Gamba la Nyoka
JF-Expert Member
- May 1, 2007
- 7,022
- 9,285
Watu wanasema ati kuna "hali ya dharura"; kwa miaka yote hii karibu ishirini hawajawahi kutangaza rasmi hali ya dharura. Wanachofanya ni kuliingiza taifa kwenye "mikataba ya dharura" bila kutangaza hali ya dharura. Huu ulikuwa ugomvi wangu na Lowassa alipounda ile tume ya dharura wakati wa Richmond. Hakuwa na madaraka hayo - isipokuwa Rais tu.
Hata leo hii, badala ya kumtaka Rais atangaze hali ya hatari ili ajirudishie madaraka aliyonayo kisheria na kuweza kuliondoa tatizo hili watu wamekubali kuahirisha mjadala ilii waje baadaye wazungumzeeeeee na Watanzania wafurahia " wabunge walikuwa wakali kweli". Ukweli uliopo mbele yetu ni kuwa hawataki kutangaza hali ya dharura kwa sababu wakifanya hivyo wanajifunga kisheria kutatua tatizo kwa haraka zaidi!
Mtu pekee anayeweza kufanya hivi ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye akitaka na akilazimishwa na wabunge anaweza kutangaza hali ya hatari kesho, keshokutwa akaigiza mitambo ya dharura, paid, owned and operated by the Tanzanin Government! Aidha kuna hali ya dharura kweli au hakuna - kama hakuna mnaweza kujivuta vuta taratibu na kukaa chini na vikamati, kuzungumza hadi mtondogoo kwani siku 21 ni kupoteza muda mwingi sana kwenye uchumi.
Sasa kumbe jibu liko wazi, Kama tatizo ni kwamba raisi hajatangaza hali ya hatari, je Ngeleja ameshamshauri Raisi kufanya hivyo?, kama hajamshauri kwa nini hajafanya hivyo? na hiyo inakuwa ni sababu ya msingi kabisa ya yeye kujiuzulu, kwa maana kwamba ameshindwa kumpa ushauri mzuri mheshimiwa raisi kutatua tatizo hilo. Hata hivyo pia kama ameshamshauri Raisi na Raisi amekataa ushauri wake au anajivutavuta ni sababu nyingine pia pia ya yeye Ngeleja kujiuzulu.
Excuse ya Kwamba Watanzania hatujawahi kuwa na umeme wa Uhakika kwa hiyo tusimwajibishe Waziri aliyekalia kiti hicho kwa miaka Sita ni ya kushangaza!, Watanzania bado tunakumbuka ahadi mbalimbali za ngeleja kutatua hili tatizo, lakini badala ya kupungua ndiyo kwanza linaongezeka, kutokana na Ngeleja kushindwa kutimiza ahadi zake za kutatua Umeme toka mwaka 2005 ni dhahiri hivi sasa anapaswa kujiuzulu.
Kiukweli kabisa serikali nzima ya JK inapaswa kujiuzulu , lakini Raisi kujiuzulu hilo jambo ni zito mno na ukichanganya na tatizo hili la umeme nchi inaweza kuyumba zaidi na hivyo Ngeleja inabidi ajiuzulu kwa niaba yao kwa kuwa kwanza yeye ndo mwenye dhamana ya umeme.
Ngeleja anaonekana hana vision, leo tuna mpango wa kuuza Uranium lakini hajaja na sera/mpango wa muda mrefu kutumia madini hayo kuzalisha umeme.
Ngeleja hana mpango wa kukidhi mahitaji ya umeme wa miaka 10 ijayo ambapo uzalishaji kutokana na viwanda na maongezeko ya mahitaji ya nyumbani kuwa yameongezeka kipindi hicho.
Ngeleja ameingia mkataba wa kuzalisha umeme na Symbion bila kufuta taratibu za procurement, kutangaza tenda na kushindanisha kampuni tofauti tofauti.
Hata raisi akitangaza hali ya hatari still Ngeleja ndo atakuwa incharge, kama ameshindwa kuja na japo ya kiduchu ya solution kwa miaka sita aliyokalia kiti cha wizara unategemea atakuwa na ugenius gani wa kutatua tatizo hilohilo in one to three months?.
I think Ngeleja should go