Utatu wenye utata: Umri, Pesa na Mapenzi

Utatu wenye utata: Umri, Pesa na Mapenzi

Na familia nyingi ambazo ziko vizuri ni zile ambazo mme na mke wameanza bila kitu na mwisho Mungu kawabariki na kujikuta wamefanikiwa sana....

Na ndoa za namna hii mara nyingi huwa zimebarikiwa sana tofouti na zile ambazo mke kaolewa kakuta mme ana mali na mara nyingi wanawake wa dizaini hii huwa na majivuno chungu nzima but ukija kwa reality kichwani hakuna kitu na ndoa za namna hii huvunjika bado zikiwa changa....


Kuna tofauti kati ya utajiri na kuweza kuendesha familia kwa mahitaji muhimu ya kifamilia na wakati huo ukiwa umejiwekea misingi ya maendeleo endelevu then hapo ao tu.

Sasa Kijana(Mvulana) unataka kuoa wakati hata kukimu mahitaji yako muhimu huwezi eti unataka uje kusaidiana mke wako watakusaidia kweli alafu uanze kulia lia.

Mambo makubwa ya kimaendeleo ni vizuri ukayatafuta ukiwa na mkeo kama msaidizi wako.

Lakini ukishindwa oa tu kijana katika yoyote na usubirie masimango ya mkeo huko mbeleni yaani ukimkosea kidogo tu anakumbushia unakusema alivyokuvumilia ulivyokuwa choka mbaya utasikia sasa hivi umepata unajifanya jeuri kumbe hakuna jeuri yoyote bali ni fimbo yake ya kukuchapia tu.
 
Sky Eclat hapo kuna upendo wa kweli sio wa kuigiza wenye tamaa na vitisho. wengi wanashindwa, wanafikiri wana nuksi, wana laana, hawapendwi lahasha akili zao ndio mbaya sana ila sio siri wengine wanalaana ila hawajui kama wana laana, akikutana na mwanaume anajua huyu anaweza akanioa ah haipiti siku jama anakimbia sasa huishia kusema kuwa wanaume wote wako sawa ni wababaishaji ni waongo sasa laana zako mi nizipeleke wapi ( kuna jinsi ya ku cross check kama mtu ana laana ni rahisi sana tu unafanya hivi......), mwanamke anataka kuolewa anapanga aina ya uwezo wa mwanaume anaye mtaka kisa eti anataka asilete aibu nyumbani kwao na kwa ndugu zake. msimamo wa mtu ni kutafuta maisha yeye na mumewe hata kam ni from the ground or scratch that's life. wengine wameshaanza kuzeheka wanabaki wanashusha umri wa kuzaliwa kisa kuchagua ila time will tell wewe una umri gani.

Kumjua mwanamke ni mkubwa au mdogo muangalie vidole vya miguuni kwa juu kuna sign utaziona na utajua rika lake nimeziweka kwenye mabano maana wengine watakuwa wanaficha ila kila mtu ajue hawezi kuficha umri, acheni kina dada mnachagua sana unataka mwanaume awe na uwezo mkubwa kifedha eti awe ana kazi yake nzuri ndio atanioa lol kwani kuoa ni lazima, mbona watu hawaoi na wanaishi vizuri na maisha yao tu au wanaishi kwa kipato kidogo na maisha yanaenda tu, kama unataka mwenye uwezo, mwenye pesa basi tafuta kwanza wewe zakwako halafu umtafute na mwenye nazo. SIKU HIZI NASIKIA MNAUA WANAUME ILI MBAKI MNAFAIDI MALI sijui ni kweli.
Koh koh
 
[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] kweli kabisa
Eeeh Kweli kabisa bora kuwa na mume wa mtu tu uinjoy Maisha,kuliko kuwa na mwanaume ambaye Hana hela anajifanya anakupenda akizipata anakukimbia [emoji12] [emoji12] [emoji12]
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]

Jamani vlad nimechekaaaa
Unajua nn Yna4 , kuna wadada kazi yao nikujiangalia ktk vioo miguu yao ilojaa,au makalio ,maumbo yalojaa. Yanawafanya wajihisi wao kua tmwanahitajika sana,kwaivo wao ktk mahusiano huamin muda wowote anapendwa na hana haja yakuangalia muda ,sasa basi mbwembwe atakaokua nazo hahahah.

Wanaume niwajanja sana. Hawaoi makalio wala sura wala mihips ....hujikuta wadogo zake alowaacha sekondar wanaolewa yeye bado akisoma namba.

Amini nakuambia. Wanawake waivo weng wao wanazalishwa tu....jarib kufatilia ndoa nyingi utagundua " Mama mwenye nyumba sio mzuri kwamwonekano" . Unahisi nikwann???

Kwasababu wanajielewa kua wao sio wazur hivo wanajitahidi kufanya vile mwanamme angependa .nahapo anamuwin kiurahisi kabisa.
 
Mwanamke ulieanza nae mbali siku moja mkafanikiwa tegemea haya!
Conflict of interest:hapa mwanamke ataona hadi umefika hapo ni juhudi zake hivyo huwezi kumfanya lolote.hapo kidume ataona hatari inamkaribia ya kuendeshwa km gari bovu!kitachoendelea nyumba itakosa amani.
Nyumba ikikosa amani michepuko lazima iingilie kati hapo jamaa atafarijiwa hadi amjengee mchepuko ili waje kuishi wote.ndio hapo utaanza kuskia mwanaume anakwambia nitaondoka hapa nikuachie kila kitu
 
Mimi kwa kweli mambo ya kumvumilia mwanaume nlishaacha,umenikuta na mali pesa njoo na zako uniongezee,ila zangu huzigusi,huna pesa tambaa tafuta wanaoweza kukuvumilia mambo ya kumvumilia halafu akipata anakuona hafai sitaki kabisa.
[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] amuuu
 
Mara nyingi hali ya umasikini kwa familia inaleta amani na upendo ,vilevile kuna familia zenye kipato cha kati na bado upendo na amani vinashamiri.Hata hivyo familia nyingi tajiri hazina amani wala upendo ,,,,,,
 
Kuna saloon ninakwenda kusukwa nywele. Mmoja wa Wasusi wa pale amenizoea, alinipa namba yake akaniambia kama unataka kusuka nipigie simu tupange. Nilimpigia simu na tulipanga mimi niende kwake.

Anaishi kwenye chumba kimoja alichokipanga vizuri sana. Aliniambia anaishi na mume wake ambae ni kondakta mjini. Malengo yao ni mume kupata leseni ya udereva.

Tulipiga story za hapa na pale. Mume alirudi kutoka kazini. Bibi yule aliniomba radhi, alikwenda kumtengea mumewe chakula. Kwa heshima zote mume alinawishwa mikono baada ya ugali kuiva.

Baada ya kula mume alimsaidia mkewe kupanga nywele nilizosukwa. Tulipiga stori wakanieleza changamoto walizopitia kufikia pale. Niliwapa moyo kuwa ni wachache sana wanazaliwa na kukuta mali nyumbani wote tuna pigana.

Kwa kweli nilijisemea moyoni. Wawili hawa wanaishi kwa amani kuliko anaendesha vogue lakini amani nyumbani hakuna.
Huu ni ukweli 100% .

Penye pesa Mapenzi ni 40%
 
Back
Top Bottom