Uteuzi: Rais Samia amteua Humphrey Polepole kuwa Balozi Malawi, Mchechu arudishwa NHC

Baraka Mina

JF-Expert Member
Sep 3, 2020
581
574
Rais Samia Suluhu amemteua Humphrey Polepole kuwa Balozi wa Tanzania nchini Malawi.

Sambamba na hilo Rais Samia Suluhu amemteua Shamsi Vuai Nahodha kuwa Mbunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Pia Rais Samia Suluhu amemteua Waziri Kindamba kuwa Mkuu wa Mkoa wa Njombe.

Kindamba alikuwa Mkurugenzi Mkuu wa TTCL na anachukua nafasi ya Mhandisi Marwa Rubirya ambaye amestaafu kwa umri.

Polepole na Kindamba wanatarajiwa kuapishwa kesho Jumanne tarehe 15 Machi 2022 Ikulu ya Chamwino Dodoma saa 04:00 Asubuhi.

Katika hatua nyingine Rais Samia Suluhu amemteua Nehemia Mchechu kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC).

Mchechu ambaye amewahi kuhudumu kwenye wadhifa huo, anachukua nafasi ya Dkt. Maulid Banyani ambaye atapangiwa kazi nyingine.

Pia amemteua Balozi na Mkuu wa Jeshi la Polisi (Mstaafu) Ernest Jumbe Mangu kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi Mamlaka ya Bandari (Tanzania Port Authority).

Na Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amemteua Peter Ulanga kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL).

Ulanga ni Mkurugenzi Mstaafu wa Mfuko wa Mawasiliano kwa wote (UCSAF).

Na Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amemteua Meja Jenerali John Julius Mbungo, Mkurugenzi Mstaafu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) kuwa Mwenyekiti wa Bodi wa Shirika la Meli Tanzania (MSCL).

ikulu_mawasiliano-20220314-0001.jpg


WAZIRI NAPE NNAUYE ALIVYOTANGAZA UTEUZI WA HUMPHREY POLEPOLE
 
Back
Top Bottom