UTEUZI: Rais Samia afanya uteuzi na uhamisho wa Naibu Makatibu Wakuu. Dkt. Msonde kulamba asali TAMISEMI (Elimu)

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan amefanya uteuzi na uhamisho kwa Naibu Makatibu Wakuu kama ifuatavyo:

Amemteua Dkt. Charles Enock Msonde kuwa Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa – TAMISEMI (Elimu). Bwana Msonde amechukua nafasi ya Bw. Gerald Mweli ambaye amehamishiwa Wizara ya Kilimo. Kabla ya uteuzi huu Dkt. Msonde alikuwa Mtendaji Mkuu wa Baraza la Mitihani Tanzania (NECTA).

Amemteua Dkt. Maduhu Kazi kuwa Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi. Dkt. Kazi amechukua nafasi ya Bwana Ramadhani Kailima aliyehamishiwa TAMISEMI. Kabla ya uteuzi huu Dkt. Kazi alikuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji (TIC).

Bwana Ramadhan Kailima Kombweyi, Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi amehamishwa na kuwa Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais – Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), amechukua nafasi ya Dkt. Switbert Zakaria Mkama ambaye amehamishiwa Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira na Muungano).

Bwana Gerald Mweli, Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) amehamishwa na kuwa Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Kilimo.

Dkt. Switbert Zakaria Mkama, Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais – Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) amehamishwa na kuwa Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Makamu wa Rais, amechukua nafasi ya Bwana Edward Gerald Nyamanga ambaye atapangiwa kazi nyingine.
 
NECTA itakuwaje sasa? Maana ukitaja neno Msonde unaiona NECTA hiyo hapo.
Wanaleta baragashea kama walivyofanya sekretarieti ya ajira. Nakuonya Balozi Hussein Katanga wacha njama zako unazoendelea nazo za sectorolization katika utumishi wa umma.
 
NECTA yatakiwa ijitegemee binafsi, iwe na sera za muda mrefu na mfupi...
Hii kukaririsha watoto haina msaada kwa muda mrefu
 
Kuondolewa kwa Msonde Necta kunaweza kuleta maswali mengi sana ikiwa hata mbadala wake hajajulikana ...Msonde ameibarand Necta vizuri hatusemi akae pale milele lakini kimsingi ni kama kuna siasa kwenye elimu ni kama vile Rais anajaribu kuwaridhisha watu fulani walio kuwa wanailalamikia Necta ya Msonde!

Hii sio promotion ni kama kushushwa cheo vile kule anakwenda kupewa maelekezo tuu...

Utendaji wa Msonde Necta ulikuwa wa kutukuka sana
 
Visiwani huwa wanalalamika hawajawahi kuongoza kwenye matokeo na wakati hawataki shule
 
Why ?.

Hiyo necta aliikuta na kuna siku angeondoka tu
Amechangamsha sana necta kwa kuleta Mabadiliko makubwa mfano;
1.Mitihani ya competence based.

2.Kutumia mbinu ya kubadilisha mitihani sio kama zamani mtihani unajulikana mwezi kabla lakini Ktk kipindi chake kuna kuwa na mitihani karibia mitatu au zaidi ya mwaka husika halafu pepa la siku linachaguliwa siku ya mtihani au karibia.

3.Mwaka jana kulikuwa na mtindo mpya wa ufanyaji wa mitihani ya practicals hakuna ile ya mwalimu kupewa specimen na muongozo unatolewa asubuhi na mitihani inachelewa mpk saa 3 au 4 .Tofauti na zamani mwalimu anapewa muongozo siku moja kabla ya mtihani na kusababisha mitihani ya practicals kuvuka usiku mpk ikazoeleka kwa wanafunzi kwamba practicals uhakika ukifeli mzembe/

4.Nk
 
Kuna mahali fulani fulani nimesikia kuwa msingi wa huu uteuzi umekaa kimkakati wa BAKWATA!

Kuna mgalatia alikuwa anang'olewa pale NECTA ili mfilisti awekwe pale, halafu ile michezo ya kuwabeba wanafunzi wa dini fulani ili kwenda sambamba kwa pamoja kiwiano iende fresh. Hizo hamisha hamisha zingine ni kuzuga tu ili wajinga wasielewe mchezo kirahisi.

Alianza Profesa Joyce kutolewa pale wizara ya elimu, sasa amefuata Dr. Charles kuondoka pale NECTA........

Mama endelea hivyo hivyo kuupiga mwingi mpaka akili za walishwa mashonde na divai ziwakae vizuri.

dini fulani miaka yote shule zao zina bebwa wana kuwa top 10 kumbe mitihani wanapewa sasa tunataka tuone watoto wenye akili sio kupewa mitihani
 
Nikupe hongera sana rafiki yangu na ndugu haswaa dkt msonde kwa kupata uteuzi huu leo...dkt msonde wewe ni mchapakazi kwa hili halina upinzani..nani asiefahamu kuwa dkt msonde ulipokuwa necta umekuwa unapambana hasa na suala la wizi wa mitihani..na hiki ndicho kilichofanya wewe upate uteuzi, umekuwa ukijitoa kwa kufanya kazi bila kuchoka, ..dkt hapo TAMISEMI kuna uozo mkubwa kuna watu wanaitwa vishoka, ondoa vishoka wa ajira.....kwamba mtu hawezi kupata ajira mpaka awe na connection na mtu mkubwa hapo TAMISEMI..kwamba huwezi kupata ajira mpaka utoe chochote..wapo jamaa hapo utawaona tu wanapenda kuvaa shati za mtumba na kuchomekea kwa suruali za kadeti haisee hao jamaa wana njaa kwelikweli..DKT MSONDE TUNAOMBA UWAONDOE VISHOKA WA AJIRA ZA SERIKALI ILI WADOGO ZETU NAO WAPATE HAKI YA KUAJIRIWA...
 
Nikupe hongera sana rafiki yangu na ndugu haswaa dkt msonde kwa kupata uteuzi huu leo...dkt msonde wewe ni mchapakazi kwa hili halina upinzani..nani asiefahamu kuwa dkt msonde ulipokuwa nacte umekuwa unapambana hasa na suala la wizi wa mitihani..na hiki ndicho kilichofanya wewe upate uteuzi, umekuwa ukijitoa kwa kufanya kazi bila kuchoka, ..dkt hapo TAMISEMI kuna uozo mkubwa kuna watu wanaitwa vishoka, ondoa vishoka wa ajira.....kwamba mtu hawezi kupata ajira mpaka awe na connection na mtu mkubwa hapo TAMISEMI..kwamba huwezi kupata ajira mpaka utoe chochote..wapo jamaa hapo utawaona tu wanapenda kuvaa shati za mtumba na kuchomekea kwa suruali za kadeti haisee hao jamaa wana njaa kwelikweli..DKT MSONDE TUNAOMBA UWAONDOE VISHOKA WA AJIRA ZA SERIKALI ILI WADOGO ZETU NAO WAPATE HAKI YA KUAJIRIWA...
... shati za mtumba ...
 
Kumbe alikua NACTE? Naibu Katibu Mkuu ana influence gani?
 
Back
Top Bottom