Utatu wenye utata: Umri, Pesa na Mapenzi

Utatu wenye utata: Umri, Pesa na Mapenzi

Hao viserengeti boys ndio mnaelewana hata muandiko, mimi kwa muandiko huo tu you're total out of my favourite.

wanawake wenye miandiko hii ndio wale muda wote simu haziwatoki mkononi hata kama mmekaa sehemu mnatakiwa kushare maongezi na wengine.

ur not my favourite too!
 
Uoga wako tu, binafsi my special one nimemzidi umri lakini tunaishi vizuri sana na anajivunia kuwa na mimi, mimi pia sijawahi kujutia kuwa naye. Labda kama una sababu nyingine.
 
Issue ni kuheshimiana na kupendana. Ukiwa nae nani atajua ww mdogo yy mkubwa acha hz. Hy ndio habari ya mjini
 
Kuna saloon ninakwenda kusukwa nywele. Mmoja wa Wasusi wa pale amenizoea, alinipa namba yake akaniambia kama unataka kusuka nipigie simu tupange. Nilimpigia simu na tulipanga mimi niende kwake.

Anaishi kwenye chumba kimoja alichokipanga vizuri sana. Aliniambia anaishi na mume wake ambae ni kondakta mjini. Malengo yao ni mume kupata leseni ya udereva.

Tulipiga story za hapa na pale. Mume alirudi kutoka kazini. Bibi yule aliniomba radhi, alikwenda kumtengea mumewe chakula. Kwa heshima zote mume alinawishwa mikono baada ya ugali kuiva.

Baada ya kula mume alimsaidia mkewe kupanga nywele nilizosukwa. Tulipiga stori wakanieleza changamoto walizopitia kufikia pale. Niliwapa moyo kuwa ni wachache sana wanazaliwa na kukuta mali nyumbani wote tuna pigana.

Kwa kweli nilijisemea moyoni. Wawili hawa wanaishi kwa amani kuliko anaendesha vogue lakini amani nyumbani hakuna.
 
Nawashauri wale wote wenye mapenzi ya pesa waache mara moja coz huu ni mwaka mpya hivyo inabidi tuache mapenzi ya pesa.
 
Mapenzi ya pesa ndio aina gani ya mapenzi???
 
Akikupendea pesa na wewe mpendee kidude chake hapo inakua ngoma droo..
 
Mapenzi ya pesa! Ni ya ukweli na mazuri coz you will learn how to look for money and uphold your values! Mapenzi ya bure ni umalaya na ngono zembe coz you easily flatter around for no good reason!
 
Pesa jamani ndio kila kitu .. Bila pesa hakuna mapenzi trust me
Hawa walioleta msemo kuwa mapenzi sio pesa nia yao ni kufarijiana na kuulinda umaskini.. Ni kama wale wanaodai kuwa eti kibamia sio kero
Note:ceteris paribus
 
Back
Top Bottom