyewe na si nguvu ya kuwawajibisha watumishi kuachwa kwa wanasiasa na baadhi ya watu.

UTARATIBU WA KUSHUSHWA CHEO AMA KUHAMISHWA KITENGO KWA MTUMISHI GOIGOI UFUTWE
Kumekua na kasumba na zoea la kuhamishwa kwa watumishi toka ofisi/mkoa mmoja kwenda mwingine pindi muhusika anapoonekana kutotosha katika nafasi pangwa. Zoea hili si afya saana katika utumishi wa umma hivyo serikali inapaswa kuachana na taratibu hii, pindi mtu anapoharibu basi iwe ndio mwisho wa uhudumu katika ofisi.

NAFASI KATIKA BAADHI YA OFISI ZA UMMA ZITANGAZWE NA WANANCHI WOTE WENYE SIFA WAOMBE NA KUPITISHWA NA WANANCHI WENYEWE
Baadhi ya ofisi za umma mfano; bodi za maji, mazingira, bodi za mashirika ya umma, ukuu wa wilaya, ukuu wa mikoa nakadharika. Visiwe vya kuteuliwa kama ilivyo sasa bali uundwe mfumo rasmi wa kuwapa nafasi wananchi kuomba na kupewa ridhaa kuongoza katika taasisi mbali mbali za umma.

PAWEPO NA UKOMO WA UTUMISHI WA UMMA
Hapa patauma kidogo kwa baadhi ya watu! Hasusani wale waliowahi kuhudumu katika taasisi ama vitengo mbalimbali vya umma! Ukomo huu utasaidia kutoa nafasi ya mawazo mapya na sura mpya katika utumishi waumma. Kasumba na taratibu ya mtu alikua kitengo ABC baada ya kustaafu anapewa jukumu jipya kiachwe na kutoa nafasi ya watu wengine na wao kuingia na kuhudumu. Dhana ya kustaafu utumishi wa umma iheshimiwe.

MOTISHA KWA WATUMISHI WAWAJIBIKAO IPASAVYO
Motisha hii inaweza kuwa ya kupandishwa vyeo, posho nakadhalika. Nafasi kama ukurugenzi, ukatibu, uenyekiti n.k zitolewe kwa wale watumishi wanaoonekana kuwa na sifa ya kielimu na kuhudumu kwa muda mrefu na kwa viwango katika halmashauri husika.

Mwisho, utumishi wa umma ni huduma yakihaki kwa mwanchi...shime kwenu watumishi kuwajibika ipasavyo kutetea maslai ya waajiri(wananchi) na kuyafikia malengo ya kimkakati ya maendeleo kwa woote! Assalamu.
 
Ulichokinena ni sahihi kabisa.

Wasiwasi wangu tu ni kwanba isijekuwa tunachopambana nacho ni culture tu yaani, desturi za mbongo kiujumla.

Mfano: wamiliki wa mabasi mikoani to dar, kuchukua nauli yangu ya Dar hata wasinifikishe Dar nnaishia Moro huko sio kukosa uwajibikaji.
Madalali nao.
Wapiga debe.
Mkulima anayedai ruzuku ili alime ila akishalima auze anavyojua yeye bila kuwajibika kwa yeyote.
Serikali isiyotoa ruzuku halafu watu wajianzishie vya kwao ije kudai kodi na kuwapangia tena.

Wananchi wanayaona haya na hawapigi kelele wanaona ni kawaida basi hizo ndizo desturi mbaya nnazozungumzia.


Suluhisho kwa upande wa elimu kwa mwananchi kama ulivyoongea ni muhimu sana. Tena elimu itolewe kwa maana halisi ya elimu yaani kutamadunisha na kustaarabisha.

Kura yangu unayo.
 
Back
Top Bottom