Umri sometime ni tatizo, inategemea na mwili wa mtu, mtaani kwangu kuna jamaa ana miaka 50 lakini mkewe tayari ni mzee na ukimkisia umri ni anaonekana kama yuko over 60, tusidanganayane hapa, wanawake waliowengi wanazeeka haraka after 45 of age.
What's your point mkuu, kwamba she aint fit for him? na kwamba ni afadhali aachane nae kwa kuwa wanawake wanazeeka haraka? Na umetoa mfano wa mtaani kwako, ila ungetuypa na background ya maisha yao ingekuwa poa, maana najua hali ya maisha inasabababisha hilo, so usitake kugeneralize.
Mi ni Me umri haujaenda sana
Nina mpenzi wangu ambaye tumekua nae katika mahusiano tokea tuko advance, mpaka sasa nna kazi baada ya kumaliza chuo kikuu, mpenzi wangu nae kamaliza chuo lakini vyuo tofauti ye yuko nchini mi Nafanya kazi nje ya nchi lakini maisha yangu kiujumla yako Tanzania.
Sasa hvi ameniweka kidete tuende kwa wazazi tukajitambulishe.. NAMPENDA.. lakini Kanizidi umri kwa miaka miwili. hili jambo linaniumiza sana akili.
Niliwaza kuvunja mahusiano.. lakini alikua ali react tofauti sana... Yeye nikimuuliza kuhusu future ya family na hii age difference anasema kwake haoni kama ni tatizo.
Lakini kwangu nahisi ni tatizo.. tena ambalo laweza kua hata kubwa zaidi baadae. kulingana na mazingira yangu ya kifamilia(wazazi)
Kichwa kinauma nimwacheje?... au kama kuna wazo mbadala!.. Tafadhali wanajamvi.
Okay mkuu, let us get back to the drawing board,
1. Mmekuwa pamoja tokea advance (2 years), na sasa umemaliza chuo kikuu (3 years) unafanya kazi. tuseme that is 5 years of being together.
2. Amekuwekea kidete mwende kwa wazazi. (of course miaka 5 sio kidogo kwa namna yoyote ile)
3. Unahisi tatizo la age difference linaweza kuwa kubwa baadae kulingana na mazingira ya familia yako, yaani wazazi. Lakini ujue anayeoa sio mzazi, na Biblicaly wewe unao na kwenda kuuanza mji wako, hutoishi na wazazi forever, but mke wako ndiye unaishi naye forever.
4. Unasema ulijipa hope ya kumuacha soon, ila sasa hali ni ngumu, kichwa kinakuuma umwacheje..
That signifies kwamba haukuwa na mpango naye, but rather 'part time'.
Kwa maelezo yote hayo niliiyasoma, naona ni kama kuna driving force behind, na si kigezo cha umri. Nina rafiki yangu amezidiwa 4 years na mchumba wake, and they are processing ndoa. Wewe miaka miwili unaona nongwa, ama hujui kwamba yuko matured enough kukulea wewe na watoto wenu.
kama naamua kutafuta teenage, hawa hawa ambao mostly wanahangaika na viblackberry na vi-iphone, then goodluck. Ila kama unataka mke mwema, ingia magotini muulize Mungu. Umri sio sababu kubwa, unaoa mtu, sio umri.
All in all, we huan beings do not know what we have until when it is gone, asipokuwepo ndio labda utaona kuwa alikuwa na uzuri wake, ambao hakuna mwenye nao, maana sijasikia ukisema kuwa ni kikojozi, kidokozi, fuska, kiruka njia, mlozi, nk.
All the best katika maamuzi yako, ila usisahau kwamba ni wewe ndiye unayeoa, sio wazazi, wala JF members. Hilo ni la kwako, pima na ufanye maamuzi sahihi brother.