Dkt. James Mataragio ateuliwa kuwa Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Nishati

BARD AI

JF-Expert Member
Jul 24, 2018
3,376
8,118
IMG_20240221_212139_225.jpg

UTEUZI: Rais Samia Sululu Hassan, amemteua Dkt. James P. Mataragio, kuwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini

Dkt. Mataragio anachukua nafasi ya Athumani Selemani Mbuttuka ambaye Uteuzi wake Umetenguliwa na atapangiwa kazi nyingine

Kabla ya Uteuzi huu, Dkt. Mataragio aliwahi kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC).

Disemba 2014, Dkt. James Mataragio aliteuliwa na Rais Kikwete kuwa Mkurugenzi Mkuu wa TPDC

August 2016 alisimamishwa kazi na Bodi ya Wakurugenzi ya TPDC

Julai 2019 Rais Magufuli Aliagiza arejeshwe kazini

Aprili 4 2021 alitolewa TPDC nafasi ikachukuliwa na Thobias Mwesiga.

Aprili 5 2021 aliteuliwa tena kuwa Mkurugenzi TPDC.

Februari 2023 alitolewa TPDC nafasi yake ikachukuliwa na Mohamed Makame na taarifa ilisema atapangiwa kazi nyingine.

Februari 2024 ameteuliwa kuwa Naibu Katibu Wizara ya Nishati.
 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan amemteua Dkt. James Peter Mataragio kuwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati.

Dkt. Mataragio aliwahi kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Mandeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) na anachukua nafasi ya Bw.
Athumani Selemani Mbuttuka ambaye uteuzi wake umetenguliwa na atapangiwa kazi nyingine.

57644939-e885-461d-9d3f-22f080c90c2d.jpg
 
Attachments

  • 57644939-e885-461d-9d3f-22f080c90c2d.jpg
    57644939-e885-461d-9d3f-22f080c90c2d.jpg
    80.4 KB · Views: 9
Naona mwamba karudi tena kitini baada ya kuharibiwa CV yake na wapika majungu wa CCM, JK alimtoa USA huyu jamaa akamleta TPDC kabla ya kuzinguliwa na JPM kisa mshahara wa 35m.

Tanesco ni fupa gumu sana linahitaji uchizi kudeal nalo, ukileta theory linakuaibisha mchana kweupe.
 
Yaani Wanazungushwa wale wale walioshindwa
Yani hapo ndio nashindwa kuelewa kwanini kwenye nchi yenye population ya watu zaidi ya milion 60

Linapokuja swala la teuzi wanaopewa nafasi ni walewale ambao tayari wapo kwenye vitengo vingine

Utaskia Steven wasila kateuliwa kuwa mkuu wa idara fulani. Huyu jamaa tangu kipindi cha Nyerere anateuliwaga tu.

Hii nchi hii we acha tu
 
Wasira ameanza kua mkuu wa mkoa wa Mara mwaka 1971, leo ni miaka 53 bado ni mtumishi wa umma.
 
Yani hapo ndio nashindwa kuelewa kwanini kwenye nchi yenye population ya watu zaidi ya milion 60

Linapokuja swala la teuzi wanaopewa nafasi ni walewale ambao tayari wapo kwenye vitengo vingine

Utaskia Steven wasila kateuliwa kuwa mkuu wa idara fulani. Huyu jamaa tangu kipindi cha Nyerere anateuliwaga tu.

Hii nchi hii we acha tu
Wasirra bodi ya parole akafie huko kama mrema
 
Naona mwamba karudi tena kitini baada ya kuharibiwa CV yake na wapika majungu wa CCM, JK alimtoa USA huyu jamaa akamleta TPDC kabla ya kuzinguliwa na JPM kisa mshahara wa 35m.

Tanesco ni fupa gumu sana linahitaji uchizi kudeal nalo, ukileta theory linakuaibisha mchana kweupe.
Ajirudie tu USA.... Maza hakuwa anataka pale. Alijaribu kumtoa mara ya kwanza kachemsha..
Safari hii alimfanyia mahesabu ya kumtoa bila kelele.
 
Yani hapo ndio nashindwa kuelewa kwanini kwenye nchi yenye population ya watu zaidi ya milion 60

Linapokuja swala la teuzi wanaopewa nafasi ni walewale ambao tayari wapo kwenye vitengo vingine

Utaskia Steven wasila kateuliwa kuwa mkuu wa idara fulani. Huyu jamaa tangu kipindi cha Nyerere anateuliwaga tu.

Hii nchi hii we acha tu
Hao ndio waliopo kwenye 'inner circle ' .
 
Back
Top Bottom