Kuteuwa Wakurugenzi nje ya Utumishi wa Umma hakupaswi kufumbiwa Macho

naggy

Member
Apr 27, 2011
97
152
Kimsingi, hakuna teuzi yeyote anayofanya Rais isiyokuwa na masharti. Wakurugenzi ni watumishi wa umma ambao ni permanent and pensionable. Wanatambulika kwenye muundo wa utumishi wa umma. Na sifa za kuwa mkurugenzi ni kuwa angalau umetumikia managerial position ya ukuu wa Idara kwa miaka mitano.

Makosa ya kuteua watendaji nje ya utumishi wa umma alianza nayo Magufuli, naona mama nae anaendeleza. Hii ni dhambi, inapaswa tuikemee kama ambavyo tulikemea DPW.

Mkurugenzi wa Tanesco alitoka nje ya utumishi wa umma. Tanesco imemshinda. Sasa wanamhamishia TTCL, si kwa sababu anaweza, bali hamna pa kumpeleka kwa sababu tayari kawa mtumishi wa umma wa ajira ya kudumu. Na mshahara wake hautashuka hata kama watampa kazi ya kufagia ofisi.

Huko halmashauri ni yale yale. Rais anateua mwenyekiti wa CCM kuwa mkurugenzi wa halmashauri. Kweli? Anajuwa kazi? Ana vigezo kwa mujibu wa utumishi wa umma na scheme of service? Kwa kawaida mkurugenzi anapaswa kuwa kawahi kuwa mkuu wa idara kwenye local government au hata kwenye madhirika ya umma. Sasa unaleta mtu kutoka nje. Inamaanisha watu waliopo ndani ya utumishi wa umma hawafai? Hii ni kuwadharau seniors walioko kwenye utumishi wa umma. Na kumbuka kwenye utumishi wa umma kuna succession plan. Mkurugenzi lazima aandae mtu ambae anaweza kushika nafasi yake kwa kuwa anamkaimisha na. Ndivyo utumishi wa umma unafanya kazi.
Sasa huyu wa kufundishwa kazi anawezaje andaa viongozi wengine? Remember, namna utumishi wa umma unafanya kazi ni tofauti kabisa na uongozi ktk siasa ama private sector.

Fikiria akaja Rais mwingine na akaona mkurugenzi huyu hafai, anamtengua. Atafanya kazi gani? Magufuli alikuwa anawatengua, anakaa kimya. Wanakaa kula mshahara bila kazi. Wakienda kuomba msamaha anawapa kazi nyingine kama ukatibu tawala. Ndo maana wage bill ilikuwa kubwa sana.

Jambo jingine, Mkurugenzi kupewa jukumu la kusimamia uchaguzi ni kwa sababu kikatiba mkurugenzi hapaswi kuwa kada wa chama chochote cha siasa. Sasa unamuweka kada, anawezaje kutenda haki?

Tukemee kwa nguvu zetu zote
 
Screenshot_2023-09-23-16-59-34-1.png
 
Madhara yaliyosababishwa na magufuli Tanzania yatadumu kwa miaka mingi sana. Tukisema wanasema tumefukuzwa kwa vyeti feki wakati wengi waliofukuzwa walikuwa ni watumishi hewa wa lumumba
 
Back
Top Bottom