Uteuzi: Rais Samia amteua Humphrey Polepole kuwa Balozi Malawi, Mchechu arudishwa NHC

Kuteuliwa na Mkuu Wa Nchi kumuwakilisha kama Barozi ni heshima kubwa, inawezekana isiwe nafasi kubwa kwako lakini inaonyesha imani kubwa aliyo nayo Rais kwako...
Sema broo pole pole hajachoma sindano ya covid 19 so ataendajee kule
 
Covid 19 was not there ndiyo maana JPM ana remain hero ktk vita hiyo ya kiuchumi ya Mabwanyenye na hata waliokufa ni kwa dhana walikufa kwa woga tu na wengine walitolewa sadaka kujustfy walichokuwa wanataka wakubwa.

Polepole aende tu kwa raha zake, ni shujaa na mbeleni wasipomkolimba anaweza kubwa kiongozi mkubwa Wa Nchi hii.
 
  • Thanks
Reactions: Ame
Nasubiri teuzi za ukuu wa mikoa kwa zitto, tundu na mbowe. Mama acha awatrain kwanza aone utendaji wao wa kazi kama unafaa waendelee.
 
Mbinu iliyotumika kuwapoteza lukuvi na kabudi ndio hii hii tu.

Mtu akipelekwa huko malawi sijui msumbiji huyo ndio basi tena
 
Nafikiri ni wakati sahihi hizi nafasi zitolewe matangazo ya wazi watu waombe.

Maana kwa staili hii ni kama hakuna watanzania wengine wenye sifa
 
Nehemia Mchechu NHC tena? Ni sababu zipi zilipelekea kutumbuliwa? Hazikuwa genuine?Hivi hakuna watanzania wengine?
Tushike lipi tuache lipi? Lakutumbuliwa ama la hakuna watanzania wengi? Nyoosha maelezo mkuu.
 
Rais Samia Suluhu amemteua Humphrey Polepole kuwa Balozi wa Tanzania nchini Malawi.

Sambamba na hilo Rais Samia Suluhu amemteua Shamsi Vuai Nahodha kuwa Mbunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Pia Rais Samia Suluhu amemteua Waziri Kindamba kuwa Mkuu wa Mkoa wa Njombe.

Kindamba alikuwa Mkurugenzi Mkuu wa TTCL na anachukua nafasi ya Mhandisi Marwa Rubirya ambaye amestaafu kwa umri.

Polepole na Kindamba wanatarajiwa kuapishwa kesho Jumanne tarehe 15 Machi 2022 Ikulu ya Chamwino Dodoma saa 04:00 Asubuhi.

Katika hatua nyingine Rais Samia Suluhu amemteua Nehemia Mchechu kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC).

Mchechu ambaye amewahi kuhudumu kwenye wadhifa huo, anachukua nafasi ya Dkt. Maulid Banyani ambaye atapangiwa kazi nyingine.

Pia amemteua Balozi na Mkuu wa Jeshi la Polisi (Mstaafu) Ernest Jumbe Mangu kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi Mamlaka ya Bandari (Tanzania Port Authority).

Na Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amemteua Peter Ulanga kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL).

Ulanga ni Mkurugenzi Mstaafu wa Mfuko wa Mawasiliano kwa wote (UCSAF).

Na Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amemteua Meja Jenerali John Julius Mbungo, Mkurugenzi Mstaafu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) kuwa Mwenyekiti wa Bodi wa Shirika la Meli Tanzania (MSCL).

View attachment 2150380
View attachment 2150479
WAZIRI NAPE NNAUYE ALIVYOTANGAZA UTEUZI WA HUMPHREY POLEPOLE

Anaenda kula kwa urefu wa kamba yake
 
Likizo akiomba si mpaka akubaliwe?
Hakuna mwajili anakataa kutoa likizo ya bila malipo! Tena kwa serikali nadhani itakuwa rahisi maana mbadala mfanyakazi tena balozi si wakuumuza kichwa siku hizi...kwa hiyo ikiwa vingenevyo basi kuna jambo linginelo...!!!ha ha haaa bado natania mjue!
 
Back
Top Bottom