Rais Samia ateua Mtendaji Mkuu TANROADS na Naibu Makatibu Wakuu

benzemah

JF-Expert Member
Nov 19, 2014
1,504
3,034
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan amewateua wafuatao:-

1. Amemteua Mhandisi Rogatus Hussein Mativila kuwa Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais - TAMISEMI (Miundombinu). Mhandisi Mativila alikuwa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barbara Tanzania (TANROADS).

2. Amemteua Mhandisi Mohamed Besta kuwa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barbara Tanzania (TANROADS). Mhandisi Best ni Mkurugenzi wa Ufundi wa Wakala wa Usimamizi wa Usalama wa Usafiri wa Anga wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (CASSOA).

Mhandisi Besta anachukua nafasi ya Mhandisi Rogatus Hussein Mativila ambaye ameteuliwa kuwa Naibu Katibu Mkuu.

3. Amemteua Kamishna Benedict Wakulyamba kuwa Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Maliasili na Utalii. Kamishna Wakulyamba anachukua nafasi ya Bw. Anderson Mutatembwa ambaye amehamishiwa kuwa Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu); na

4) Amemteua Mhandisi Amin Nathaniel Mcharo kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya. Ushauri ya Wakala wa Barbara Tanzania (TANROADS).

WhatsApp Image 2023-06-13 at 14.38.11.jpeg
 
Ukiona uteuzi jua kuna kitu wanalenga.

Hapo unaweza kuta kuna barabara wanataka ipiga bei.

Tukae tayari.
 
#UTEUZI Rais @samia_suluhu_hassan amemteua Mhandisi Rogatus Hussein Mativila kuwa Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais TAMISEMI (Miundombinu). Kabla ya uteuzi huo alikuwa ni Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS).

#EastAfricaTV
FB_IMG_1686659851080.jpg
 
Mkurugenzi Mtendaji wa Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS), Mhandisi Rogatus Hussein Mativila amepata uteuzi kutoka kwa Rais Samia Suluhu Hassan.

0ead133e-5925-4bd1-8313-30dd7bfa3115.jpg
 
Kwa tunaoifahamu TANROADS hapo mamalaka ya uteuzi imevurunda.
Always, kama jeshi, mkuu wa TANROADS lazima atoke from within.
Kuna a big cycle of learning hapo.
Tusubiri madudu.
Mbarawa and co! mnaendelea na madudu.
 
Back
Top Bottom