Stories of Change - 2023 Competition

Dave4148

New Member
Jun 1, 2023
1
0
Uwajibikaji ni maana ya ule wajibu wa kuhakikisha kuwa watumishi wa umma na viongozi wanawajibika kwa vitendo na wanawajibika kwa matendo yao kwa watu wanaowahudumia. Uwajibikaji umekuwa ni muhimu sana kwa kuboresha utawala bora kwa nchi yetu ya Tanzania, hii inatokana na mambo ambayo viongozi na watumishi wa umma wanapaswa kuyaangazia mojawapo ikiwa ni uwazi. Serikali imeanzisha mfumo wa tathmini ya utendaji kazi na mfumo wa malalamiko ambayo inahakikisha kwamba watumishi wa umma wanafanya kwa ufanisi kazi zao na kuwajibika kwa matendo yao ya kila siku. Lengo ni kuimarisha uwajibikaji na kuhakikisha kuwa watumishi wa serikali na viongozi wengine wanawahudumia wananchi kwa ufanisi.

Uwajibikaji ni jambo la muhimu sana serikalini na taasisi zake, kwani inapaswa kuhakikisha watumishi wake wanafanya kazi kwa uadilifu na kwa ufanisi huku wakiwajibika kwa matendo yao,Ofisi ya Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa zinapaswa kufanya kazi yake kwa ufanisi ili kuwawajibisha watumishi wa umma watakaobainika kukiuka masharti na maadili ya utumishi wao.

Hili kuhakikisha kuwa wananchi wanapata huduma bora na haki zao zinaheshimiwa na kulindwa, uwajibikaji wa watumishi wa serikali na viongozi wengine ni muhimu sana. Hii ni dhana ambayo uhusisha wajibu wa mtu au Taasisi kufanya kazi zake kwa uadilifu, uwazi na ufanisi na kuhakikisha uwajibikaji wao kwa vitendo.Serikali inapaswa kufanya kazi kwa uwazi sana katika utoaji wa taarifa zao na maamuzi yake kwa wananchi. Kwa kufanya hili watawawezesha wananchi kupata taarifa sahihi na kufanya maamuzi sahihi kuhusu masuala mbalimbali yanayowahusu wao kwa wao kuhusu maisha yao ya sasa na ya baadaye. Uwazi kwa utoaji wa zabuni na mikataba inayotiwa saini na serikali, ili kuhakikisha kuwa hakuna rushwa ama ubadhirifu wowote wa fedha za umma utakaofanyika

Serikali ina wajibu wa kuweka mfumo imara na iliyo madhubuti ya uwajibikaji ili kuhakikisha kuwa watumishi wa umma wanawajibika ipasavyo kwa matendo na sio kwa maneno, wanapinga dhuluma na rushwa. Hii inatakiwa uwepo na mfumo imara wa tathmini ya utendaji kazi ambao utawawezesha watumishi wa umma na viongozi wengine kujua jinsi wanavyofanya na kutekeleza kazi zao na kupata marejesho kuhusu utendaji wao.

Uwepo kwa mfumo wa malalamiko, na kupata mrejesho kuhusu utendaji wao,huu ni mfumo ambao unawezesha watumishi na wananchi kwa ujumla kutoa maoni au malalamiko yao kuhusu ubora na upungufu wa huduma mbalimbali za umma wanayoipata.

Uwajibikaji wa viongozi wa kisiasa ni sehemu kuu ya kuleta maendeleo katika jamii na kuuza demokrasia ya nchi, hii inapaswa kuwa viongozi wa kisiasa wanawajibika kwa wananchi wao na kuhakikisha kuwa wanafanya kazi zao kwa uadilifu na ufanisi zaidi ili kuleta umoja na maendeleo kwa watu. Hawa pia viongozi wa kisiasa anapaswa uwajibika kwa matendo yao hususani yote yaliyo sehemu ya utendaji kazi wao uliyowekwa kisheria kwa kuyapa kipaumbele na kupiga aina zote za matendo yasiyokuwa ya haki mbele za sheria.

Uwepo kwa uboreshaji wa mfumo wa uwajibikaji, ambao utawalazimisha viongozi wa kisiasa na watumishi wa umma kufanya kazi zao kwa uwazi, ufanisi na uadilifu,na kutoa adhabu kali kwa wore watakaobainika kukiuka maadili ya utumishi wa umma au kufanya vitendo vya ufisadi mfano hai ni kuanzishwa kwa mahakama ya kupambana na Rushwa mwaka 2015.

Pamoja na uwepo na uwajibikaji kwa viongozi wetu wa kisiasa katika kuilinda na kutetea hilani zao na watumishi wa umma kusudi kuwanufaisha wananchi mfano maboresho ya elimu, mahakama, Hata hivyo, bado changamoto kadhaa katika utekelezaji wa uwajibikaji katika utawala bora nchini Tanzania zinajidhihirisha. Baadhi ya changamoto hizo ni pamoja na

Ukosefu wa uwazi katika utoaji wa taarifa za umma, kumekuwepo na taarifa nyingi wakati wa utoaji na utekelezaji wa hizi huduma za watumishi kutokuwa na uwazi. Kuondokana na hili serikali Kuondokana na hili serikali inapaswa mfumo wa Usimamizi wa fedha za umma (IFMS) na mfumo wa taarifa za kiuchumi na kijamii nchini (SESRIC) ambao lengo lake ni kuboresha upatikanaji wa takwimu za kiuchumi na kijamii nchini.

Rushwa na ufisadi, katika kupambana na rushwa serikali imefanikiwa kuanzisha mahakama inayoshughulikia vitendo vyote vya rushwa na ufisadi ambapo inapaswa kuwawajibisha viongozi wote watakaobainika kufanya vitendo vya ubadhirifu wa fedha za umma. Hii itapaswa kuwa serikali kupitia chombo kinachosimamia manunuzi ya umma(PPRA),kuweka utaratibu madhubuti na sheria kali zitakazowezesha kuhifadhi taarifa na kutoa taarifa sahihi kuhusu manunuzi na matumizi ya umma.

Upungufu wa rasilimali za kutosha katika taasisi za udhibiti, kuboresha mfumo wa kielekteoniki wa usimamizi wa rasilimali watu kutaongeza uwajibikaji wa watumishi wa umma. Sera hii ya Taifa ya usimamizi wa rasilimali watu katika utumishi wa umma kwa njia ya kielektroniki (HCMIS), inapaswa kuboresha usimamizi wa hizi rasilimali kwa maendeleo ya wananchi na nchi kwa ujumla.

Kwahiyo, ili kuboresha utawala bora nchini Tanzania, serikali kupitia Ofisi ya Raisi Menejimenti ya utumishi wa umma na Utawala bora inapaswa kuchukua hatua zaidi za kuhakikisha kuwa misingi ya utawala bora inazingatiwa ili kuwaletea mafanikio wananchi. Hatua hizo zinapaswa kujumuisha kuboresha uwajibikaji wa watumishi wa umma, kuongeza uwazi katika utoaji wa taarifa za umma, kuhakikisha ushiriki wa wananchi katika maamuzi yanayowahusu, kuimarisha utawala wa sheria, na kupambana na rushwa na ufisadi. Kwa kufanya hivyo, Tanzania itaweza kufikia malengo yake ya maendeleo ya kisiasa, kiuchumi na kijamii.
 
Back
Top Bottom